CCM yafukuzwa mijini

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
297
UCHAGUZI Mkuu wa 2010, umeelezwa kuifikisha pabaya CCM, kwa kuangushwa na wapinzani katika majimbo mengi yaliyo kwenye majiji makubwa na makao makuu ya halmashauri za wilaya nchini, hali inayotafsiriwa kuwa ni hatari kwa chama hicho tawala.

Aidha, katika baadhi ya majiji upo uwezekano mkubwa wa wapinzani kuongoza halmashauri za miji na majiji baada ya kupata madiwani wengi na hivyo kuwa ndio msingi mkubwa wa maamuzi ya serikali katika ngazi hizo.

Hali hiyo inaifanya CCM kuhitaji kufanya kazi ya ziada ili kulinda majimbo yake ya vijijini kutokana na kinachoelezwa kuwa nguvu ya wapinzani ina mwelekeo wa kwenda vijijini, baada ya kufanikiwa kuyatawala majimbo ya mijini.

Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kuwa hadi sasa CCM imejikita zaidi katika majimbo ya vijijini huku, wapinzani wakijikita zaidi katika majimbo yaliyopo katika majiji na makao makuu ya halmashauri.

Katika Uchaguzi Mkuu wa urais, wabunge na madiwani uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu na kiporo chake kumalizika Novemba 14, CCM imepoteza zaidi ya majimbo, huku upinzani ukiwa mkali katika majimbo ya mijini kuliko vijijini.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameweka bayana kuwa, kama CCM inataka kuendelea kuongoza nchi hii kupitia ridhaa ya wananchi, ni vyema ikajiandaa mapema kubadilika na kusikiliza matakwa ya wananchi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

“Venginevyo CCM inajiandaa kuanguka na kuadhirika vibaya mwaka 2015,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa ForDIA, Bubelwa Kaiza.

Katika uchaguzi huo CCM imepoteza majimbo ya Mbeya Mjini (Chadema), Lindi Mjini (CUF), Arusha Mjini (Chadema), Nyamagana na Ilemela ya Mwanza Mjini (Chadema), Moshi Mjini (Chadema), Musoma Mjini (Chadema), Iringa Mjini (Chadema), Zanzibar Mjini (CUF), Ubungo (Chadema) na Kawe Jijini Dar es Salaam (Chadema).

Hata hivyo, CCM imejikuta baadhi ya Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ikiwa ni pamoja na Karatu (Chadema), Kasulu Mjini (NCCR), Bukombe (Chadema), Mpanda Mjini (Chadema) na Meatu (Chadema).

Lakini Kaiza alisema CCM imepoteza imani ya wananchi wa kawaida ambao wanasumbuliwa na ugumu wa maisha na hivyo kuona ndoto zao haziwezi kukamilika chini ya uongozi wa CCM.

“Na kwa matokeo haya sasa CCM imejikuta ikiwa katika pingu za wapinzani kwa sababu haiwezi kufanya tena inavyotaka, ni lazima isikilize watu wengine wanasemaje,” alisema Kaiza.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema CCM imeanza kukosa jamii msingi ambayo ilijijengea tangu awali, baada ya kujitambulisha kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi.

“Lakini kwa upande wa pili vyama vya upinzani vimeanza kuwa na ‘social base’ (jamii msingi) ambapo makundi ya wasomi, wafanyakazi, watu wenye uelewa, vijana wasio na kazi katika majiji na miji wamekumbatia mabadiliko,” alisema Dk Bana na kuongeza:

“Katika uchaguzi wa mwaka huu watu wote wenye uelewa na wale wanaojitambua wamepigia mabadiliko na hili ni jambo zuri kwa kweli.”

Alifafanua kuwa CCM inapaswa kujiuliza mara mbili zaidi kwamba bado ni chama cha wakulima na wafanyakazi au ni chama cha wafanyabiashara na matajiri.

“Kwa sababu jumuiya za wafanyakazi, wasomi hasa wa vyuo vikuu na vijana wasiokuwa na kazi mijini wote wamejitambulisha kama jamii msingi ya upinzani,” alifafanua.

Alisema katika historia ya dunia siku zote mabadiliko huanzia mjini jambo ambalo limeshaanza kuonekana Tanzania, hivyo ni wazi kabisa kuwa sasa yanaelekea vijijini.

Alisema hadi sasa CCM imebakia kuwa na nguvu vijijini kwa sababu bado teknolojia ya habari na mawasiliano haijajikita katika vijiji vingi nchini jambo ambalo linawafanya baadhi ya wakazi wa huko kukosa sera za mabadiliko.

“Lakini wakiweza kufikiwa na habari hizi za magazeti, redio na televisheni kwa kweli CCM itakuwa katika hali mbaya,” alitabiri Dk Bana.
 

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
Na bado tutawafukuza hata vijijini

Kweli mkuu, kijijini kwetu ilikuwa huwaambii kitu kuhusu CHIHIEMU ila mpaka sasa nina ndugu nimewapa ukweli wa mambo kiasi ukiwatajia CHICHIEMU wanaweza kukutoa baru. Tuwaelimishe wajue CHICHIEMU inapoipeleka nchi kisha 2015 CHICHIEMU :rip: HADI VIJIJINI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom