CCM Yalaani vikali kitendo cha baadhi ya vyama vya siasa kuanzisha viashiria vya uvunjifu wa amani na mpasuko Zanzibar

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
CCM YALAANI VIKALI KITENDO CHA BAADHI YA VYAMA VYA SIASA KUANZISHA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI NA MPASUKO ZANZIBAR

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani vikali kauli za baadhi ya wafuasi, wanachama na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani Zanzibar kuanza kuhubiri mgawanyiko na kauli zenye kuashiria uvunjifu wa amani nchini.

Hayo yamesemwa Desemba 17, 2022 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, wakati wa mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi yaliyofanyika Mkoa wa Kusini Pemba.

"Chama Cha Mapinduzi kinalaani vikali vitendo vilivyoanza kujitokeza siku za karibuni hasa kisiwani Pemba kwa baadhi ya wafuasi, wanachama na viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa kuhubiri mgawanyiko kuchochea uvunjifu wa amani, sio utamaduni wetu wazanzibari, sio utamaduni wetu Watanzania, CCM inalaani vikali," amesema.

Video🕹️🕹️

===
 

Attachments

  • VID-20221218-WA0000.mp4
    12.8 MB
CCM inalaani vikali mpasuko huku inapora chaguzi kwa mtindo uleule wa siku zote! Katika kitu ACT walikosea ni kukaa meza moja na CCM kufanya maridhiano uchwara. Hao CCM inatakiwa watengwe moja kwa moja. Hakuna kushirikiana nao kuanzia misiba, sherehe, kwenye nyumba za ibada nk. Ni upuuzi kushirikiana na washenzi wasio na haya, wala kuona vibaya.
 
Back
Top Bottom