Ccm yajitengenezea mazingira ya kupinga matokeo ya urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm yajitengenezea mazingira ya kupinga matokeo ya urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DOMA, May 18, 2012.

 1. D

  DOMA JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Wakuu
  kweli ccm imeshikwa pabaya na bila shaka inajua mwaka 2015 ndio mwisho wake na hili la kamati kuu ya ccm kukubali kwamba matokeo ya urais yawe na pingamizi yamedhihirisha hilo
  natoa hoja...
   
 2. o

  oakwilini Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haitasaidia,ngoja watapetape
   
 3. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  DOMA

  Kila mtu makini,mzalendo na mwanamapinduzi wa nchi hii anajua kabisa kuwa CCM wanaona MAJI YAMEZIDI UNGA ndiyo maana kwa sasa wameshaanza kuboresha sheria na taratibu ambazo huko nyuma zilikuwa zinakilinda CHAMA TWAWALA!
  CCM wamesoma alama za nyakati na wanajua kabisa Watanzania wamechoka na chama hiki cha wababaishaji ambacho kwa zaidi ya NUSU KARNE tangu nchi imepata uhuru mwaka 1961 HAKUNA MAENDELEO YOYOTE KWA WATANZANIA. Kila kunapokucha hali za Watanzania walio wengi zinazidi kuwa mbaya huku wakidanganywa kuwa HAYO NDIYO MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.

  Mimi nawashauri CCM wasiishie tu kwenye kuweka pingamizi kwenye matokeo ya Urais baali pia na hili la Rais kushtakiwa Mahakamani kama alikiuka katiba na sheria wakti akiwa madarakani wakubaliane nalo.Hiyo ndiyo DEMOKRASIA!
   
 4. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Rais apite hata kwa kura moja. Hii nayo wataibadilisha.
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Halmashauri kuu ya Chama chochote kile haina haki wala mandate ya kuwaamulia watanzania watoe maoni ya aina gani tunapoelekea katika mchakato wa katiba. CCM haiwezi kukimbia kivuli chake yenyewe ni nani asiyejua kuwa CCM ndiyo imekuwa kikwazo cha mgombea binafsi kwa kuingilia uhuru wa mahakama?.

  CCM kama chama wanaweza kukaa chini na kuandaa maoni yao ya jinsi wanavyoona katiba mpya iwe kama vile ambavyo vyama, makundi na watu binafsi wanavyoweza kufanya, ila ni nini kiingie wapi na vipi kinabakia kuwa kwa waandaaji warasimu ya katiba kwa kuzingatia uwingi wa maoni fulani.

  CCM ikija na tamko lake basi ni mwanzo wa kuuharibu mchakato wa katiba kwani CUF nao wanaweza kuja na tamko la kubariki kuvunjwa kwa muungano kuongelewe katika mchakato, CDM nao watakuja na lao, waislam, wakristo na lao.

  Huu si mfano mzuri unaopaswa kuigwa toka kwa CCM. Inayoandaliwa si katiba ya CCM bali ni katiba ya Tanzania. CCM wangeweza sema kuwa wao maoni yao wanaonelea mgombea binafsi awepo ningekubaliana nao kama maoni ya chama na si kuwapangia watanzania kuwa wanaweza kujadili.

  Suala la katiba mpya halipaswi kuwa politicised, we will all fail tusipoangalia.
   
 6. Asango

  Asango JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jiliwaze tu ndgu yng!
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Huree nimetoka kwenye ban sasa hivi kwi! Kwi! Kwi! Magamba mtanikoma
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Wamechanganyikiwa hawa, wamekuwa wakisema kuwa Katiba mpya ni wazo Lao, sheria wametunga wao, tena kwa kutoa matusi mengi kwa wapinzani, vitu vya kujadili na kutojadili wameweka wao, tume wameteua wao, tena kwa mbwembwe kibao, wajumbe wengi ni wao, kabla tume haijaanza kazi wao tayari wameshaanza kutoa maoni. Kama Ndio maoni Yao na serikali ni Yao kulikuwa na sababu gani ya kuunda sheria si wangeagiza tu serikali Yao ifanye wanavyotaka, kuliko Kupoteza hela bure.

  Wahenga walisema mfa maji haachi kutapatapa.

  WAzee wa upinzanI na politiki, Dalili za kufa CCM hizo!!!!!!!!!!
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi kinachonishangaza kuhusu matendo ya CCM ni kule kuanza kutoa matamko toka katika vikao vyao. Ina maana wanaona kuwa huenda mnyama waliemchagua (Tume) Akaenda rogue na kusimamia masilahi ya nchi badala ya masilahi ya CCM. Tena wasivyo na haya wanatoa matamko ya kuruhusu vitu fulani vijadiliwe vitu fulani visijadiliwe kana kwamba wao ndiyo wananchi pekee wa Tanzania wenye haki na mchakato.

  Hata kule kutembelea tembelea tume mara Pinda, mara JK, mara makamu wake inaonesha ni jinsi gani jinamizi hili linavyowawewesesa. Mimi binafsi ningependa tume iachwe ifanye kazi yake kwa uhuru na uwazi bila ya kuonekana kuwa serikali inawaingilia. Kazi ya serikali kama JK alivyosema ni kuwapatia resources na ulinzi basi. Tume imekaa inaandaa hadidu zake wao wanaanza kutoa matamko ya ku-influence mchakato. Hizi ni dalili za kushindwa kabla hujaanza.

  CCM wangeweza kabisa na wana uhalali kabisa wa kutoa mapendekezo yao kama chama, ila si kujifanya wanatoa ruhusa kwa wengine, kila mtu na kundi lina mawazo yake. Kuongoza mchakato wa katiba si ki hivi, kazi yao imeisha pale walipotumia bunge lao, rais wa chama chao kutunga sheria na kuteua wajumbe sasa wakae pembeni waone vile ngoma inachezwa si kuanza kujipatia nafasi ya kupasha ngoma moto ili itoe mlio wautakao wao.
   
 10. k

  kbhoke Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  CCM inaonekana kiukweli kutaka kujitengenezea mazingira ya kukimbilia mahakamani endapo mgombea wake wa urais atashindwa. Kadhalika nafikiri pia, wapo wana CCM ambao sasa wanatamani kuchaguliwa bila kupitia mgongo wa CCM maana CCM inaendelea kukosa umaarufu miongoni mwa watanzania. Hivyo wanataka kupigia kelele hoja ya kuruhusiwa mgombea binafsi, hoja ambayo iliibuliwa na Mtikila na kupingwa vikali na serikali ya CCM! Kazi kweli kweli..
   
Loading...