CCM yajipanga zaidi kuwasaidia wananchi

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Viwanda 10 vya nyama kujengwa
Ni ndani ya miaka mitatu
NA MWANDISHI MAALUM, ARUSHA
WAZIRI Mkuu Edward Lowassa, amesema Tanzania inatarajia kuwa na viwanda 10 vya kusindika nyama nchini katika miaka mitatu ijayo, ili kuinua kipato cha wafugaji.
Akifungua mkutano wa viongozi wa kimila wa kabila la Wamasai mjini Arusha jana, Lowassa alisema viwanda hivyo pia vitaendeleza ufugaji nchini.
“Wafugaji wengi nchini hivi sasa wanachunga tu mifugo na hawafugi kisasa, hivyo wanashindwa kupata maendeleo kutokana na mifugo yao kama ilivyo kwa mazao ya wakulima.
“Kama wakulima wanavuna kahawa kwa nini wafugaji wasivune mifugo …kama wakulima wanavuna pamba, kwa nini wafugaje wasivune mifugo?” alihoji Waziri Mkuu.
Tangu kufungwa kwa kiwanda cha Tanganyika Packers cha Dar es Salaam miaka kadhaa iliyopita, Tanzani haina kiwanda kikubwa cha kusindika nyama.
Kuna viwanda kadhaa vinakamilishwa hivi sasa katika mikoa ya Shinyanga, Rukwa na Arusha.
Kutokana na kutokuwa na viwanda vya kutosha vya usindikaji nyama, baadhi ya wafugaji na wafanyabiashara wengine wanasafirisha nje wanyama wazima, hususan katika nchi za Komoro na Arabuni.
Tanzania ni ya tatu katika Afrika, baada ya Sudan na Ethiopia kwa kuwa na ng’ombe, mbuzi na kondoo.
Waziri Mkuu alisema kutokana na mifugo kushindwa kuhimili mahitaji ya kiuchumi ya wafugaji, ndiyo maana vijana wa wafugaji wa kabila la Kimasai wanakimbilia mijini kufanya kazi za ulinzi wa usiku.
“Wamasai sasa wametapakaa Dar es Salaam na Zanzibar; Nairobi, Kenya; Kampala, Uganda na katika miji mingine kufanya kazi za ulinzi wa usiku …tuwasaidie hawa waachane na kazi hii isiyo na tija,” alisema.
Lowassa alisema njia nzuri ya kuondokana na hali hiyo ni kuendeleza elimu, ili wafugaji hao wawe bora zaidi na waingie katika mfumo wa uchumi wa kawaida.
Alisema wale waliopewa ‘rungu’ kuongoza, wawaongoze watu wao kwa kuhakikisha wanapata elimu. Katika mila za Kimasai, kiongozi hukabidhiwa rungu.
Waziri Mkuu aliwataka wafugaji kote nchini wawe wafugaji wa kweli kwa kunenepesha mifugo yao na kuiuza ndani na nje, na siyo kuwa wachungaji kwa kuzunguka nchi nzima kutafuta malisho.
“Hamuwezi kuzunguka na kusambaa nchi nzima kutafuta malisho. Hamtakiwi kuigeuza Tanzania yote kuwa ni eneo la malisho,” alisema.
Mkutano huo wa viongozi wa kimila ulikuwa sehemu ya shughuli za Waziri Mkuu katika ziara yake ya siku mbili ya mkoa wa Arusha.
Juzi alitembelea wilaya ya Monduli ambako alikagua shule, bwawa la maji na kuzungumza na vijana waliokuwa katika kambikazi ya kimataifa kabla ya kufuturu na waumini wa Kiislamu walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, katika futari aliyowandalia katika mji mdogo wa Mto wa Mbu.
source: uhuru
 
Hadithi za abunuwasi zimeanza, siwezi kuwaamini Mafisadi kwa sababu ya ubabaishaji wao. Hiyo ndio ndege yao inayopaa.
 
Je?hivyo viwanda ni kwa ajili ya kugawa nyama ya kale kasungura ka Lowassa nini?

Ama huko watachinja wanyama gani? naomba jibu tafadhali kwani waziri mkuu aliwahi kusema kuwa nchi hii kuna kasungura kakugawana.
 
kweli sera zao zimekwisha, fisadi ataletaje maendeleo? au anatafutia soko ngombe zake alizonunua kutumia vijisenti vyetu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom