CCM Yakiri dhahiri kuelemewa kwa kasi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Yakiri dhahiri kuelemewa kwa kasi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ChescoMatunda, Sep 15, 2012.

 1. ChescoMatunda

  ChescoMatunda JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,189
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  CHAMA cha Mapinduzi (CCM), sasa kimekiri kuelemewa na wimbi la kukimbiwa na wanachama wake hususan vijana wanaojiunga na vyama vya upinzani baada ya kuona matarajio yao hayapatikani ndani ya chama hicho.

  Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Mbeya Dk. Steven Mwakajumilo pamoja na kukiri hali hiyo, alionya kuwa ikiwa chama hicho kinataka kuendelea kuungwa mkono, lazima kichukue hatua za makusudi za kukabiliana na hali ngumu ya maisha ya Watanzania.

  Dk. Mwwakajumilo alisema hayo juzi wakati akiendesha harambee ya mfuko wa vijana wa chama hicho, katika kata ya Ihyela, jijini Mbeya.

  Alisema kuwa vijana wengi nchini kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya kiuchumi, hivyo kuwakatisha tamaa.

  “Vijana wengi wamekimbilia upinzani pengine kwa kuona matarajio yao hayapatikani ndani chama, tunazo sera nzuri sana ndani ya CCM za kumkwamua kijana kiuchumi, lakini inawezekana wimbo tunaoimba ni tofauti na ule tunaoucheza,” alisema Dk. Mwakajumilo.

  Dk. Mwakajumilo ambaye pia ni mchumi na mtumishi wa Benki Kuu ya Tanzania alitoa wito kwa kila tawi la CCM mahali lilipo kujizatiti kwa kuanzisha vikundi vya vijana vya ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wa kiuchumi sambamba na kulipatia uwezo tawi husika kufanya shughuli za maendeleo ya chama.

  “Kila tawi la CCM mahali lilipo lijizatiti kuanzisha vikundi vya ujasiriamali, ndipo litakuwa na uwezo hata wa kujenga nyumba na ofisi za chama,” alisema Dk. Mwakajumilo.

  Dk. Mwakajumilo aliahidi kufanya operesheni ya kuanzisha vikundi hivyo vya ujasiriamali katika kila tawi la CCM ndani ya kata ya Ihyela jijini Mbeya ili kuonyesha mfano wa uanzishwaji wa vikundi hivyo. Chanzo GAZETI (Tanzania daima).
   
 2. m

  mmwaisoba JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 434
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania Daima ni Gazeti la Freeman Mbowe. Huyu bwana amekiri sawa na Shibuda aliposema CHADEMA kunaminyoo tu hakuna watu wa kuchaguliwa Urais. SASA HII JAMII FORUM SI YA KUWEKA PROPAGANDA MUFILISI. Kama vijana wamekimbilia CHADEMA na Slaa utamwitaje maana naye ni ajuza aliyetoka CCM kukimbilia CHADEMA. Hapana shaka CHADEMA INATAPATAPA BAADA YA KUHADAA WAFADHILI WAKE KUWA INGECHUKUA NCHI 2010 IKAANGUKIA PUA SASA INAWEWESEKA MZIMU WA ZITTO KABWE NA SHIBUDA.
   
 3. m

  mmwaisoba JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 434
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kichwa Cha habari hakifanani na yaliyoandikwa kwa huyu jamaa wa CHAGA DEVELOPMENT MANIFESTOS ALIYEWEKA HII MADA, TOA MADA SIYO
   
 4. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,964
  Likes Received: 6,735
  Trophy Points: 280
  Kunywa pombe kabla ya kula, ndiyo matokeo yake haya!!
   
 5. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tatizo lililopo ndani ya CCM yetu, hakuna hata mmoja wa kushaurika. Hapo Nikisubiri sawa na kumpigia mbuzi gitaa kwa ufundi wote.
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  wanadhani vikundi vya ujasiriamali ndo itarudisha vijana?
  Ccm inabidi ijisafishe taka zote, ije ikiwa safi nyeuoe ili wananchi waiamini, lakini kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ilhali imejaa taka haisaidii
   
 7. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ccm bye bye mbwembwe zote chini n ful kunuka!Wanajifanya wajuaaaji kumbe ni hamneni,kaz wanayo!.Tumewapa kaza wameshdwa kufanya na kuleta maendeleo,je tutawaaminije!?,wanakimbilia udini,ukabila na ukanda kuwachafua wenzao,ccm ni dustbin tena isiyofaaa!
   
 8. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  mdau punguza hasira zenye wivu na husuda.Pasipo shaka nguvu ya chadema ni moto wa tipper na si upepo unaopita.Kukuonyesha kuwa nguvu yake ni kubwa, pamoja na ahadi nyingi arumeru mashariki , ccm iliangukia pua.angalia m4c inavyochangiwa mafdha na wanyonge, ndo hapo utathibitisha namna gani inakubalika.Hili halipingiki, tuchambue ukweli,ccm kipi cha maana imewatendea wakulima hasa wa mikoa ya kanda ya ziwa kwnye zao la pamba kuhusu bei ya zao hilo?ni blabla tu na kuwakatisha tamaa.Mpka wakulima wa korosho , walifikia kuandamana, wakati serikali ipo.je haya huoni yanawakera jamii?pia ufisadi mkubwa unapoibuliwa, na cdm kupigia kelele, ccm inapuuza na kusema propoganda, haya ndo yanayoipa nguvu cdm.Mdau acha wivu na porojo za kwenye mitandao
   
 9. H

  HIMO Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ccm kwishney hata gadaffi alikuwa anaambiwa nchi inaondoka anabisha
   
 10. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,156
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  well said mkuu
   
 11. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ccm hawaamini ila kumesha kucha kama wanaakili watakuwa kama KANU ilivyopoteza umaarufu mpaka kuwa chama cha kubebwa
   
 12. K

  Keil JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwakajumilo siyo Dr.

  Labda kama amechakachua zile za ki-CCM CCM ... kama za akina Nchimbi, Kamala na wengineo.
   
 13. K

  Kiboko ya washamba Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnaongea sana CDM.Debe tupu alikosi kelele:baby:
   
 14. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Cdm wajiandae kuchukua nchi 2015...
   
 15. congobe

  congobe JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 499
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  wewe una mapenzi na ccm ,yote yanayotendeka mabaya unaona ni mema tu ,acha unafki huwezi mshawishi mtu kwa ujinga kama huu ,tembea mbele huko
   
Loading...