CCM yaiagiza Serikali kununua mahindi tani 100,000

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
By Mtanzania Digital | September 8, 2021



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiagiza Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua tani 100,000 za mahindi katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini baada ya awali kukunua tani 24,000 sababu ni kutokana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) kudai kutakuwa na upungufu wa mvua msimu ujao wa kilimo.

Pia, kimeziagiza Wizara za Kilimo na Fedha na Mipango wakutane kujadiliana jinsi ya kupunguza bei ya mbolea kutokana na kuwa juu hivyo kumuumiza mkulima.

Akizungumza na Waandishi wa Habari juzi Septemba 6, jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa (CCM), Daniel Chongolo amesema mwezi wa saba Sekretariet ya CCM ilifanya ziara katika mikoa ya Rukwa, Songwe na Mbeya ambapo walikutana na changamoto ya wakulima kukosa soko la zao la mahindi.

Amesema mara baada ya ziara hiyo waliiagiza serikali kununua mahindi hayo ambapo ilitoa zaidi ya Sh bilioni 14, ambazo zilinunua zaidi ya tani 24,000.

Amedai kwa sasa fedha hizo zimeisha na wakulima wanaendelea kuhangaika kutafuta soko la kuuzia mahindi yao.

Kutokana na hali hiyo Chongolo ameiagiza serikali kutoa tena fedha na inunue tani 100,000 za wakulima hao kwani wanazo taarifa kwamba msimu ujao wa kilimo mvua zitakuwa chache.

“Tena kwa bei ile ile ya Sh 500 kwa kilogramu na wafanye zoezi hilo liwe endelevu kwani mamkala ya hali ya hewa imesema kuna changamoto katika mvua za vuli mpaka katika mvua za masika hivyo kutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula,” amesema.

Pia amesema katika ziara hiyo wamejifunza kwamba uchache wa vituo vya kununulia mahindi hivyo ameiagiza NFRA kuweka vituo ambavyo vitakuwa karibu na wakukulima.

“Kuna malalamiko kukatwa fedha katika Sh 500 tunasema hapana mtu aliyepo Mufindi, Ileje, Mbozi, Nkasi tunataka bei ya mahindi iwe moja kwa wote wa karibu na mbali,” amesema Chongolo.

Katika hatua nyingine, ameziagiza Wizara za Kilimo na Fedha na Mipango wakutane kujadiliana jinsi ya kupunguza bei ya mbolea kutokana na kuwa juu hivyo kumuumiza mkulima.

Amesema kwa sasa bei ya mbolea aina ya Urea imepanda maradufu kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona ambapo awali ilikuwa shilingi 50,000 mpaka 55,000 lakini kwa sasa ni Sh 80,000 mpaka 85,000.

“Tunaiagiza Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango waanze mchakato wa jinsi ya kuwasaidia wakulima.Nasisitiza Wizara zikutane mapema kuwezesha kupungua kwa bei ya mbolea,” amesema.

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo amesema mara baada ya maagizo hayo baada ya wiki mbili wataanza ziara ya kukagua maelekezo hayo.
 
Bila shaka ni maccm. Yuko wapi Mwenyekiti wa maccm mpaka Serikali yake ipewe maagizo hadharani? Yuko busy anafanya Tour guide na kutangaza kwamba 2025 ataupiga mwingi tena nchi nzima!!!😂😂

CCM na serikali nani boss
 
..this is stupid.

..watenganishe uenyekiti na uraisi ndipo chama kitaweza kuiagiza serikali.
 
Nini kimazuia kuwa na kiwanda cha mbolea, matrekta, majembe nk nchi hii? Mbona chuma kipo kibao?
 
Uko sawa kabisa Mkuu.



Serikali inanunua mahindi kutoka wapi?

Na kwa bei gani?

Wananchi hawatakiwi kuiuzia serikali chochote maana private buyers buy kwa bei kubwa zaidi yao

Na pia hata kama wangekua wananunua bei sawa,binafsi siuzii serikali mahindi yangu

Serikali ni takataka,inadhani inaweza kuamua jasho langu nilifanyie nini kwa lazima yao

Alievumbua serikali kasababishia wanadamu matatizo mabaya sana mpaka leo hii
 
Katika mazingira haya ya kofia mbili, je kuna tofauti ya msingi kati ya CCM na serikali?
 
Back
Top Bottom