CCM yaibuka na ushindi mnono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yaibuka na ushindi mnono

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Feb 1, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,724
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  CCM yaibuka na ushindi mnono

  Monday, 31 January 2011 19:35 administrator  NA SOLOMON MWANSELE, MBEYA
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Mbeya mjini, kimeibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa serikali za Mitaa na wajumbe, kwa kunyakua mitaa sita kati ya saba iliyofanya uchaguzi, Januari 30, mwaka huu.
  Sambamba na hilo, CCM imefanikiwa pia kushinda nafasi 12 za ujumbe, kati ya 14 zilizokuwa zinawania katika mitaa mbalimbali mjini hapa.
  Katibu wa CCM wilayani hapa, Bahati Makalanzi, akizungumza jana, alisema matokeo hayo yanaonyesha kuwa wananchi wengi bado wana imani na Chama, hali iliyopelekea maeneo mengine wagombea wake kupita bila kupingwa.
  Alisema uchaguzi huo umefanyika kufuatia baadhi ya wenyeviti kujiuzulu kwa kuchaguliwa katika nafasi za udiwani na katika mitaa mingine, kufariki.
  Bahati aliitaja mitaa mitatu kati ya saba ambayo wagombea wa nafasi ya Uenyekiti kwa tiketi ya CCM wamepita bila kupingwa na kata yake ikiwa kwenye mabano ni Paul Sangu wa mtaa wa Kanda ya chini (Iduda).
  Mingine ni mtaa wa Jacaranda (Sisimba) ambapo mgombea Alinanga Kamwela alipita bila kupingwa na mtaa wa Kagera (Ilomba), Anyosisye Mwambona amepita bila kupingwa.
  Katibu huyo wa CCM wilaya ya Mbeya mjini, alisema Chama kimefanikiwa kuibuka kidedea kwa wagombea wake waliosimamishwa katika mitaa ya Ghana magharibi (Ghana), ambapo Sudi Kipande, alimshinda mgombea wa CHADEMA kwa kujizolea kura 137 dhidi ya 18 za mpinzani wake.
  Katika mtaa wa Kiwanja Ngoma (Maendeleo), mgombea uenyekiti aliyesimamishwa na CCM, Richard Mwakoba, aliibuka mshindi kwa kujizolea kura 120 dhidi ya 21 alizozipata mgombea wa CUF.
  Pia CCM imeibuka mshindi katika mtaa wa Nsalaga (Nsalaga), ambapo mgombea wake Peter Ngonde, alimshinda mgombea aliyekuwa amesimamishwa na CHADEMA, kwa kupata kura 252. Mtaa wa Ndeje (Iwambi), umechukuliwa na CHADEMA.
  Kwa upande wa nafasi za ujumbe zilizokuwa zinagombewa kwa wilaya ya Mbeya mjini ni 14, ambapo CCM kimefanikiwa kushinda nafasi 12, huku moja ikichukuliwa na CHADEMA.
  Katibu Bahati, alisema uchaguzi wa kumtafuta mjumbe wa mtaa wa Nkuyu, uliopo kata ya Isanga, utarudiwa baada ya wagombea ujumbe kupitia CCM na CHADEMA kulingana kwa kura.
  Aliongeza kuwa, katika uchaguzi huo mdogo, CCM imefanikiwa pia kuirudisha mitaa ya Nsalaga na Kagera ambayo awali ilikuwa inashikiliwa na wenyeviti kutoka CHADEMA, ambao safari hii wameshindwa vibaya.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,724
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Uhuru wakati likifurahia matokeo haya lakini halituelezi ni kwa sababu zipi chaguzi hizi hazikufanyika wakati mwafaka....................inakuwa kama ni kuviziana vile.....................................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,724
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Katibu wa CCM wilayani hapaBahati Makalanziakizungumza janaalisema matokeo hayo yanaonyesha kuwa wananchi wengi bado wana imani na Chamahali iliyopelekea maeneo mengine wagombea wake kupita bila kupingwa.
   
  Alisema uchaguzi huo umefanyika kufuatia baadhi ya wenyeviti kujiuzulu kwa kuchaguliwa katika nafasi za udiwani na katika mitaa minginekufariki
  Wana imani na CCM au na ufisadi?
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  :A S thumbs_down: HUYU NAYE!
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  :clap2::clap2::clap2::clap2:
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,724
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  HTML:
  :clap2::clap2::clap2::clap2:
  
  Approving evil or what?
   
 7. msikonge

  msikonge Senior Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pumba x 100!!! U are :embarrassed::embarrassed::embarrassed::embarrassed::embarrassed::embarrassed: ment!!!
  You must present'behind the scene episodes"!!!
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kilo ya sukari Shs. 2000. Lita ya mafuta ya alizeti Shs. 3,500 (Octoba 2010 ilikuwa 2000), huo ndio ushindi mnono!!!!
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  CCM bwana na strategy za kitoto. Subiri uchaguzi mkuu ufanyike na watu kubana mianya yote ya chakachua ndipo utajua kuwa ushindi mnono ni nini?. Hutu tuuchaguzi twa makatibu kata wa CCM ndito twa kuandikia habari za ushindi? au ndiyo consolation?. Wajiandae 2015 ama kuingia katika uchaguzi kukiwa na katiba mpya ama kuipeleka nchi katika matatizo yatakayotugharimu na kujutia sana the past. Wakati wa kuchakachua unaisha na kama CCM na watendaji wake hawasomi alama za nyakati na kuendelea na mbinu zilezile za Mwalimu Nyerere na uchaguzi wa zanzibar 1995 we are doomed for the worse.
   
 10. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  CCM mgonjwa, CHADEMA daktari.
   
Loading...