CCM yaendelea kupimana ubavu na kanisa katoliki Sumbawanga.......

Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
639,488
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 639,488 280
Kanisa Katoliki lagoma kuzika

Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga; Tarehe: 14th December 2010 @ 08:00

KANISA Katoliki Parokia ya Familia Takatifu Jimbo la Sumbawanga, limegoma kuendesha ibada ya maziko kwa marehemu wawili wakidai ibada haitaendelea mpaka pale waumini ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotengwa na kanisa hilo, watakapoondoka ndani ya kanisa hilo.

Marehemu hao ni aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Msua iliyopo Manispaa ya Sumbawanga, Mekitrida Maufi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Rukwa ambaye pia kwa sasa ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa, Patrick Maufi.

Maiti nyingine ambayo jina lake halikuweza kupatikana mara moja, ni ya mtoto wa darasa la nne ambaye pia shule aliyokuwa akisoma haijajulikana.

Tukio hilo lilitokea jana saa 8 mchana na lilidumu kwa saa tatu pale waombolezaji walipoleta miili ya marehemu hao kanisani hapo kwa ibada ya maziko.

Wengi wa waombolezaji hao walikuwa ni wanaCCM wakimsindikiza mfiwa na wengi wao walikuwa wameshatengwa kwa kinachodaiwa kuwa waliisaliti imani yao ya dini wakati wa Uchaguzi Mkuu kwa kumshabikia mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aesh Hilaly.

Baada ya waombolezaji kufika na majeneza ya miili hiyo mbele ya milango ya kanisa wakiwa tayari kuingia ndani, yalisomwa matangazo yaliyodai kuwa ibada ya kuombea marehemu haiwezi kufanyika hadi waumini waliotengwa (wanaCCM), watawanyike na wasionekane nje wala katika maeneo ya karibu na kanisa hilo.

Miongoni mwa waumini hao waliohudhuria, lakini wametengwa ni pamoja na mwenyekiti wa CCM Mkoa, Hypolitus Matete, Mwenyekiti CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini, Charles Kabanga, Katibu wa CCM Mkoa, Fraten Kiwango, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini aliyefahamika kwa jina moja la Tumombe na Diwani wa CCM Viti Maalumu Kata ya Sumbawanga, Aurelia Kanyengele.

Hali hiyo iliibua dhahama na kusababisha vurugu ya makundi mawili kati ya waliyotengwa na wanaounga mkono maamuzi hayo ambayo yalitiliwa nguvu na Paroko wa Parokia ya Kristu Mfalme, Pambo Mlongwa aliyefika maeneo hayo na kuwashinikiza mapadri waliokuwepo pale kuendelea na msimamo huo huo na kuwafanya waumini kuwataka waliokataliwa waondoke ili ibada ifanyike.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mjini, John Mzurikwao aliwataka waumini hao kwa kuwa wametengwa, watii maamuzi hayo na kuwasihi kuondoka hapo ili utaratibu wa ibada ya mazishi uendelee.

Viongozi hao baadhi walikubali na kurejea msibani, lakini baadhi ya waliotengwa walitoka nje ya uzio na kusubiri miili ya marehemu ili waungane na wenzao ili kwenda mazikoni. Ibada ya mazishi iliendelea.

Francis Chale ambaye ni Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM Wilaya ya Sumbawanga akizungumza na gazeti hili, alikiri si kutengwa tu, bali alivuliwa ukatoliki wake, akituhumiwa kumshabikia Hilaly ambaye ni Muislamu, aliyetuhumiwa na kanisa hilo kwa kuukufuru utatu mtakatifu katika moja ya mikutano yake ya kampeni alipojifananisha na Yesu Kristo kwa kuelezea dhana nzima ya mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani.

“Kitendo hiki kimetusikitisha sana, tulidhani kwamba tumezuiwa tu kuhudhuria ibada za misa takatifu kumbe hata ibada za mazishi. Sasa kama hali ndio hiyo na kanisa linajitambulisha kwamba ni wakala wa Chadema, basi na sisi tuliotengwa tunajipanga tupandishe bendera ya Chadema kwa kila Parokia iliyopo katika jimbo hili,” alidai Chale.

