CCM yajipanga kurejesha kata/mitaa zilizochukuliwa na UKAWA Dar

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,494
1 (1).jpg
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejipanga kuhakikisha kinarejesha Kata mbalimbali kilizopoteza na kuchukuliwa na vyama vya upinzani katika jiji la Dar es Salaam na kusema kuwa kwa sasa wanajipanga kuhakikisha Kata pamoja na mitaa waliyopoteza inarudi.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ubungo, Mbaruku Masudi wakati akiongea na waandisha wa habari amedai kuwa kwa sasa wameanza kuondoa changamoto mbalimbali ndani ya chama hicho kuhakikisha wanashinda na kukomboa mitaa na Kata ambazo zipo chini ya wapinzani.

"Tutahakikisha katika changuzi zozote zilizopo mbele yetu kama ule wa Saranga uchaguzi mdogo ni kuhakikisha tunarudisha mitaa iliyobaki na Kata zilizobakia" alisisitiza Mbaruku

Katika uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika Novemba 26, 2017 uliwapa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Saranga Ubungo na kuweza kukomboa Kata hiyo ambayo awali ilikuwa chini ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Muungwana
 
Back
Top Bottom