CCM yafunga kampeni za uchaguzi jimbo la Kalenga kwa kishindo

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
2.+Mashabiki+wakimbeba+Mgimwa.jpg

Wananchi wakiwa wamembeba kwa furaha mgombea wa Ubunge jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kwa tiketi ya CCM, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, kwenye Uwanja wa Mnada, Kijiji cha Kidamali, Kata ya Nzihi, leo
3.+Kinana%252C+Mgombea+na+Mwigulu+wakisalimia+wananchi+Kijiji+cha+Kidamali.jpg

4.+Kinana%252C+Mgimwa+na+Mwigulu+wakisalimia+wananchi.jpg

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Naibu Katibu Mkuu (Bara) Mwigulu Nchemba na Mgombea wa CCM jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa wakisalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano huo.
6.+Kinana+akimnadi+Mgimwa.jpg

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akimnadi Mgimwa kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni
5.+Mwigulu+akihutubia.jpg

Naibu Katibu Mkuu(Bara), Mwigulu Nchemba akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni
8.+Mgimwa+akihutubia+maelfu+ya+watu+2.jpg

Mgimwa akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni
10.+Mgimwa+akionyesha+mkewe.jpg

Mgimwa akiionyesha hadhara mkewe Robi, kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni za CCM.
7.+umati+wa+watu+ukinyoosha+mikono+kuafiki+kumchagua+Mgimwa.jpg

Umati wa wananchi wakinyoosha mikono kuafiki kumchagua mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa kesho.
 
Sera na ilani ya uchaguzi ya CCM ndiyo itakayokivusha chama katika chaguzi mbali kama ilivyothibitika na inavyoendelea kuthibitika katika chaguzi mbali mbali nchini.

Chama makini kinajionesha kwa wanachama wake na katika wanachama wake ndiyo kinapata wagombea wake na katika wagombea wake ndiyo ushindi hupatikana katika chaguzi.

Huwezi kuwa na chama kinachoendesha kwa misingi ya ubaguzi wa makabila au dini ukategemea kupata ushindi katika jamii inayochukia ubaguzi hata wa kifikra achilia mbali ubaguzi wa kabila au dini.

HUwezi ukawa na chama kinaendeshwa kwa mapenzi na mtazamo wa mwanzilishi wa chama ukategemea kutakuwepo na uhuru wa wananchama na viongozi kupingana katika fikra na mitazamo.

Huwezi ukawa na chama kinawashughurikia baadhi ya viongozi kwa sababu hawatokei sehemu fulani ya nchi ukategemea kitaweza kukabidhiwa ridhaa ya kuongoza taifa.

CCM ni amani, CCM ni upendo, CCM ni Mshikamano na CCM ni furaha.

CCM ni Itikadi, CCM ni sera, CCM ni Ilani ya uchaguzi na CCM ni ushindi.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.
 
jamani kuna habari zinakuja hapa jf vipande vipande kwamba kuna mbunge kakamatwa akigawa rushwa! hii imekaaje! maana hizi siasa mh!
 
...

....Ndani ya mioyo yao kuna siri kubwa na kesho wataisema kwa vitendo....ukitazama kwa makini picha hata unyooshaji wa mikono unaonyesha !!!

Chadema ni Mpango wa Mungu wengine kwa Shetani tu...
 
Sera na ilani ya uchaguzi ya CCM ndiyo itakayokivusha chama katika chaguzi mbali kama ilivyothibitika na inavyoendelea kuthibitika katika chaguzi mbali mbali nchini.

Chama makini kinajionesha kwa wanachama wake na katika wanachama wake ndiyo kinapata wagombea wake na katika wagombea wake ndiyo ushindi hupatikana katika chaguzi.

Huwezi kuwa na chama kinachoendesha kwa misingi ya ubaguzi wa makabila au dini ukategemea kupata ushindi katika jamii inayochukia ubaguzi hata wa kifikra achilia mbali ubaguzi wa kabila au dini.

HUwezi ukawa na chama kinaendeshwa kwa mapenzi na mtazamo wa mwanzilishi wa chama ukategemea kutakuwepo na uhuru wa wananchama na viongozi kupingana katika fikra na mitazamo.

Huwezi ukawa na chama kinawashughurikia baadhi ya viongozi kwa sababu hawatokei sehemu fulani ya nchi ukategemea kitaweza kukabidhiwa ridhaa ya kuongoza taifa.