Hivi karibuni, Parokia kadhaa za Jimbo Katoliki limewasimamisha waumini wake kwa madai ya kuisaliti imani yao kwa kutotii imani ya kanisa ambayo yaliwataka wasishabikie mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Katika msuguano huo wa kiimani, tayari kanisa hilo limewasimamisha na kuwatenga makatekista kwa madai wamelisaliti kanisa kwa kuwahamasisha waumini wao kumshabikia mgombea wa CCM.

Hata hivyo, kutokana na mchakato huo, kanisa hilo linajiandaa kutangaza orodha ya mapadri waliolisaliti hadharani ili nao waadhibiwe kama walivyoadhibiwa waumini hao.
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
639,488
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 639,488 280
CCM Sumbawanga hawapo pekee yao..................Wakati wa kampeni za kule Mwanga.................huyu Dr. David Mathayo aliimba nyimbo za kanisani kama mbinu za kumnadi bosi wake JK na huku akibadilisha majina ya watakatifu na kuliingiza la JK...........ni ajabu hadi leo kanisa Katoliki halijamchukulia hatua mbambaishaji huyu.....................
 
MKUNGA

MKUNGA

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2009
Messages
442
Likes
6
Points
35
MKUNGA

MKUNGA

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2009
442 6 35
Dini + siasa = matatizo kama hayo
 
M

Mkerio

Member
Joined
Mar 12, 2006
Messages
35
Likes
0
Points
0
M

Mkerio

Member
Joined Mar 12, 2006
35 0 0
CCM Sumbawanga hawapo pekee yao..................Wakati wa kampeni za kule Mwanga.................huyu Dr. David Mathayo aliimba nyimbo za kanisani kama mbinu za kumnadi bosi wake JK na huku akibadilisha majina ya watakatifu na kuliingiza la JK...........ni ajabu hadi leo kanisa Katoliki halijamchukulia hatua mbambaishaji huyu.....................
Tatizo la wakristo ni wapole sana. Ingekuwa ni Mkristo amemkufuru Mtume ungewaka moto na angetangaziwa fatwa. Huwezi kulinganisha utatu mtakatifu na visiasa vyako.
 
Ndachuwa

Ndachuwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2006
Messages
4,855
Likes
1,102
Points
280
Ndachuwa

Ndachuwa

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2006
4,855 1,102 280

Kwani yeye ni muumini wa Kanisa Katoliki?
 
M

mbezibeach

Senior Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
119
Likes
0
Points
0
M

mbezibeach

Senior Member
Joined Oct 4, 2010
119 0 0
Hivi CCM Makao makuu kimetoa kauli gani dhidi ya huyo Aeshy..? Pinda hajui kinachoendelea hapo..? Ninaamini huenda hao jamaa wa katoliki Sumbawanga wapo right..la sivyo Policarp angekuwa ashawashukia kama mwewe..

USIDHARAU IMANI YA MWENZAKO...KWANI NDIYO INAYOMPA MATUMAINI DUNIANI
 
Bramo

Bramo

JF Bronze Member
Joined
Oct 21, 2009
Messages
9,983
Likes
3,141
Points
280
Bramo

Bramo

JF Bronze Member
Joined Oct 21, 2009
9,983 3,141 280
I see,i was not aware of what was reported,ila Baada ya kusoma hiyo habari ingawa haindenani na kichwa cha habari,niemgundua kuwa kuna Mpango mchafu wa kulihusisha Kanisa Katoliki na CHADEMA,kwa mtazamo wangu hii sio sahihi kabisa,ukuiangalia kwa undani zaid utagundua kuwa Hapo suala sio kumshabikia Mgombea wa CCM (Kama watu wanavyojaribu kupotosha),hapo suala ni Kuwaadhibu waumini waliokuwa wanamshabikia Mgombea ambaye amekufuru IMANI YA KANISA Kwa kjuifananisha na YESU KRISTU,na kumfananisha Mkwere na Mungu,hata kama mgombea huyo angekuwa ni CHADEMA,NCCR,TLP,CUF nk Kanisa lingechukua uamuzi huohuo,mimi sioni suala la CHADEMA hapo linakujaje,watu wanajaribu kuchochea udini ambao kimsingi haupo Tanzania,imekuwa kila mara Kanisa KATOLIKI linapokemea vitendo vya Ufisadi wether umefanywa na watu wa CCM au la CCM imekuwa ikijistukia na kusema KANISA linawachukia,mie sioni msingi wa hili kabisa especialy wa kulihusisha KANISA katoliki na CHADEMA.
Mtu hawezi akakufuru IMANI ya KANISA,halafu wewe muumini wa IMANI hiyo ukaendelea kumshabikia,hiyo ni technically utakuwa na wewe unashabikia ukiukwaji wa KANUNI za KANISA na KINISA lna kila sababu za kukutenga (Mungu amewapa Mamlala M Padre wa Kania KATOLIKI kuwafungia watu Duniani,na hakika watakuwa wamefungiwa MBINGUNI pia,hii ni kwa mujibu wa KANUNI za KANISA KATOLIKI,kama muumini wa KANISA unapaswa kuzi obey,kama huwezi toka nje ya KANISA kama alivyofanya Martin Lutherna usiharibu MAPOKEO ya KANISA).
Me naona CCM ndo wanachochea haya Mambo,na hawajui tu,moto wanaoukoka siku ukiwaka hawataweza kuuzima asilaani,kila Mara KANISA likikemae UFISADI,CCM wanaibuka na kusema wao ndo wanasemwa,sijui Msingi wa hili though najua MAFISADI wako CCM na sehemu nyingine Pia.
Kila Mkatoliki siku alipobatizwa alisema "Nitatii dini katoliki Mpaka kufa" na hiki kiapo kinarudiwa tena siku ya KIPAIMARA,sasa kama wewe ni Mkatoliki,then unshabikia Mtu anayekufuru KANISA kwa kujifananisha na YESU (e.g Karamagi) unataka KANISA likuchekee!!!
 
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
7,236
Likes
326
Points
180
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
7,236 326 180
Hivi CCM Makao makuu kimetoa kauli gani dhidi ya huyo Aeshy..? Pinda hajui kinachoendelea hapo..? Ninaamini huenda hao jamaa wa katoliki Sumbawanga wapo right..la sivyo Policarp angekuwa ashawashukia kama mwewe..

USIDHARAU IMANI YA MWENZAKO...KWANI NDIYO INAYOMPA MATUMAINI DUNIANI
Mkuu, Nimeweka msisitizo hapo kwenye Blue. Kiini cha Tatizo lililoko Sumbawanga ni Pinda mwenyewe. Hili analijua, Mzindakaya na wenzake wanalijua hata viongozi wa CCM Mkoa, Wilaya, Taifa na wananchi wote wa sumbawanga wanalifahamu.

Wananchi wa Sumbawanga walikuwa wamemkataa Aeshy kuwa mbunge wao na yeye mwenyewe alikuwa amekubali kushindwa. Kabla ya kusaini kukubali kuwa ameshindwa ubunge, alimconsult Pinda ambaye wakati huo alikuwa kijijini kwao Mpanda. Pinda laitumia magari ya serikali akaja sumbawanga kama waziri mkuu kwa zaidi ya maili 70 kutoka mpanda (inasemekana alikuwa na masanduku matatu yaliyojaa kura feki) alipofika kulitokea mvutano mkali sana kiasi kwamba watu walitaka kuchoma moto jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa.

