CCM yadaiwa kuihujumu Chadema Geita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yadaiwa kuihujumu Chadema Geita

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 3, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMATANO, OCTOBA 03, 2012 06:21 NA VICTOR BARIETY, GEITA

  BAADHI ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Geita, wanadaiwa kupanga njama za kukidhoofisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Chama hicho kinadaiwa kufanya hivyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, kuihujumu Chadema katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Lwezera zinazoanza Oktoba 6 mwaka huu.

  Tayari Jeshi la Polisi wilayani hapa, linamsaka aliyekuwa Diwani wa Kata ya Sombetini, kupitia CCM, kabla ya kuhamia Chadema, Alphonce Mawazo.

  Mawazo ambaye anafanya mikutano ya Chadema chini ya kaulimbiu ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), anatafutwa kwa tuhuma za uchochezi.

  Baadhi ya viongozi wa Chadema wilayani hapa wameeleza kuwa, kutafutwa kwa Mawazo ni sehemu ya mkakati huo wenye lengo la kuwatisha wafuasi wa chama hicho.

  Wamesema kuwa, mkakati huo unalenga kuzuia viongozi wa kitaifa wa Chadema walioletwa wilayani hapa, kuongeza nguvu katika kampeni hizo.

  Taarifa hizo zinasema, katika mpango huo, baadhi ya viongozi wa CCM wamepanga kuwakamata na kuwafungulia kesi viongozi wa Chadema waliokuja Geita, kuhakikisha kata ya Lwezera ambayo awali ilikuwa ya CCM inarudi mikononi mwa Chadema.

  Mawazo anadaiwa kuchochea vurugu katika mkutano wa uzinduzi wa M4C uliofanyika juzi katika viwanja vya magereza, uliohutubiwa na Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje (CHADEMA).

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jeshi la Polisi wilayani hapa, Mawazo anatafutwa kwa tuhuma za uchochezi, ambapo wakati akihutubia katika mkutano huo, aliwahamasisha wananchi kutokubali kunyanyaswa na jeshi hilo na kusema kuwa jeshi hilo linatumika vibaya.

  Tuhuma nyingine ni kwamba, katika mkutano huo Mawazo alidai kuwa, Mkuu wa Wilaya ya Geita (DC) alipata wadhifa huo kwa hisani ya Rais Jakaya Kikwete.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  POLICE wa CCM wanawapokea CUF Aiport kwa NGOMA na VIGELEGELE; Lakini Wanawafuata CHADEMA

  Majimboni kwa SILAHA ZA MOTO na HARI ya KUUA... Sasa CHADEMA sio CHAMA sahihi cha UPINZANI ?
   
 3. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Upinzani unaokumbatiwa na anayepingwa huo sio upinzani wa kweli.
   
 4. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Pamoja mkuu,upinzani nikupambana.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  These kuna akina Mawazo wengi sana sasa watawakamata wote then magereza si yatakuwa yamejaa watuhumiwa ? Na kweli wanaweza kupingana na ukweli au wanataka na wao kujaribu ?
   
Loading...