CCM yafika pabaya: Dk. Kigwangala, Bashe watishiana bastola Nzega! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yafika pabaya: Dk. Kigwangala, Bashe watishiana bastola Nzega!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAKOLE, Aug 29, 2012.

 1. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  KATIKA kile kinachoonekana kama vita ya urais wa mwaka 2015, makundi yanayokinzana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yamedaiwa kuanza mkakati wa kujiimarisha kwa kutumia uchaguzi wa ndani unaoendelea sasa.

  Hatua hiyo vile vile inaelezwa kuwa ni mwendelezo wa visasi vya Uchaguzi Mkuu uliopita katika baadhi ya maeneo, ambapo wagombea wanaokubalika waliachwa na kuchukuliwa wengine.

  Mathalani katika Jimbo la Nzega, mkoani Tabora, visasi hivyo vimedumu baina ya Mbunge wa sasa, Dk. Hamis Kigwangala na kada aliyeenguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa, Hussein Bashe, akidaiwa si raia wa Tanzania.

  Wawili hawa juzi wanadaiwa kutishiana bastola katika ofisi ya CCM wilayani humo wakati wakirejesha fomu za kuomba kuwania nafasi mbalimbali.


  Taarifa kutoka vyanzo vyetu vya ndani ya chama hicho, zinaeleza kuwa miongoni mwa vigogo wanaotajwa kuutaka urais, makundi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na lile la Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, ndiyo yanamsuguano mkali.

  Wakati uchaguzi wa ndani wa CCM ukizidi kupamba moto, makundi hayo yanadaiwa kuwa kila moja linahaha kuhakikisha wale wanaoliunga mkono wanaibuka kidedea katika nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu, Mkutano Mkuu na jumuiya za Wanawake, Wazazi na Vijana kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa.

  Tanzania Daima limedokezwa kuwa katika kuweka mambo sawa, mmoja wa vigogo hao amebaini kutoungwa mkono na wenyeviti wanaomaliza muda wao katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Dar es Salaam na Arusha, hivyo amesuka mkakati ili wasichaguliwe tena.

  "Mkakati huu mchafu na hatari kwa ustawi wa demokrasia unatumia mamilioni ya fedha, maarufu kama ‘mamilioni ya Gadaffi' na unaratibiwa na mmoja wa vigogo anayetajwa kuwa na lengo la kuwania urais mwaka 2015 kupitia CCM," kilisema chanzo chetu.

  Mabilioni hayo ya fedha yanadaiwa kuanza kumwagwa katika mikoa husika ikiwa ni lengo la kuhakikisha wenyeviti hao, Clement Mabina (Mwanza), Hamis Mgeja (Shinyanga), John Guninita (Dar es Salaam) na Ole Nangole wa Arusha hawarudi tena katika nafasi zao.

  Baadhi ya makada wa CCM waliozungumza na gazeti hili, wamewaomba wenyeviti wastaafu wa chama hicho, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa kuingilia kati na kumsadia Rais Jakaya Kikwete kudhibiti matumizi ya fedha katika uchaguzi.

  "Ili kuinusuru CCM katika anguko la kihistoria, tunawaomba sana Mwinyi na Mkapa waingilie kati kuhakikisha wanadhibiti kabisa matumizi ya fedha katika chaguzi zote za ndani," alisema kada mmoja.

  Chanzo chetu kimebaini kuwa kundi hilo limeanza kujipenyeza mikoani kuwachafua viongozi wa CCM wasiofungamana nao, hivyo kuandaa safu yao mpya.

  Kigwangala vs Bashe


  Kuhusu wawili hawa wanaowania ujumbe wa NEC Wilaya ya Nzega, taarifa zinasema kuwa tukio hilo la aibu lilitokea katika ofisi za CCM saa 09:30 alasiri baada ya Dk. Kigwangala kumwambia Katibu wa wa chama wa Wilaya, Kajoro Vyohoroka, asiipokee fomu ya Bashe kwani alikuwa amechelewa kuijaza na kuirejesha.

  Tanzania Daima lilitonywa kuwa baada ya Dk. Kigwangala kumwambia katibu maneno hayo, Bashe akatoa lugha ya matusi kwa mbunge huyo.

  "Kufuatia matusi hayo, Dk. Kigwangala alinyanyuka ghafla na kutaka kumpiga Bashe huku akimtishia kumtandika bastola...lakini baadhi ya wanachama wakawaamulia," kilisema chanzo chetu.

  Katibu wa CCM wa Wilaya ya Nzega, Vyohoroka, alikiri kutokea kwa tukio hilo ofisini kwake juzi na kwamba awali Dk. Kigwangala alikuwa akijaza fomu hiyo ofisini hapo na Bashe alikuwa ofisini kwa Mwenyekiti, Francis Shija.

  Alifafanua kuwa Bashe alirejesha fomu saa 09:50 na Dk. Kigwangala naye alirejesha saa 09:48 lakini kwa mshangao mbunge huyo alitamka kuwa fomu ya Bashe imechelewa hivyo isipokewe.

  Alisema kuwa baada ya hapo ndipo maneno makali yalipoanza hadi kufikia vitisho vya silaha.

  Bashe alizungumza na gazeti hili akisema kuwa Dk. Kigwangala alimtishia kwa bastola akidai fomu yake isipokewe kwani muda wa kurejesha ulikuwa umekwisha.

  "Si kweli kuwa muda ulikuwa umeisha, bali huyu ndugu yangu ana visa na chuki dhidi yangu, ni kweli alichomoa bastola yake lakini wanachama walituamua," alisema Bashe.

  Naye Dk. Kigwangala alikanusha akisema hakuna kitu cha namna hiyo, bali Bashe ni mzushi anayetaka kuyakuza mambo hayo.

  "Si kweli na hamna kitu cha namna hiyo…Bashe anataka kuyakuza tu, ni kweli katibu amembeba muda wa kurejesha fomu ulikuwa umekwisha," alisisitiza.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Anthony Rutta, aliliambia gazeti hili kuwa taarifa za tukio hilo anazo lakini atafuatilia kujua chanzo.

  Chanzo: Tanzania Daima
   
 2. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,540
  Likes Received: 10,465
  Trophy Points: 280
  wamezozana humu jf wamekuta haitoshi bora kutishana live.! Sisi tupo likizo ya siku ya siku tano, ngoja tuendelee kuwachora.!
   
 3. Root

  Root JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,304
  Likes Received: 13,012
  Trophy Points: 280
  wauane wenyewe
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Si wauane tu ili wapungue,
   
 5. m

  malaka JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hahahah. Raha. Ehe risasi au bomu la machozi. Ccm bana.
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Waacheni watishiane, CCM wanazosilaha nyingi sana kama tulivyoambiwa kuwa hazikusajiliwa zilipata baraza za Mwema zitumike na Jeshi la CCM baada ya kuona Policcm wanaanza kushindwa kazi.

   
 7. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  isije ikawa wanagombea tu vile vitumbua jamani
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hawa jamaa inapaswa kuwafatilia kwa umakini, watauana kweli.
   
 9. M

  MLERAI JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Si wauwane turudi kwenye uchaguzi igunga na nzega si jirani.Kama mtu hana sifa analazimisha nini kuwa kiongozi
   
 10. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  ni wa chama cha mapinduzi,chama cha kupinduana kwa hira ,majungu na silaha!
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Hizo ni laana zina waandama maana wamezoe kuwatishia wananchi sasa wanataka kuuana wenyewe!
   
 12. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Wameamua kupelekana mabwepande wao kwa wao
   
 13. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu only83, hivi kuna mtu yeyote mwenye akili timamu anyeweza kuyaonea huruma magamba yanapogombania ufisadi?
   
 14. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ccm wote wanajiruhusu kumiliki silaha.
   
 15. a

  afwe JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Kuna wakati tuliandika kuhusu Dr. Kigwangala kuwa tuwe waangalifu kwani he is not that genuine to keep us discussing his behavior through JF. Ukweli wa mambo unazidi kujidhihirisha
   
 16. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Rais ajae hatatoka Kaskazini -Prince, Rais ajae atatoka Nyanda za juu kusini - Wilson Mukama,Baraza la mawaziri lapongeza kusimamishwa Management ya Tanzania Port Authority, Rais wa 2015 ni.............! Igunga hizo ni Trela picha linakuja soon!
   
 17. we gule

  we gule Senior Member

  #17
  Aug 29, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wananzega hwbu nijuzeni hivi huyu Bashe aliisha ukana UAl-shababu mpaka anataka kugombea ujumbe wa NEC?
   
 18. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni siasa tu? Au wamegongeana mademu au wake zao...
   
 19. only83

  only83 JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Taarifa za sasa ni kuwa polisi mkoani Tabora wilaya ya Nzega imewaweka ndani yaani selo Hussein Bashe pamoja na
  Sango na wafuasi wengine wa Bashe baada ya bwana Sango kumtishia mbunge wa Nzega Kigwangala kwa bastola.

  Chanzo: KITUO CHA POLISI NZEGA
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Toka siasa za maji taka hadi siasa za bunduki!
   
Loading...