CCM yabwagwa Lindi na UKAWA, ndani ya Mitaa saba yaambulia patupu

Kwa hiyo ziara ya AIGIPII na zawadi ya ubunge hazikufua dafu. Safi sana watani zangu. Na hivi wameondoa hongo ya Tshirt na Khanga huku vijijini hao walie tu. Maana tafsiri iliyoko huku vijijini ni kuwa AIGIPII ana mkono wa birika ndio maana kapunguza vyeo vyao.
 
March 12, 2017

Wananchi wa Lindi kweli ni mfano wa kuigwa, maana ni juzijuzi ujumbe mzito toka Dsm ulikuwepo mjini Lindi na Mkoani Lindi kuahidi utekelezaji wa miradi mingi kwa manufaa ya wakaazi lakini inaonekana wananchi hawana imani na mikakati wala ahadi za viongozi wa CCM. Pongezi kwa wananchi kutambua miradi yote mikubwa ya serikali kuu inatokana na kodi zao na wana haki ya kidemokrasia kuchagua chama na viongozi wanaowaamini.

Tujikumbushe ziara hiyo nzito ya Mwenyekiti Taifa CCM :
Published on 3 Mar 2017
Rais Dkt John Magufuli amewaahidi wakazi wa Lindi kuwapatia kivuko kitakachowaunganisha wananchi wa Lindi mjini na eneo la Kitunda . Pia katika ziara yake Mkoani Lindi, Rais John Pombe Magufuli ameagiza kushikiliwa kwa hati za kusafiria za mwakilishi wa kampuni ya ukandarasi ya Overseas Infranstructure Alliance Private Limited ya India Bw. Rajendra Kumar pamoja na wasaidizi wake mpaka hapo kampuni hiyo itakapokamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Ng'apa Mjini Lindi ambao ulipaswa kuwa umekamilika tangu tarehe 17 Machi, 2015.


Source: DailyNews Habarileo
 
Je Mzee Lipumba nae hakusimamisha wagombea wake wa Buguruni?

Yaani Mzee Lipumba kazi yake kumendea ruuzuku za CUF tu ila wanaofanya kazi na kuleta ushindi ni watu wengine.
 
Nilitegemea kuiona CCM Mpya ikiibuka Na ushindi mkubwa huko mkoani Lindi katika Uchaguzi Mdogo wa Wenyeviti wa Mitaa lakini wananchi Na RAIA wa Lindi kupitia chama chao CUF wameigalagaza CCM Mpya Kwa kupata viti vyote 7 Na CCM Mpya haikupata hata kiti kimoja
 
Lipumba mwizi wa pesa za Ruzuku za CCM wengi kule CCM wanamchukia sana wamechoka kwenda kuchukua mapesa ya CCM kwa kisingizio kuwa anazitumia kudhoofisha ukawa na kuua CUF, sasa wana-CCM watashituka kuwa Lipumba ni mwizi wa pesa za CCM kwani hawaoni chochote zaidi ya kula mamilioni yao.
Yule jamaa sijui hata kama ana watoto uenda wangemshauri
 
Nashauri hao viongozi was ccm katika hiyo mitaa wafukuzwe uanachama,maana wameshindwa kukisaidia chama,
 
Nilitegemea kuiona CCM Mpya ikiibuka Na ushindi mkubwa huko mkoani Lindi katika Uchaguzi Mdogo wa Wenyeviti wa Mitaa lakini wananchi Na RAIA wa Lindi kupitia chama chao CUF wameigalagaza CCM Mpya Kwa kupata viti vyote 7 Na CCM Mpya haikupata hata kiti kimoja
CC: tetty
 
ila kusini na kaskazini mbona wanauelewa sana upinzani, walau sasa hivi kidogo mashariki magharibi kunanini maana ccm mwanzo mwisho
 
Back
Top Bottom