CCM yachekelea

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802

Tangu jana hapa Ofisi Ndogo za CCM,Lumumba kuna furaha. Furaha ya kichama inahusu sarakasi zilizoanzishwa nasi juu ya Rasimu ya Katiba na wengine kuziiga. Makada waandamizi wa chama hapa Lumumba wanaziona sarakasi hizo kama zenye uwezo wa kuchelewesha uandikwaji wa Katiba mpya na hivyo kuifanya iliyopo kuendelea kufanya kazi.



Wanatamani mabishano yapambe moto na kuendelea na chama chetu kizidi kushika hatamu.'Rasimu ya Muungano tu hivi,je ikianza ya Tanganyika?' aliuliza Afisa mmoja wa Idara ya Uenezi.



‘Mwaka 2015 uchaguzi utafanyika kwa Katiba ya sasa. Mambo yatakuwa vilevile kama zamani.Cha kufanya ni kuendelea kupinga sehemu kubwa ya Rasimu hii.' aliongeza Afisa huyo anayejiita 'Tsunami'. Je,wanaamini katika kweli?



Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

 
kumbe mnajua kwa katiba yenye kujali misingi ya haki na sheria hamna ubavu wa kushinda? hata hivyo Warioba amesema ya tanganyika itakuwa faster kuliko mnavyofikiri kwa sababu maoni yote walisha kusanya wakati wa mchakato wa katiba ya mungano
 
unahali mbaya mkuu, naona umekosa thread sikuhizi, uwe hata unatupa dondoo za mashindano ya langalanga
 
Tume ya warioba imetuhakikishia kuwa 2015 tunatumia sahani mpya kwa mpunga mpya.Lazima ccm tuwanyonye macho na tongotongo zenu hatutajali
 
Back
Top Bottom