Pinda kwa ujasiri huku akijua kuwa mshindi wa halali ni Ndg Yamsebo wa CHADEMA alimlazimisha msimamizi wa uchaguzi amtangaze mtu wa CCM kuwa mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini. Jambo hilo limeleta mtafaruku mkubwa kati ya Pinda na hata wanasiasa waandamizi wa ccm mkoa wa rukwa wakiongozwa na Mzindakaya ambao hawakukubaliana na uamuzi wa ccm wa kumsimamisha Aishey kuwa mgombea wa Ubunge Tangu mwanzo.

Wengi tunajua kuwa Pinda alilazimishwa na either Makamba, JK au RA kuwa asipolazimisha hivyo hatapata U-PM.
 
Chizi Fureshi

Chizi Fureshi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Messages
1,710
Likes
141
Points
160
Chizi Fureshi

Chizi Fureshi

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2010
1,710 141 160
Kwa taarifa, sakramenti walizofungiwa waamini hao ni zote. Km upako, ndoa, upadri km wanautaka, ubatizo. Hatua hii huo ni pigo kuwa. Tuitafakari.
 
mgen

mgen

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Messages
18,509
Likes
3,033
Points
280
mgen

mgen

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2010
18,509 3,033 280
Tatizo la wakristo ni wapole sana. Ingekuwa ni Mkristo amemkufuru Mtume ungewaka moto na angetangaziwa fatwa. Huwezi kulinganisha utatu mtakatifu na visiasa vyako.
Ni kweli mwanangu Hata hivyo Yesu ametufundisha IWENI WAPOLE KAMA HUA LAKINI MUWE WEREVU KAMA NYOKA PIA fundisho jingine tunaelekezwa kuwa MAMBO MENGINE HAYAWEZEKANI BALI KWA KUFUNGA NA KUSALI ILI MUNGU MWENYEZI AINGILIE KATI NA KUTOA HUKUMU YA HAKI!
 
Ndachuwa

Ndachuwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2006
Messages
4,855
Likes
1,102
Points
280
Ndachuwa

Ndachuwa

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2006
4,855 1,102 280
Mkuu, Nimeweka msisitizo hapo kwenye Blue. Kiini cha Tatizo lililoko Sumbawanga ni Pinda mwenyewe. Hili analijua, Mzindakaya na wenzake wanalijua hata viongozi wa CCM Mkoa, Wilaya, Taifa na wananchi wote wa sumbawanga wanalifahamu.

Wananchi wa Sumbawanga walikuwa wamemkataa Aeshy kuwa mbunge wao na yeye mwenyewe alikuwa amekubali kushindwa. Kabla ya kusaini kukubali kuwa ameshindwa ubunge, alimconsult Pinda ambaye wakati huo alikuwa kijijini kwao Mpanda. Pinda laitumia magari ya serikali akaja sumbawanga kama waziri mkuu kwa zaidi ya maili 70 kutoka mpanda (inasemekana alikuwa na masanduku matatu yaliyojaa kura feki) alipofika kulitokea mvutano mkali sana kiasi kwamba watu walitaka kuchoma moto jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa.

Pinda kwa ujasiri huku akijua kuwa mshindi wa halali ni Ndg Yamsebo wa CHADEMA alimlazimisha msimamizi wa uchaguzi amtangaze mtu wa CCM kuwa mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini. Jambo hilo limeleta mtafaruku mkubwa kati ya Pinda na hata wanasiasa waandamizi wa ccm mkoa wa rukwa wakiongozwa na Mzindakaya ambao hawakukubaliana na uamuzi wa ccm wa kumsimamisha Aishey kuwa mgombea wa Ubunge Tangu mwanzo.

Wengi tunajua kuwa Pinda alilazimishwa na either Makamba, JK au RA kuwa asipolazimisha hivyo hatapata U-PM.
Sidhani kama mada inajadili ushindi wa Ubunge wa Sumbawanga mjini bali kukashifu imani ya kanisa katoliki
 
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
7,236
Likes
326
Points
180
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
7,236 326 180
Sidhani kama mada inajadili ushindi wa Ubunge wa Sumbawanga mjini bali kukashifu imani ya kanisa katoliki
Basi kama hujui kuwa chanzo ni hicho. Umedandia gari kwa mbele.

