CCM yakiri mahudhurio mikutano ya Dr. Slaa yatishia uchakachuaji wa matokeo ya kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yakiri mahudhurio mikutano ya Dr. Slaa yatishia uchakachuaji wa matokeo ya kura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 9, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Kwa mara ya kwanza vyanzo vyangu vya habari ndani ya CCM vimebaini pamoja na CCM kujigamba watashinda kwa kishindo lakini kichinichini wameanza kujadiliana ya kuwa kipimo cha REDET kimeonyesha uvumilivu wa watanzania ni hafifu na hivyo wako tayari kuchakachua matokeo yatakayoonyesha JK na CCM imeshinda kwa asilimia kati ya 52 hadi 56.

  Lengo la marekebisho hayo yanatokana na wao kushindwa kuwaelezea watanzania juu ya mahudhurio kwenye kampeni za Dr. Slaa ambazo kwa mbali sana zimemfunika JK na CCM yake.

  Taarifa ndani ya chama hicho zimebaini ya kuwa matamshi yao ya asilimia themanini na zaidi kuwa JK atashinda ni kuwaandaa wapigakura kuja kuona hata CCM haikufanikiwa kama ilivyopanga na ya kuwa hakuna mshindi wa wazi kwenye chaguzi hii. Au kwa lugha nyingine hata wao CCM pamoja na kuitetea Ikulu "kimagendo" lakini umaarufu wao umeshuka sana. Watakuwa tayari kukiri hivyo baada ya uchaguzi ili kuwapooza Chadema na haswa Dr. Slaa.

  Njama hizo za kubaki Ikulu kinyume na matakwa yetu tunaweza kuzifuta kama tutajitoa mhanga na saa kumi na mbili jioni siku ya uchaguzi tukarudi vituoni vya kupigakura ili kujulishwa matokeo ya kura tulizozipiga.

  Hicho ndiyo kiama cha CCM na mbinu zao chafu za kubaki madarakani isivyo halali na kinyume cha sheria..............
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Nguvu ya umma basi tu mwaka huu ni mpaka wonq'oke
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  wamechelewa kuliona hilo . Siku za mwisho za kampeni hawataenda kamwe hata ccm wenyewe
   
 4. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  watakiri vizuri on the judgement day imean 31 octoba
   
 5. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #5
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  Asiyehudhuria midahalo hapati kura yangu
   
 6. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata hivyo nilishasema; jinsi siku za mwisho zinapokaribia ndio Dr Slaa atajipambanua i can see; hadi kuna msg za kihuni ambazo uzuri zinawaamsha watu wampigie hata wale ambao walikuwa hawamjui maana naona ujumbe ule ni mzuri tu hauna matatizo kwa mtu anayetafakari; kuna watu wawili wamepiga kwangu kuulizia habari za Dr Slaa; nikawaambia pamoja na kunua kitabu; dr Slaa ndiye anayefaa kuwa rais wa TZ; so kuna kura mbili zilijificha sasa zimefichuliwa na sms za miraji; safi sana
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Slaa kanyaga twende
   
 8. Kionambele

  Kionambele JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sababu moja tu ya kutilia shaka uhalisi wa stori yako ni jinsi unavyotilia shaka mada zingine ambazo ni za ki-espionage.

  Sikujua kwamba wewe ni mtungaji na mbunifu wa mada, kumbe ndio maana zinapoandikwa za kweli unadhani zimetungwa.

  Tutajie kwanza majina ya hao vyanzo vyako vya habari ndio tutakuamini.


  Anyway mkuu Ruta hayo hapo juu sio mawazo yangu, mimi nakukubali sana ila najua utakutana na hoja za kipuuzi kukupinga, nimezifuatilia sana kwenye mada mbalimbali, lengo lao hasa wanataka 'kumkombe' mtu.

  Nyie endeleeni kuzianika tu, kama mlivyowaanika REDET wiki mbili kabla hawajatoa matokeo yao ya kijambazi. Wananchi watajionea tu mbeleni.

  Nakugongea thanks nyingine hapa. Big up.
   
 9. R

  RMA JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa yes we can! :llama:
  Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.


  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!


  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini?


  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..


  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.


  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi?


  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!


  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Nani anabisha! Si tumeona alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekalia mawe? We must be serious!


  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu?


  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?


  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!


  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.
  :llama:

  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.

  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi.


  Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela.. :tonguez: :llama:
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  CCM ipo hooooi sasa.
  na hizo sms zao za chuki na kikaburu wanazozituma ndizo zinawamaliza kabisa.

  wameshatuma sms mbili tofauti kwenye simu zetu. lakini hatuwapi kura ng'ooo.
  Bora utawaliwe na shetani kuliko ccm
   
 11. N

  Nginana JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 774
  Likes Received: 635
  Trophy Points: 180
  CCM, what is all this fuss for? The draconian stance to steal the election is nothing but a recipe for anarchy. Is it worth it? Are there no sensible strategists at CCM? Losing an election is a direct consequence of failing to deliver on promises. It's a lesson. It's an unavoidable democracy check!
   
 12. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Iko mammbo mbili afya ya CCM siyo nzuri hata kidogo mpaka vijijini tunapata nyeti zote.
  1. watachakachua wananchi wasipolinda.
  2. 2015 mipango wa wapinzani ikoje? Elimu ya uraia bado inahitajika sana hata kwa wajanja wa DAR
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hata wapinzani wakishindwa mwaka huu 2015 ndio kiama cha CCM maana watu wameshaamka. Lakini hivi sasa wanaipata fresh maana kila wanachofanya ndio wanazidi kujiharibia wenyewe.
   
 14. m

  matawi JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Zumbemkuu avata yako imenipa raha sana ya kulala. Asante sana kwa leo
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280

  Huo ndio ukweli wa CCM leo na hauna ubishi wowote ule
   
Loading...