CCM yaendelea kusisitiza ushirikiano wa asasi za kiraia nchini katika utetezi wa kisera

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
*CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAENDELEA KUSISITIZA USHIRIKIANO NA ASASI ZA KIRAIA NCHINI KATIKA UTETEZI WA KISERA WA MASUALA YA WANANCHI*

26 Oktoba 2018

Katika Mkutano wa wiki ya Asasi za kiraia Nchini Jijini Dodoma, Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi ameendelea kusisitiza ushirikiano na Asasi za Kiraia Nchini katika utetezi wa kisera wa masuala ya wananchi.

Akifafanua suala hilo Ndg. Poleple amesema CCM ipo tayari muda wote kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwepo Asasi za kiraia ikiwa ni sehemu ya kufanikisha marekebisho, mabadiliko na mageuzi ya kisera yanayohusu masuala na maendeleo ya wananchi na kwamba CCM ipo tayari kusikiliza na kufanyiakazi maoni mazuri ya wananchi wote.

Aidha akijibu swali juu ya nini ushauri wake kwa Viongozi Vijana Ndg. Polepole ametumia mkutano huo kuwakumbusha Viongozi Vijana kutumia muda wao mwingi kujifunza, kujiendeleza kielimu, kuwa wanyenyekevu, kuwa wasikivu na kumcha Mungu kwakuwa ndio siri ya mafanikio katika maisha.

*"Siri kubwa ya kufanikiwa kwa Vijana ni kupenda kujifunza, kusoma, kusikiliza zaidi, kuwa wanyenyekevu na wamshirikishe Mungu katika kila jambo"* amesema Ndg. Polepole

Ndg. Polepole amewashukuru sana Shirika linalotoa Ruzuku kwa Asasi za Kiraia (FCS) kwa kumualika katika tukio hilo muhimu.

Huu ni muendelezo wa kazi za Chama, nje ya Chama ndani ya Jamii.

Imetolewa na
*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI*
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
 
Back
Top Bottom