NB: Utatu Mtakatifu si imani ya kikatoliki, ndiyo msingi wa Ukristo na Utimilifu wa maisha ya umilele wa mwanadamu-wokovu wetu. Ndiye Mungu Mwenyewe-Yehova. Si ukatoliki kwa sababu Mungu (YEHOVA) si mkatoliki, umekaririshwa vibaya.
 
Kaa la Moto

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
7,700
Likes
202
Points
160
Kaa la Moto

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
7,700 202 160
Kanisa Katoliki lagoma kuzika

Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga; Tarehe: 14th December 2010 @ 08:00

KANISA Katoliki Parokia ya Familia Takatifu Jimbo la Sumbawanga, limegoma kuendesha ibada ya maziko kwa marehemu wawili wakidai ibada haitaendelea mpaka pale waumini ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotengwa na kanisa hilo, watakapoondoka ndani ya kanisa hilo.

Marehemu hao ni aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Msua iliyopo Manispaa ya Sumbawanga, Mekitrida Maufi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Rukwa ambaye pia kwa sasa ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa, Patrick Maufi.

Maiti nyingine ambayo jina lake halikuweza kupatikana mara moja, ni ya mtoto wa darasa la nne ambaye pia shule aliyokuwa akisoma haijajulikana.

Tukio hilo lilitokea jana saa 8 mchana na lilidumu kwa saa tatu pale waombolezaji walipoleta miili ya marehemu hao kanisani hapo kwa ibada ya maziko.

Wengi wa waombolezaji hao walikuwa ni wanaCCM wakimsindikiza mfiwa na wengi wao walikuwa wameshatengwa kwa kinachodaiwa kuwa waliisaliti imani yao ya dini wakati wa Uchaguzi Mkuu kwa kumshabikia mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aesh Hilaly.

Baada ya waombolezaji kufika na majeneza ya miili hiyo mbele ya milango ya kanisa wakiwa tayari kuingia ndani, yalisomwa matangazo yaliyodai kuwa ibada ya kuombea marehemu haiwezi kufanyika hadi waumini waliotengwa (wanaCCM), watawanyike na wasionekane nje wala katika maeneo ya karibu na kanisa hilo.

Miongoni mwa waumini hao waliohudhuria, lakini wametengwa ni pamoja na mwenyekiti wa CCM Mkoa, Hypolitus Matete, Mwenyekiti CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini, Charles Kabanga, Katibu wa CCM Mkoa, Fraten Kiwango, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini aliyefahamika kwa jina moja la Tumombe na Diwani wa CCM Viti Maalumu Kata ya Sumbawanga, Aurelia Kanyengele.

Hali hiyo iliibua dhahama na kusababisha vurugu ya makundi mawili kati ya waliyotengwa na wanaounga mkono maamuzi hayo ambayo yalitiliwa nguvu na Paroko wa Parokia ya Kristu Mfalme, Pambo Mlongwa aliyefika maeneo hayo na kuwashinikiza mapadri waliokuwepo pale kuendelea na msimamo huo huo na kuwafanya waumini kuwataka waliokataliwa waondoke ili ibada ifanyike.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mjini, John Mzurikwao aliwataka waumini hao kwa kuwa wametengwa, watii maamuzi hayo na kuwasihi kuondoka hapo ili utaratibu wa ibada ya mazishi uendelee.

Viongozi hao baadhi walikubali na kurejea msibani, lakini baadhi ya waliotengwa walitoka nje ya uzio na kusubiri miili ya marehemu ili waungane na wenzao ili kwenda mazikoni. Ibada ya mazishi iliendelea.

Francis Chale ambaye ni Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM Wilaya ya Sumbawanga akizungumza na gazeti hili, alikiri si kutengwa tu, bali alivuliwa ukatoliki wake, akituhumiwa kumshabikia Hilaly ambaye ni Muislamu, aliyetuhumiwa na kanisa hilo kwa kuukufuru utatu mtakatifu katika moja ya mikutano yake ya kampeni alipojifananisha na Yesu Kristo kwa kuelezea dhana nzima ya mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani.