CCM ni amani, CCM ni upendo, CCM ni Mshikamano na CCM ni furaha.

CCM ni Itikadi, CCM ni sera, CCM ni Ilani ya uchaguzi na CCM ni ushindi.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.
Mimi nipo iringa nimeshuhudia mabasi ya upendo yanasomba watu kutoka sehemu mbalimbali"
 
hongera zake..... sasa sisi tusio na mababa mawaziri tutarithi nini....?
 
jamani kuna habari zinakuja hapa jf vipande vipande kwamba kuna mbunge kakamatwa akigawa rushwa! hii imekaaje! maana hizi siasa mh!
Ndiyo mbunge wa Chadema mzazi mwenzie Dr.Slaa Bi Rose Kamili alikuwa anatoa rushwa kwa wapiga kura.
 
Wahehe amkeni, nchi inatafunwa na wenye meno, na inajengwa na wenye moyo! Ccm imetunyonya vya kutosha sana! Chagueni chadema..
 
Sera na ilani ya uchaguzi ya CCM ndiyo itakayokivusha chama katika chaguzi mbali kama ilivyothibitika na inavyoendelea kuthibitika katika chaguzi mbali mbali nchini.

Chama makini kinajionesha kwa wanachama wake na katika wanachama wake ndiyo kinapata wagombea wake na katika wagombea wake ndiyo ushindi hupatikana katika chaguzi.

Huwezi kuwa na chama kinachoendesha kwa misingi ya ubaguzi wa makabila au dini ukategemea kupata ushindi katika jamii inayochukia ubaguzi hata wa kifikra achilia mbali ubaguzi wa kabila au dini.

HUwezi ukawa na chama kinaendeshwa kwa mapenzi na mtazamo wa mwanzilishi wa chama ukategemea kutakuwepo na uhuru wa wananchama na viongozi kupingana katika fikra na mitazamo.

Huwezi ukawa na chama kinawashughurikia baadhi ya viongozi kwa sababu hawatokei sehemu fulani ya nchi ukategemea kitaweza kukabidhiwa ridhaa ya kuongoza taifa.

CCM ni amani, CCM ni upendo, CCM ni Mshikamano na CCM ni furaha.

CCM ni Itikadi, CCM ni sera, CCM ni Ilani ya uchaguzi na CCM ni ushindi.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

umesahau mkuu pia ccm ni watoa rushwa ccm ni majangili ccm ni ya kurisishana ccm ni wauza unga ccm ni kulala tu bungeni
 
Ndiyo mbunge wa Chadema mzazi mwenzie Dr.Slaa Bi Rose Kamili alikuwa anatoa rushwa kwa wapiga kura.

Chadema kwa kubebana kwa hiyo babu akaona mtonyo aupitishie kwa mkewe ili salio wagawane
 
Tatizo hawa waungwana wanajua kuchonga kweli ila kesho tunawakamua mbaya. Kama mnakumbuka hadi ktk Uchaguzi wa Madiwani 27 - 3 walituvyokua wanasema nitakua nimetenda haki nikiwafananisha na yule Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iraq aliyekua anaenda kwa jina la Al Sahaf watakwambia mfano Bunda mgombea anasubiri kuapishwa tu. J3 watakuja hadithi ya Uboreshaji wa Daftari. Nawashauri wakati matokeo yanatangazwa mkae karibu na kopo la Panadol kwavile mtashangazwa na kile mnachokisikia.
 
jamani kuna habari zinakuja hapa jf vipande vipande kwamba kuna mbunge kakamatwa akigawa rushwa! hii imekaaje! maana hizi siasa mh!
Sina uhakika vizuri lakini hata huyu inadaiwa amekamatwa na polisi akigawa rushwa.
IMG_9865.jpg
 
nimeona clip moja ya kinana akijaribu kuwaimbisha wananchi kwamba kwanini kalenga hakuna maji, umeme, shule za karne za ujima no windows, no doors but mostly no teacher inside the class yaani utacheka swali ambalo nilkuwa najiuliza how can you can explain away problems citizens have been suffering for decades? millions of excuses with no solution on hand. nimeona picha za kampeni vijijini yaani hakuna tofauti za enzi za ujima yaani ni kama vile vijiji vya sudan ya kusini madhara ya utawala mbaya wa ccm hayachagui jamani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom