CCM yafanikiwa: Movie ya Lwakatare yafunika kabisa unyama dhidi ya Kibanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yafanikiwa: Movie ya Lwakatare yafunika kabisa unyama dhidi ya Kibanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mystery, Mar 21, 2013.

 1. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #1
  Mar 21, 2013
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 8,695
  Likes Received: 8,419
  Trophy Points: 280
  Zipo dalili za wazi kwa hapa nchini kwa sasa kuwa huwa wanafanya timing ya mambo fulani yatokee, ili kuwasahaulisha wananchi kuhusu tukio kubwa lililotokea kabla.

  Usiku wa tarehe 6/03/2013, Mhariri Mtendaji wa Habari Corporations, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, Absolom Kibanda, alivamiwa na watu wasiojulikana akiwa karibu kabisa na nyumbani kwake, na watu hao walimuumiza vibaya hadi kumtoboa jicho, ambapo hivi sasa ametiwa kilema cha maisha, ambapo jicho hilo halitaona tena. Baada ya tukio hilo, vyombo vyote vya habari na wananchi wote walilaani kwa nguvu zote tukio hilo, na kulitaka Jeshi la Polisi liwasake kwa nguvu zote na kuwanasa wahalifu hao.

  Kilichotokea baada ya tukio hilo, likaibuka ghafla suala la kukamatwa kwa mkurugenzi wa usalama wa Chadema, Alfred Lwakatare, ambaye alifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashitaka ya ugaidi kwa ushahidi wa clip ya video iliyochukuchuliwa mwezi Desemba mwaka jana, ikidaiwa kuwa yeye na mwenzake Ludovick walipanga njama za kutaka kumteka Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Deus Msacky.

  Sasa hapa ndipo yanapoibuka maswali lukuki, kuhusiana na hili suala la 'kufikirika' la ugaidi wa akina Lwakatare. Swali la kwanza, je intelejensia ya kikosi cha Polisi cha Mwema kulikuwa likizo hadi tukio la hatari kama hilo la ugaidi, wakae nalo tokea mwezi Desemba mwaka jana hadi kuliibua hivi majuzi tu??!!

  Swali la pili, kama kweli Polisi wako serious na kazi yao, na suala lolote la utekaji nyara mtu, ni tukio la ugaidi, ni kwa nini hadi hivi leo, hawajamkamata Ramadhan Ighondu, ambaye ni mtuhumiwa namba moja wa tukio la kutekwa kwa Dr Ulimboka, ambapo tukio hilo litokea siku za nyuma zaidi, mwezi Desemba mwaka jana??!!

  Swali la tatu, ni kwa vipi hata Mtuhumiwa feki wa Kova, yule chizi wa Kenya, ambaye alifikishwa mahakamani kwa kosa la kumteka Dr Ulimboka, ni kwa nini mtuhumiwa huyo, hajafunguliwa mashitaka ya ugaidi kwa kumteka Dr Ulimboka na badala yake amefunguliwa mashitaka ya Jinai ya kawaida??!!

  Swali la nne, iwapo zipo picha zinazoonyesha wazi mapolisi kadhaa, chini ya usimamizi wa kamanda wao Kamuhanda zilonyesha jinsi wanavyomsulubu Mwangosi mwaka jana, hadi hatimaye kamanda Kamuhanda akamuamrisha yule askari wa cheo cha chini, amfyatulie lile bomu, ambalo lilimchana chana Mwangosi, hadi kumtoa utumbo.

  Ni kwa nini hadi leo kamanda Kamuhanda hajakamatwa na wale askari walioonekana kwenye picha wakimsulubu Mwangosi ili waunganishwe kwenye ile kesi ambayo amefunguliwa askari mmoja tu? Na kwa nini hiyo kesi pia isibadilishwe badala ya kuwa mauaji ya kawaida, yaitwe ni mauaji ya kigaidi??!!

  Ukiangalia huu mlolongo wa matukio ya mauaji ya raia wasio na hatia na kutekwa watu na kuteswa hadi kutiwa vilema vya maisha na watuhumiwa wote hao wanashindwa kutiwa nguvuni, wakati tukio la kuuawa kamanda Barlow kule Mwanza mwaka jana watuhumiwa wake walikamatwa fasta na kufikishwa mahakamani, ni dhahiri huo ni ushahidi tosha kuwa kwenye hayo matukio ambayo watuhumiwa wanashindikana kupatikana, itakuwa ni vyombo vya ulinzi na usalama inavyotekeleza unyama huo kwa kuamrishwa na watawala!!

  Sasa kwa kuwa hatua tuliyofikia sasa ni mbaya sana, ambapo hatuwezi kujua ni mwanaharakati gani anayefuata kuuawa au kunyofolewa kucha, meno na kutobolewa macho, hivi sasa ni wajibu wetu wananchi wote kwa kusadiwa na vyombo vyetu vya habari kushinikiza mfululizo kila siku bila kuchoka kumtaka IGP Mwema na waziri wake wa ndani Nchimbi, wawafikishe mahakamani watuhumiwa wote wa kadhia ya Ulimboka, Mwangosi na Kibanda.

  Tena wote wafunguliwe mashitaka ya ugaidi na hilo likiwashinda wajiuzulu mara moja, shinikizo hilo liendelee bila kukoma hadi wakuu hao wa vyombo vya usalama, waachie ngazi, tusipofanya hivyo maana yake zipo dalili za wazi kuwa hadi ifikapo 2015 wananchi wengi tanaoipinga serikali ya CCM wengi watu tatakuwa hatuna meno, kucha hadi tutakuwa vipofu kutokana na kunyofolewa macho!!

  Tufahamu pia IGP Mwema lazima anapata kiburi hiki kutoka kwa mtu aliyemteua, ambaye ndiye Rais mwenyewe, kwa kuwa haiingii akilini ni kwa nini Rais hamfukuzi kazi IGP Mwema, pamoja na kuwa katika kipindi chake cha kuliongoza Jeshi la Polisi ndiyo kumetokea mauaji mengi zaidi ya raia wasio na hatia na hao watu wengine ambao wanatekwa katika mazingira ya kutatanisha, kuliko vipindi vingine vyote vya ma-IGP wengine, na cha ajabu zaidi watekaji hao na wauaji hao, kamwe hawakamatwi na Jeshi la Polisi!!

  Na zipo dalili za wazi kabisa
  .
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2013
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,615
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 180
  Upo sahii kaka..maccm ni watu wa matukio haramu,wanafanya bak bandua.
   
 3. kistwangara

  kistwangara JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2013
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 657
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  hawawezi kujiudhuru sana, mkuu lazima utambue kuwa tutaendelea kuuliwa cc wote tunaopinga serikali. Hv we unadhani mwanahalisi limefungiwa kwa sababu ya rama wa ikulu. Ngoja labda wanataka kuona watz tukipigana na sijui kwa faida ya nani? Au wao watakuwa hawapo.
   
 4. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2013
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Wana Jf,

  Katika tafakuri yangu juu ya matukio yanayoendelea hivi sasa hapa nchini nahisi kwamba ccm na ikulu wamechez game mbili,
  moja ni kum-"ulimboka" kibanda kiukweli kwa lengo maalum na pili ni ku release mkanda wa kisanii wa lwakatare ili ku divert attention. They knw they would rather use more time and even loose(they knw they will loose) but watu hawata concetrate tena kwenye ishu mbaya kwao ya kibanda.
  Nadhani wanafanikiwa kwa hilo.
  Kibanda issue is theirs 100%, they cant face it!

  Let us not be diverted so easily fellas!
  Ulimboka na Kibanda kuna mkono wa TISS!
  Movie ya lwakatare ilitengenezwa kama dirisha la kuchomokea in case of fire hazard.
  Wanachomoka hata kama watajehuhiwa.
  Ya ulimboka ilitaka kuwaua, wakapona kwa kuua mwana halisi kinyama, ya kibanda inaweza kuwamaliza kabisa, wanatokea kwa lwakatare movie hata kama watakuwa majeruhi lakini angalau watakuwa hai.

  Let us finish them, lets not be diverted.

  Nawakilisha.
   
 5. m

  mshunami JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2013
  Joined: Feb 27, 2013
  Messages: 3,793
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kuwa hakuna nayeongea yaliyomsibu Kibanda tena wakati video ya Lwakatere haina uhusiano wowote na masahibu yaliyompata Kibanda! Anatuhumiwa kupanga kumteka mtu mwingine kabisa! Je nani anahusika kumteke na kumtese Kibanda??? Hata Polisi hawaongelei hilo tena na suidhani hata kama wanajishughulisha nalo. Sisi ndugu, jamaa na marafiki wa kibanda tuna maswali mengi sana juu ya uhusiano wa tukio lile na dola yetu!
   
 6. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2013
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  ni rahisin sana kudivert macho yetu wadanganyika ujue.
  Kwa sasa hot news ni "Lwakatare, Ludovick na bla bla kam hizo
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2013
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,977
  Likes Received: 6,671
  Trophy Points: 280
  aaah wapi!! hiyo ya Kibanda haifi!! kwanza issue ya Lwakatare imefungwa na Lisu leo na wala hutasikia makeke tena!

  Unajua walioandaliwa kuichafua Chadema leo kwanini wameingia mitini?

  CCM wanafanya makosa mengi ya kutia aibu na ndio yameongeza chuki kwao!
   
 8. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2013
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Itakuwa dhambi na usaliti mkubwa dhidi ya haki za binadamu ambayo sote tutaibeba kama tutapumbazwa na hizi cheap ccm/tiss movie arts za lakwatare na kuacha kutaka kwa nguvu zote kujua;
  1.nani walihusika kumfanyizia Kibanda,
  2.walitumwa na nani.
  3.kwa lengo lipi.
  4.kwa nn
  5.nn wasifu wao na ajira zao/mwajiri wao
  6. Hatima ya kibanda na familia na taaluma yake baada ya kudhuriwa na wajibu wa wote waliohusika,individuals and institutions on this mbele ya sheria kwa uwazi na uhuru wa vyombo vyetu vya sheria kwa kadri ya katiba yetu na ya umoja wa mataifa.

  Tusiburuzwe.
  Ss c zao la waziri wa elimu huyu.
   
 9. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2013
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nahisi mastermind ni Mwigulu. Akamtumia Ludovick ku-cut a deal with Lwakatare. Kwakuwa Lwakatare alishapewa mchongo mzima akamweka Msaki kama ndo target na hata modus operandi akai-twist kidogo ili asiwe in trouble with the law. Hivyo Lwakatare, Ludovick na Msaki wakawa kitu kimoja(mawasiliano) wanajua lipi litakalotokea kwa Kibanda. Sitashangaa kama Ludovick ali-oversee the whole plan from start to completion as directed by Mwigulu. Kitu ambacho Mwigulu hakujua ni kwamba mchongo umekuwa twisted kidogo ili kuiangamiza CCM. One million dollar question though is how Ludovick going to be able to walk free!!!
   
 10. M

  Maubero JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 1,533
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Walifanikiwa hata pale walipowaaminisha watanzania kuhusu tiba ya babu wa Loliondo na kusahau matukio makubwa yaliyokuwa yanalisibu taifa hili
   
 11. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2013
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  kibanda,msaki,mwangosi yote kazi ya lwakatale
   
 12. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2013
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Are you serious???
   
 13. m

  mshunami JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2013
  Joined: Feb 27, 2013
  Messages: 3,793
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Hata Mwangosi? Du! Huyu Lwakatare ana nguvu sana hata kumobilize Polisi hadi RPC na kumtumia kwa ugaidi wa kuumuua Mwangisi! Lwakatare basi ana nguvu sana!!!!!!
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2013
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,834
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  sio CCM sema washabiki wa Membe
   
 15. Msenyele

  Msenyele JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2013
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 329
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Prove it! hata mahakama na policcm hawana majibu wewe tayari unayo,nawewe unatakiwa upelelezwe. nirushie namba yako tuanze kazi.
   
 16. Msenyele

  Msenyele JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2013
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 329
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Membe yuko chama gani eti? au washabiki wake wanatoka chama kipi?
   
 17. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2013
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  How DO you KNOW THAT??? What GOES AROUND COMES AROUND!!!
   
 18. Ranks

  Ranks JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 2,599
  Likes Received: 861
  Trophy Points: 280
  Kama kwa usanii wameweza kwenye hili la msacky,yatubidi sasa tuandamane taifa zima kudai washtakiwa wa Ulimboka,Mwangosi,Ally na Kibanda tuwaone mahakamani ili haki itendeke bila kusahau Arusha Jan 5.
   
 19. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2013
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,486
  Likes Received: 1,354
  Trophy Points: 280
  Endelea kujidanganya,huku mitaani kwetu tunajua kazi ya ikulu! Na uzuri wananchi pia wanajua hilo,na tunaendelea kuelimisha uma...
   
 20. ChescoMatunda

  ChescoMatunda JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2013
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,189
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  samahani hivi mrema mwana usalama mtiifu alipona kabisa ama bado ana kisukari? maana yeye ndo alikwenda mpaka tbc kueleza ubora wa dawa na kukuza uzushi kuhusu samonge kwa babu loliondo.
   
Loading...