CCM yaendesha mafunzo ya kijeshi Mbeya

palalisote

JF-Expert Member
Aug 4, 2010
8,335
1,455
HOFU ya vitendo vya kijangili imezuka mkoani hapa baada ya kuwepo kwa tuhuma za kambi tatu zinazoendesha mafunzo ya kijeshi, zikidaiwa kuendeshwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tuhuma hizi nzito zilizotolewa na uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, zimedai kuwa kambi hizo zimeanzishwa kutokana na agizo la Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.
Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija alisema kuwa kambi hizo zimewekwa katika shule tatu za sekondari zinazomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM ambako vijana wa chama hicho wanapatiwa mafunzo ya kijeshi.
Mwambigija alisema kambi hizo zilizoko Ivumwe, Itende na Igawilo, zinaendesha mafunzo hayo huku vijana wakisikika wakitamka maneno ya ‘kata kucha', ‘ng'oa meno', ‘ingiza chupa' na mengine yanayotishia usalama wa watu.
"Tumepata taarifa kuwa vijana hao wanatekeleza maagizo yaliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba. Vijana hao wapo Ivumwe, Itende na Igawilo, wanatamka maneno hatarishi, wakiimba, kata kucha, ng'oa meno, ingiza chupa na mengine hatuwezi kuyataja, ni hatarishi sana," alisema Mwambigija.


Mwenyekiti huyo alisema wamegundua kuwa hatua hiyo inalenga pia kuwatisha wananchi wasijitokeze katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Iyela jijini Mbeya unaotarajiwa kufanyika Juni 16.

>>>Kauli ya RPC

Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Mbeya, Diwani amekiri kupokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa uongozi wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini, na kudai kuwa wanafuatilia suala hilo.
"Tumepata habari hizo na tunafuatilia kwa njia na mbinu zetu, na hadi sasa tunajua kuna mafunzo ya vijana wa CCM yanaendelea," alisema Kamanda Diwani.
Hata hivyo, Kamanda Diwani alidai kuwa wanachojua ni kuwepo kwa mafunzo ya kawaida kwa vijana wa CCM, na ndiyo maana yanafanyika ndani na kwamba hayahatarishi amani na usalama.
"Lakini bado tunawaomba CHADEMA watusaidie kufuatilia na kama watagundua tofauti na haya tunayoyajua hadi sasa, watuarifu. Kwa sasa hatuwezi kumkamata yeyote kama wanavyotaka tufanye," alisema.
 
ccm ni watu wa kwanza kulia na shutuma za kuwa CDM ni chama kinachotaka kuleta fujo na ukosefu wa amani, wakati ukweli siku zote unadhihirisha vinginevyo! Matukio haya yananikumbusha hadithi ya kimapokeo ya mtoto aliyekuwa anapiga kelele za 'mbwamwitu' na watu wakawa wanamwitika. Mwisho wakamzoea, alipokuja kuvamiwa na mbwamwitu wa kweli hakuna aliyeamini, walipokuja kesho yake wakakuta ameuawa.

Watanzania wa 2013 sio wale wa 2010. Uongo wa ccm unaonekana wazi. Mwigulu na timu yako siku zenu zinahesabika. Hakuna jeshi lolote duniani linaloweza kushinda nguvu ya umma! Ulizeni wenzenu ulimwenguni kote. Hitler alitisha dunia, jiulize aliishia wapi?
 
Othmani mbwana bawji oyeeee
Huyo ndio diwani wa mbagala mgombea anaependwa na watu....mleta maendeleo wa CCM, anaekubalika chadema mnakazi kweli mana ameshapita.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
images
Watanzania wasipolitoa hili joka 2015 ni balaa!!
 
Na hatimaye kamanda wa polisi mkoa wa mbeya amearumu kufunga kwa kambi hizo.
Swali je kamanda umedhibitisha kuwa wanajiandaa kutung'oa kucha nataman ungekuwepo JF nikupongeze kwa kazi nzuri ya kusimamia usalama wetu mbeya nakushukur xana.sana tuna aman na Maisha yetu hamna kung'oana kucha
 
Siku zote CCM inaendelea kwa vitisho, Siku ikiacha ujue imekwisha.
Mikutano na Mikusanyiko ya raia bila Askari = Hakuna uharibifu.
Inteljensia na ulinzi maridhawa + Mabomu ya machozi = Uvunjifu wa manani na vurugu.
 
Back
Top Bottom