"Kitendo hiki kimetusikitisha sana, tulidhani kwamba tumezuiwa tu kuhudhuria ibada za misa takatifu kumbe hata ibada za mazishi. Sasa kama hali ndio hiyo na kanisa linajitambulisha kwamba ni wakala wa Chadema, basi na sisi tuliotengwa tunajipanga tupandishe bendera ya Chadema kwa kila Parokia iliyopo katika jimbo hili," alidai Chale.

Hivi karibuni, Parokia kadhaa za Jimbo Katoliki limewasimamisha waumini wake kwa madai ya kuisaliti imani yao kwa kutotii imani ya kanisa ambayo yaliwataka wasishabikie mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Katika msuguano huo wa kiimani, tayari kanisa hilo limewasimamisha na kuwatenga makatekista kwa madai wamelisaliti kanisa kwa kuwahamasisha waumini wao kumshabikia mgombea wa CCM.

Hata hivyo, kutokana na mchakato huo, kanisa hilo linajiandaa kutangaza orodha ya mapadri waliolisaliti hadharani ili nao waadhibiwe kama walivyoadhibiwa waumini hao.
Source ni gazeti gani? isije kuwa uhuru, habari leo, mtanzania toiletpapers
 
Plato

Plato

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Messages
421
Likes
5
Points
33
Plato

Plato

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2010
421 5 33
uandishi wa habari wa habari leo ni wa uchochezi.wanadhani kanisa katoliki ni mbumbumbu kama ccm.canon law imeainisha makosa ambayo mkatoliki yeyote akifanya anatengwa.
Kutia neno ccm kila baada ya waliotengwa,maskini habari leo wanadhani kanisa litahofia kuhusishwa na ubaguzi wa kisiasa,mbinu chakavu.
Angalia karibuni watatenga hata mapadre wanaotaka umaarufu rahisi kwa kusaliti mafundisho ya kanisa pia.yuko wapi askofu jacob koda wa same? Alitengwa kwa kusaliti imani ya kanisa. Akina askofu milingo,lukanima nk.
Wakuu adhabu hiyo kwa kilatini inaitwa ferendae sententiae excomunicationae.
 
Gsana

Gsana

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Messages
4,413
Likes
417
Points
180
Gsana

Gsana

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2010
4,413 417 180
Si uyo mbunge Hilarly alisema Jk ni Mungu baba,yeye mungu mwana/Yesu Kristo, na madiwani Roho Mtakatifu sasa hao wafiwa kwa nini wasiende kwa Mungu hao wa imani nyingne ili waweze kupatja msaada wa kiroho? Au tuendelee na mzaha wa kujiita mungu,nabii,mchungaji wakati hatutoi huduma? Au umungu wa Jekey ni wa kumteua mama Rwakatare awe mchungaji kule bungeni na kisha umungu unakoma au? Ama kweli, Ukistaajabu ya Musa,...!
 
Plato

Plato

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Messages
421
Likes
5
Points
33
Plato

Plato

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2010
421 5 33
mashahidi wa YEHOVA hawaamini kama yesu ni mwana wa mungu, wala hawaamini utatu mtakatifu,hivyo suala hili kwao ni kama waislamu
 
Gsana

Gsana

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Messages
4,413
Likes
417
Points
180
Gsana

Gsana

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2010
4,413 417 180
Basi kama hujui kuwa chanzo ni hicho. Umedandia gari kwa mbele.

NB: Utatu Mtakatifu si imani ya kikatoliki, ndiyo msingi wa Ukristo na Utimilifu wa maisha ya umilele wa mwanadamu-wokovu wetu. Ndiye Mungu Mwenyewe-Yehova. Si ukatoliki kwa sababu Mungu (YEHOVA) si mkatoliki, umekaririshwa vibaya.
mbona utaki kumuelewa mwenzio? Kwani wakatoliki sio wakristo? Sasa mbona unasema utatu mtakatifu si wa wakatoliki? Kama ni wa wakristo basi na wakatoliki wamo ila vicent augustino kainsist on wakatoliki, Utingo upo hapo,au umeshuka?
 
