Elections 2010 CCM yahaha Karatu

Dada Makini

Member
Aug 27, 2010
28
52
Baada ya aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA Jimbo la Karatu Dr. W. Slaa kuchukua fomu za kugombea urais wanachama wa CCM Wilaya ya Karatu walifurahi sana wakijua jimbo hili litarudi mikononi mwao hasa baada ya kupita kimya kirefu kabla ya CHADEMA hawajamtangaza atakaye chukua nafasi ya Dr. Slaa.

Baada ya CHADEMA kumtangaza mgombea wake ambaye ni Ndugu Israel Yohana Natse CCM wameanza kuhaha kwani wananchi wengi wa Karatu wamempokea na kumkubali kiasi ambacho hawakutarajia hasa kutokana na mapokezi makubwa sana aliyoyapata wakati alipochukua na kurudisha fomu za kugombea Ubunge kwa Jimbo hili.

KARATU CCM HAINA NAFASI
 
Itakuwa ni aibu kwa chadema kupoteza jimbo la karatu kama walivyopoteza jimbo la hai pale mbowe alipogombea urais kwani hii inaonesha hata nyumbani kwako hukubaliki. Kwa sababu slaa hatapata urais bora tu jimbo la karatu libaki chadema ili kujenga demokrasia. All the best wanakaratu kuonesha uzalendo kwa kurudisha uwakilishi wa chadema bungeni kutoka kwenu.
 
Hizo speculation (nyekundu) siyo nzuri ni matumaini yangu kuwa hujakata tamaa kiasi hicho
 
Hata mimi nilikuwa nina wasi wasi huo kwa kuwa niliwahi kupita Karatu kipindi cha kampeni uchaguzi uliopita nikaona Dr. Slaa anavyokubalika pale na muda wote watu walikuwa wakifanya midahalo ya siasa kila sehemu, sasa nikawa najiuliza itakuwaje baada ya yeye kugombea urais? Safi sana wananchi wa jimbo la Karatu msikubali kuachia jimbo.
 
Dr. Slaa alikuwa ccm kabla ya kufanyiwa mizengwe na ccm na hivyo kuhamia chadema. Sina hakika kamahuyu naye kafanyiwa mizengwe ccm.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom