CCM yajipongeza, yajipanga

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
CCM imejipongeza kwa kuwa huru toka katika mashambilo ya wapinzani. Katika vikao mbalimbali vya kichama hapa Lumumba, CCM imesifu ubunifu wa kumwaga petrol kwenye kambi ya wapinzani na kuwafanya wapinzani waparurane.

"CCM sasa iko huru.Wapinzani wanarushiana makombora wenyewe.Huu ni muda wetu wa kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba. Tuendelee kuchochea kuni huko kwenye media" alisema Mkuu wa Kitengo cha Propaganda Ofisi Ndogo za Lumumba wakati akizungumza na timu maalum ya 'Watu wapiganaji wa mitandaoni'.

" Tusiwape nafasi wapinzani kujipanga. Tuendelee kuwaweka 'busy' hawa watu. Tuendelee kumtumia huyu jamaa ili wakati wa wanamjibu yeye,sisi tunajipanga tukiwa na nafasi na muda wa kutosha. Uteuzi wa wagombea utatukuta tukiwa na amani na utulivu" aliongeza Kada huyo Mwanadamizi wa CCM, Mtaalamu wa mipango yenye malengo.

CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
hii option ya mwisho ya CCM kwa wapinzani (divide them.....) tuipe muda tuone kama itafanya kazi - yes, ni kipimajoto tosha kwa wapinzani kabla hawajakabidhiwa nchi mwezi October.
 
Ni kujifariji, ni kujijadanganya. Enzi za ccm hazipo tena. Hakuna mbinu yoyote watakayoitumia watafanikiwa kwa sababu kuna hasira kubwa mbinguni na Mungu amesikia kilio cha watanzania cha kuwa maskini katika nchi yao tajiri na Mungu ameshuka kuwakomboa kwa maana amesikia kilio chao. Kwa hiyo hakuna hila ya ccm itakayofanikiwa. Huu ni wakati wa mabadiliko.
 
Mzee umesema ya ukweli na pongezi hizo ni matokeo ya kikao kilichofanyika Kunduchi Beach Hotel.Kikao hicho kilikuwa na lengo la kutathimini mpango huo na kuona ni jinsi gani utafanikiwa zaidi.
 
Nawataka wanachama wa CHADEMA wazunguke nchi nzima kumtangaza adui wetu namba moja ambaye ni Zitto. JJ Mnyika
 
CCM imejipongeza kwa kuwa huru toka katika mashambilo ya wapinzani. Katika vikao mbalimbali vya kichama hapa Lumumba, CCM imesifu ubunifu wa kumwaga petrol kwenye kambi ya wapinzani na kuwafanya wapinzani waparurane.

"CCM sasa iko huru.Wapinzani wanarushiana makombora wenyewe.Huu ni muda wetu wa kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba. Tuendelee kuchochea kuni huko kwenye media" alisema Mkuu wa Kitengo cha Propaganda Ofisi Ndogo za Lumumba wakati akizungumza na timu maalum ya 'Watu wapiganaji wa mitandaoni'.

" Tusiwape nafasi wapinzani kujipanga. Tuendelee kuwaweka 'busy' hawa watu. Tuendelee kumtumia huyu jamaa ili wakati wa wanamjibu yeye,sisi tunajipanga tukiwa na nafasi na muda wa kutosha. Uteuzi wa wagombea utatukuta tukiwa na amani na utulivu" aliongeza Kada huyo Mwanadamizi wa CCM, Mtaalamu wa mipango yenye malengo.

CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Kama ni kuandika tulishaandika sana sana kuhusu mgogoro wa chadema na zzk, na hata namna ya kuumaliza lakini hatukusikilizwa eti kuna watu ambao wanafahamu zaidi kuhusu chadema kuliko wengine, wakasahau msemo wa kiswahili usemao "ukijamba kwa hasira utajinyea" wacha waparurane kwenye majukwaa majuto ni mjukuu.
 
Kweli kabisa na vita ya panzi furaha ya kunguru. Majuto ni mjukuu
 
Project ACT ya CCM seems to be working. Keep it up ZZK, you will be rewarded big time...

Ni mapema mno kusema kuwa is working kwa vile watanzania tunawacheki tu na kumsikiliza huyo mtoto mliyemtuma sokoni bila hela, tunajua kuwa hatanunua kitu chochote hata mkubwa mwenye hela afike. Kwa nini tutishike na chui wa makaratasi?
 
image.jpg
Kwa nyomi hii ya Zitto Kabwe ni dhahiri kuwa akina Petro Mselewa na wenzake pale Kinondoni wamechanganyikiwa sana
 
CCM imejipongeza kwa kuwa huru toka katika mashambilo ya wapinzani. Katika vikao mbalimbali vya kichama hapa Lumumba, CCM imesifu ubunifu wa kumwaga petrol kwenye kambi ya wapinzani na kuwafanya wapinzani waparurane.

"CCM sasa iko huru.Wapinzani wanarushiana makombora wenyewe.Huu ni muda wetu wa kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba. Tuendelee kuchochea kuni huko kwenye media" alisema Mkuu wa Kitengo cha Propaganda Ofisi Ndogo za Lumumba wakati akizungumza na timu maalum ya 'Watu wapiganaji wa mitandaoni'.

" Tusiwape nafasi wapinzani kujipanga. Tuendelee kuwaweka 'busy' hawa watu. Tuendelee kumtumia huyu jamaa ili wakati wa wanamjibu yeye,sisi tunajipanga tukiwa na nafasi na muda wa kutosha. Uteuzi wa wagombea utatukuta tukiwa na amani na utulivu" aliongeza Kada huyo Mwanadamizi wa CCM, Mtaalamu wa mipango yenye malengo.

CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Wanakiona kibanzi ndani ya chadema ilihali boriti iliyo ndani ya macho yao hawajaitoa. Wenzao chadema waliitoa ikalazimisha kubaki baadae ikatoka yenyewe hivyo chadema ndio wako huru zaidi kuliko ccm ambao boriti yao bado ingali wanayo (makundi ndani ya chama) na yamewashinda kuyatoa. Hivyo hapa tunasubili muda tu ndio utaongea ukishafika
 
Back
Top Bottom