CCM yadai mwaka huu ni wao haswaaaa lakini JK kuwakwepa hawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yadai mwaka huu ni wao haswaaaa lakini JK kuwakwepa hawa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Nov 15, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,012
  Trophy Points: 280
  CCM yadai mwaka huu ni waakinamama kufuatia uteuzi wa CC kwenye nafasi ya Uspika lakini uteuzi huo ni wa kumuenzi Mama Anne Makinda pekee kama Makinda na wala siyo wanawake kwa sababu Makinda ana fikra zinazoshahibiana na hiyo CC.........................HUYU NI MWENZETU.........

  Lakini wapo hawa waheshimiwa wabunge wawili ambao tafakuri zao zatofautana na CC hususani JK ambaye hupendelea kuteua viongozi ambao watamsujudia yeye na kumsifia mara kwa mara.....kuwa haya ni mawazo ya Raisi Jakaya Mrisho Kikwete............au Raisi wetu Kikwete ametuagiza tufanye a, b, c,...........huku wakificha hayo ni mawazo yao wenyewe au ya wasaidizi wao..........

  Viongozi wengi serikalini hivi sasa hata mawazo yao na ubunifu wao hum'milikisha JK ili wasije kuonekana wanatofautiana naye au wanajitutumua kuwa ni viongozi bora kuliko yeye..............Waogopa kuonekana wanamfunika bosi wao...................

  Mtihani kwa JK ni kama kweli amenuia kuwaenzi akina mama katika uongozi kuna hawa wabunge machachari wa CCM je atawateua kuwa mawaziri kwenye wizara nyeti na kutohofu waheshimiwa hawa kumfunika yeye?

  Waheshimiwa wabunge hao ni :-

  a) Mheshimiwa Prof. Anna Tibaijuka...............

  b) Mheshimiwa Anne Kilango Malecela.....................

  Asipofanya hivyo basi teuzi za CC aliyoisimamia yeye mwenyewe kwa Anne Makinda kuwa Spika lilikuwa ni changa la usoni tumetupiwa wanaharakati wa maendeleo.......itabidi tushtuke ya kuwa kumbe mwanamke CCM huinuliwa juu juu kama waona wanaweza kumtumia watakavyo...........
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Mhh Prof.Tibaijuka sijui kama atampa wizara..labda atampa wizara ya uvuvi na mifugo
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,012
  Trophy Points: 280
  Yawezekana Jk akamkwepa kama haya ya akina Lowassa kurudi serikalini ni ya kweli..................
   
 4. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rutashumbanyuma, Nina wasiwasi kama tumechoka kufikiri. Nenda kasome posti ya Mwanakijiji uone namna Rakesh Rajani alivyojadiliwa. Kwa ufupi hata akishuka malaika leo hataweza kuleta mabadiliko katika mfumo wa uongozi ndani ya CCM. Uongozi ni mbaya na siasa ni mbaya. Hivi vitu viwili vyote ni hovyo kwa sababu wananchi hawajatumia uwezo wao wa kuwachagua viongozi bora na kuwaondoa wabaya. Kwa hivyo siasa nayo inakuwa mbovu katika mfumo mbaya wa uongozi wa CCM. Hakuna kiongozi mzuri atakayefanya kazi yoyote ya maana katika mazingira ya mfuno mbovu wa uongozi na siasa mbaya. Ni kupoteza muda kufikiria eti mteule wa JK ataleta mabadiliko. Mpaka pale wananchi watakapoweza kutumia nguvu na uwezo wao waliokuwa nao wa kuwachagua vingozi bora na kuwaondoa viongozi wabaya ndipo mabadiliko yatapatikana. Ndiyo maana watu wanalia kwa nini Dr. Slaa amewaacha watu kwenye mataa?. Wananchi wanataka kuimarisha na kuendendeleza nguvu yao ya kuliongoza taifa hili siyo kuongozwa na watawala. Kwa maana nyingine hadi pale Tanzania itakapoongozwa na Wananchi wenyewe ndipo mabadiliko yatapatikana. Hivi hatuwezi kufikiri nje ya mfumo wa kuchaguliwa viongozi na watawala? Ninapenda nifanye majadiliano na wewe kidogo kuhusu hili. Mchango wa Campanero au Kiranga na Dr Slaa kuhusu hii posti ninaukaribisha sana.
   
 5. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kipya hapa ni kuwa na spika mwanamke,ila swala la mawaziri wanawake tumekuwa tukiwaona sana na uwezo wao pia tumeuona na kuutathmini.Labda kama unataka wateuliwe unawataka wewe ndio utaona sera ya usawa imefanya kazi.
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,012
  Trophy Points: 280
  Mtazamo wangu na wa kwako bado ni uleiule......fikiria mwenzetu alonga yafuatayo kwenye uzi huu huu:-

  Mwenzetu aona Uspika kuwa mwanamke ni kipya na mawaziri wamekuwa wakiwaona na wameweza kutathmini uwezo wao..........anachoshindwa kuelewa ni kuwa suala siyo jinsia pekee swala je hawa viongozi wanayo ridhaa ya wapigakura? Kama hawana ni dhuluma na dhuluma huzaa dhuluma nyingine ya kuteua viongozi wabovu ili kujilinda na maendeleo ya nchi yanazidi kudumaa......................
   
Loading...