Kaa la Moto

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
7,700
Likes
202
Points
160
Kaa la Moto

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
7,700 202 160
Hii ilishawahi kuletwa hapa na tulilijadili vizuri. Naona Ruta amerudisha tena baada ya tukio jingine kuhusu kisa kile kile.
Wale mapadre walishatoa sababu zao kuwa hawa watu walikaidi kanisa kwa kufanya siasa ndani ya kanisa pale walipokuwa wakijihusisha na kupiga kampeni kanisani. Hata walipozuiliwa hawakutaka kutii. Nadhani kwa sababu ya kiburi kile kile cha wana ccm wakidhani kanisani hawatawafanya lolote kwa kuwa wao ni wana ccm.
Sasa kanisa limefungua makucha yake na wao kwa kutafuta public sympathy wanakuja na hoja kwamba wanatengwa kwa sababu ya u-ccm wao. Hilo haliwezi kuwasaidia. Wanaongeza makosa juu ya makosa ambayo hayatawasaidia. Watubu kuwa walikosa wasamehewe warudi kundini. La sivyo wakiwa kichwa ngumu wawe wapagani. Full stop.
 
Bantugbro

Bantugbro

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2009
Messages
2,934
Likes
525
Points
280
Bantugbro

Bantugbro

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2009
2,934 525 280
Si uyo mbunge Hilarly alisema Jk ni Mungu baba,yeye mungu mwana/Yesu Kristo, na madiwani Roho Mtakatifu sasa hao wafiwa kwa nini wasiende kwa Mungu hao wa imani nyingne ili waweze kupatja msaada wa kiroho? Au tuendelee na mzaha wa kujiita mungu,nabii,mchungaji wakati hatutoi huduma? Au umungu wa Jekey ni wa kumteua mama Rwakatare awe mchungaji kule bungeni na kisha umungu unakoma au? Ama kweli, Ukistaajabu ya Musa,...!
Na kama wakiendelea na ubishi wao wa ku-mix u-CCM na dini watapata shida sana kuishi katika mkoa ulio ktk himaya ya RC kama Rukwa.

Maana shule karibia zote ni zao, dispensari, na hospitali nzuri zote ni zao, hata baa na vijiwe vya Chimpumu vinamilikiwa na waumini wa RC...ooh! nimesahau kuwa hata mkulu Pengo nae anatoka hukohuko...

Nawashauri jamaa waende tu wakatubu ili wasiendelee kutengwa...
 
samora10

samora10

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2010
Messages
7,197
Likes
2,360
Points
280
samora10

samora10

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2010
7,197 2,360 280
Hii ilishawahi kuletwa hapa na tulilijadili vizuri. Naona Ruta amerudisha tena baada ya tukio jingine kuhusu kisa kile kile.
Wale mapadre walishatoa sababu zao kuwa hawa watu walikaidi kanisa kwa kufanya siasa ndani ya kanisa pale walipokuwa wakijihusisha na kupiga kampeni kanisani. Hata walipozuiliwa hawakutaka kutii. Nadhani kwa sababu ya kiburi kile kile cha wana ccm wakidhani kanisani hawatawafanya lolote kwa kuwa wao ni wana ccm.
Sasa kanisa limefungua makucha yake na wao kwa kutafuta public sympathy wanakuja na hoja kwamba wanatengwa kwa sababu ya u-ccm wao. Hilo haliwezi kuwasaidia. Wanaongeza makosa juu ya makosa ambayo hayatawasaidia. Watubu kuwa walikosa wasamehewe warudi kundini. La sivyo wakiwa kichwa ngumu wawe wapagani. Full stop.

asante kwa kunyambulisha vizuri mkuu!
 
Forum statistics

Threads 1,238,898
Members 476,226
Posts 29,336,070