CCM yajua itaanguka chaguzi hii, je itaitumia NEC tena kama 1995 kuahirisha chaguzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yajua itaanguka chaguzi hii, je itaitumia NEC tena kama 1995 kuahirisha chaguzi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 15, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Takwimu mbalimbali machoni pa uongozi wa juu wa CCM zimedhihirisha uchaguzi huu watadondoka vibaya katika Uraisi na Ubunge lakini watapeta katika udiwani.

  Mwaka 1995, CCM walipoona viti vyote saba vya ubunge jijini Dar vinabebwa na NCCR-MAGEUZI serikali ya CCM iliitumia NEC kuchelewesha vitendea kazi vya uchaguzi na hivyo kuahirisha uchaguzi ili kuipa CCM nafasi ya kujipanga upya na huku wakielewa hasira za wapigakura dhidi yake zitakuwa zimepoa. Vilevile wengi wa wapigakura hawatarudi kupiga kura na matokeo yake mahudhurio kwenye chaguzi zilizoahirishwa yalikuwa ni kiduchu sana na CCM ilipeta kwenye majimbo sita ukiliondoa la Ubungo ambalo Dr. masumbuko Lamwai alilishinda. Hata yeye baadaye Mahakama Kuu ilitengua ushindi wake na CCM wakalibeba kiulaini!!!

  Kutokana na historia hiyo ya kifisadi ambayo serikali ya CCM iliwahi kuitumia mwaka 1995 kwa ubunge wa majimbo ya Dar-Es-salaam upo wasiwasi mkubwa kuwa huenda mbinu hizo zikajirudia mwaka huu ili kupooza hasira za wapigakura na wakati huohuo CCM kujipanga upya kujibu mashambulizi...

  Tunahitaji NEC watuhakikishie ya zamani hayatajirudia tena safari hii......Maana ni vigumu kwa mtu yeyote mwenye akili timamu kuelewa ilikuwaje mwaka 1995 Dar iwe haina vitendea kazi vya uchaguzi lakini kwingineko nchi nzima wasipate tatizo hilo. Ikumbukwe Makao Makuu ya NEC yapo Dar-Es-Salaam!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna haja ya kujipanga
   
 3. A

  August JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  good observation, lakini utatuzi wa tatizi hilo ni nini? nafikiri ni taadhari, na kuwaambia wananchi na hao waangalizi wa kitaifa/kitamataifa
   
Loading...