CCM yakiri watumishi wa Umma kuvujisha siri nyeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yakiri watumishi wa Umma kuvujisha siri nyeti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Aug 24, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145


  Na Rehema Mohamed

  KAMPUNI ya Brands International Limited imefungua kesi katika Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara ikiilalamikia Kampuni ya Usafirishaji Dar es Salaa (UDA) kwa
  madai ya kuingilia sehemu yake ya biashara.

  Kesi hiyo namba 68 ya mwaka 2011,ilifunguliwa Agosti 17 mwaka huu mahakamani hapo na ipo mbele ya Jaji Amiri Mruma.

  Katika kesi ya msingi,inadaiwa kuwa UDA na Kampuni ya Brands International Limited walikuwa na makubaliano ya upangaji eneo la UDA,lakini shirika hilo lilionekana kuvunja makubaliano hayo.

  Kutokana na hali hiyo,Kampuni ya Brands International Limited inaitaka UDA kulipa fidia ya sh.milioni 133,400,000 kama hasara iliyopata kwa kuvunjiwa ukuta.

  Pia inataka kulipwa fidia dola 16,493 kufia hasara ambayo kampuni hiyo ilipata kila mwezi kuanzia Julai 2010.

  Kesi hiyo jana ilitajwa mbele ya Jaji Mrumi kwa ajili ya kusikiliza maombi ya mlalamikaji.

  Hata hivyo kampuni ya UDA imeamriwa kupeleka mahakamani hapo hati ya kiapo kujibu maombi ya mlalamika kabla ya Septemba 9, mwaka huu.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 12, mwaka huu.
   
 2. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kwamba hiyo ccm yenyewe haijafanya utafiti kwa nini watumishi wavujishe siri. Kama wangejaribu hilo wangegundua kwamba hakuna hata mtumishi mmoja anyeridhika na jinsi nchi inavyoendeshwa na inavyoliwa wakati yeye anataabika. Ndiyo sababu anaamua kutoa siri ili mambo yawe hadharani.
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,130
  Likes Received: 6,621
  Trophy Points: 280
  ccm yenyewe haieleweki. na lazima iwafie tu,
   
Loading...