Uchaguzi 2020 CCM yagawanyika, hawana majibu hoja za Lissu!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,045
20,408
MOJA: Reli nyingine zilizopo na zenyewe ni standard gauge - TAZARA, RELI YA KATI, (DAR -KIGOMA) na ya TANGA-ARUSHA

MBILI:
Marais wengine wote na wenyewe walianzisha mabwawa ya umeme, kuanzia Kidatu na Mtera (Nyerere), wengine wakajenga Kihansi (Morogoro - MKAPA), Hale (Tanga - NYERERE), Pangani (Tanga - MWINYI), Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro - NYERERE), Rusumo (Kagera- KIKWETE), Songwe (Mbeya - KIKWETE)

TATU:
Wakati wa uhuru kulikuwa na mbuga moja tu, ya Serengeti, iliyotengwa na Mkoloni. Nyingine zote zilianzishwa kwa amri za marais kwa kuhamisha watu, hizi za Magufuli wanahamisha wanyama, wanawapeleka Chato ambako naturally hakuna mbuga, hakuna wanyama. Na wanapounda mbuga mpya wanaingilia maeneo ya watu na hawawalipi fidia, wanasababisha maafa na migogoro ya ardhi. Anaijua migogoro yote ya mipaka ya hifadhi nchi hii, na ardhi za wananchi zilizopokwa bila fidia, kwa sababu alilifanyia utafiti katika kazi yake ya kwanza akitoka chuo.

NNE:
Daktari muanzilishi wa Hospitali ya Masana Mbezi, Dar es Salaam, alikufa kwa pressure baada ya kukutwa na mashine alizonunua kwenye mnada wa vifaa chakavu, Muhimbili, akasahau kufuta zile alama za MUHIMBILI MKWAJU SERIKALI MKWAJU HOSP MKWAJU RUFAA MKWAJU SIFURI SIFURI MBILI MKWAJU.... Alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi isiyo na dhamana, akafa na pressure halafu wakakuta ni kweli alinunua Muhimbili.

TANO:
Mbunge wa CCM, Salim Hassan Abdullah Turki, amekufa na pressure baada ya kubambikwa madai ya kodi ya mabilioni. Mheshimiwa Turki ndie aliyekodi ndege ya kumpeleka Tundu Lissu Nairobi akiwa mahututi. Hii Tundu Lissu amesema ameambiwa na familia ya marehemu.

SITA:
Mtoto wa Dada yake Magufuli, Doto James, ambae kwa sasa ndie ana saini miamala yote ya serikali, alirushwa vyeo ghafla kutoka kuwa afisa TANROADS mpaka katibu mkuu HAZINA pindi mjomba wake alipopata Urais; Na kwamba, sasa hivi kuna watu wawili tu nchi hii, Doto James na mjomba wake, ambao wanajua hela za kununua ndege na za Bwawa la Rufiji ni shiing ngapi na zimetoka wapi.

SABA:
Familia ya Mwinyi, Mkapa kila mmoja anamiliki ekari 60,000, Sumaye 45,000 za ardhi ambazo awali zilikuwa mashamba ya serikali, ikiwemo NAFCO, kabla ya kujimilikisha wakiwa marais na wa mawaziri wakuu. Viongozi wengine na matajiri wenye ekari chini ya hapo, elfu 35, elfu 20, elfu 15, elfu 10, elfu 5 ni wengi, wengi, wengi mno. Ambao walipeana kama "wawekezaji" lakini wamezikalia tu. Na ni sababu moja kubwa na migogoro ya wakulima na wafugaji, kupungua kwa ardhi.

NANE: Miaka saba baada ya kuwa tushapata uhuru, Nyerere aliandika kitabu kuelekezea kwamba bado tunahitaji uhuru licha ya kuwa tulishawaondoa wakoloni, kinaitwa Uhuru na Maendeleo. Hoja kuu ya kitabu cha Nyerere inasema jamii inapimwa kwa maendeleo ya watu, sio ya vitu na miundombinu.

TISA:
Mkandarasi wa Uwanja wa Ndege Chato, Mayanga Construction (Steven Makigo), ni mme mwenza wa Magufuli, wameoa nyumba moja. Mme mwenza aliambiwa jenga uwanja! Mpwa (Doto James) akaambiwa toa hela!

KUMI:
Kiwanja kimoja tu cha ndege kimejengwa na Mkoloni, Mwingereza, kile cha Air Wing, Ukonga. Nyerere alijenga Kilimanjaro na wakaendelea kujenga vingine vyote nchini, Magufuli si Mtanzania wa kwanza kujenga uwanja wa ndege.

NB: Mwenyekiti UVCCM TAIFA SHAKA JAMES aliyeagiza kuumizwa kwa wapinzani na mwenye kauli za kibaguzi ni mtoto wa Dada yake "MEKO"

-----------------------------------------------------------

WHAT'S THE POINT?
Anasema, wakati wote huu inajengwa hiyo miradi toka uhuru, airports, mbuga, reli, mabwawa ya umeme, mabarabara, hakuna Mtanzania aliyenyanyapaliwa, aliyeuawa kwa pressure ya kutishwa, kuhamishwa, kubambikwa kodi, kupigwa, kutiwa kizuizini miaka 5, au kumiminiwa risasi kwa kuhoji miradi au kwa kigezo kwamba nawaletea maendeleo.


Lissu 2020

Hoja kwa hoja, Tundu Lissu
 
Kampeni sio malumbano kati ya wagombea ni kila mgombea kunadi Sera zake kwa wananchi

CCM tuko bize kunadi Sera zetu kwa wananchi sio kujibizana na mbelgiji
CCM tuko bize na wasanii 200 kukata mauno, then dakika 5 za kutaja madaraja, ndege na stigla, alafu kwaheri
 
Back
Top Bottom