CCM yabembeleza watu kuwa mabalozi wa nyumba kumikumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yabembeleza watu kuwa mabalozi wa nyumba kumikumi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Apr 7, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  MWENENDO wa uchaguzi wa viongozi ngazi za shina unaoendelea ndani ya CCM wilayani hapa (Bunda), unadaiwa kuingia dosari baada ya baadhi ya wanachama wa chama hicho kususia kugombea kwa madai kuwa, chama hicho hivi sasa hakina mvuto kwa umma.

  Kufuatia hali hiyo, taarifa zinasema uongozi wa CCM ngazi za kata na wilaya, umekuwa ukihaha kubembeleza kisha kuwasimika wanachama wake wakongwe, ili kunusuru aibu ya kukoswa uwakilishi ngazi ya shina.

  Chanzo cha habari kilieleza kuwa, baadhi ya wanachama wanaojiita wenye msimamo mkali, hawaoni sababu ya kukitumikia kwa wadhifa wowote ule kwani, kimekosa mvuto kwa jamii wanaona bora kubaki wanachama wa kawaida.

  "Chama chetu kwa sasa hakina mvuto wala mshiko kwa jamii. Sasa hilo wengi hasa wenye msimamo mkali hawataki kabisa kuongoza, badala yake wanaona heri wabakie walalahoi ndani ya chama," kilieleza chanzo hicho.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho ambacho ni miongoni mwa watu waliosimikwa kwa nguvu kuwa mabalozi, baadhi ya sababu zinazowakera wanachama hao ni ukimya kilionao kuhusu tuhuma mbalimbali zinazotolewa dhidi ya mafisadi.

  Chanzo hicho kilisema hali ya chama kukaa kimya bila kuwachukulia hatua wanaotuhumiwa kwa ufisadi, vinawatia kinyaa baadhi ya wanachama.

  Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Bunda, Daudi Iramba, licha ya kudai kutojua kwa undani kuhusu mwenendo wa uchaguzi, alikana kuwapo kwa wanachama wanaogoma kugombea nafasi za ubalozi.

  "Sina taarifa rasmi maana sihusiki na uchaguzi, mhusika ni katibu maana ndiye mkurugenzi wa uchaguzi. Lakini kwa ujumla hatuna taarifa za watu kususia nafasi hizo," alisema Iramba na kuongeza:

  "Hili la chama, bado kiko imara kikiwa na mvuto tele kwa jamii kinaowatumikia kwa uadilifu mkubwa."

  Mwananchi.
   
 2. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Huko si ndiko anakotoka Wassira? Kumbe anapiga debe kwenye chaguzi ndogo wakati kwake hakujakaa sawa. Kazi kweli kweli.
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Tunaelekea kwenye saa ya ukombozi kamili kama wananchi wameeanza kujitambua vizuri namna hiyo Mungu wa Yakobo tuongoze kwenye njia hii tuenende salama
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  marketman(sokomtu)
   
 5. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,947
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  huku mwanza mabalozi wana kadi mbili, chadema na magamba. Ya magamba ni ya ubwabwa
   
 6. Lawrence Luanda

  Lawrence Luanda JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  duuu kaaazi kweli kweli magamba......
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  hakuna mtu anayetaka uongozi kwa kupitia ccm kwa sasa,vinginevyo uwe fisadi usiyekua na aibu hata kidogo
   
 8. IFUNYA

  IFUNYA JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 346
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Wananchi wamechoka na ccm, ccm waanze kusoma alama za nyakati. Yaliyotokea libya yatawafikia siku si nyingi. Leo, mheshimiwa nyerere amefanya mkutano ambao haujawahi kuonekana mjini musoma watu wametoka kila kona ya manisipaa uwanja wa mukendo umefurika sana. Hii inaonyesha hali inavyoiendea vibaya ccm. Chadema kaeni mkao wa kuchukua nchi wananchi wa tanzania wanawahitaji mkawakomboe kutoka mikononi mwa mafisadi (magamba)
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,269
  Likes Received: 22,029
  Trophy Points: 280
  CCM imeshaingia chumba cha mahututi
   
 10. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kimsingi hali ya hawa jamaa ni mbaya wiki tatu hapa Mby kulikuwa uchaguzi wa wajumbe wa serikali za mitaa kuziba mapengo kwa baadhi ya mitaa kimsingi jamaa waliangushwa mno hadi nyumbani kwa meya ambaye ni diwani wao. CDM walichukua kiti na wajumbe wengi

  Wamechelewa sana kukirudisha chama mioyoni mwa watu kwa sasa sijui wafanyeje
   
 11. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Saa ya UKOMBOZI NI SASA, NA WAKATI ULIOKUBALIKA NI HUU. CDM tutumie muda huu kuwaamsha watanzania ili tuwe fiti wakati wowote kumuondoa adui (JK na Magamba wenzake) magogoni.....tukilegeza hapa magamba wakapata nguvu...tumekwisha...but I believe in YOUTH...HAKUNA KULALA MAPAMBANO YANAENDELEA....
   
 12. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bado naitafakari kauli ya mh Vince Nyerere "Ukiona basi limeharibika na kuna abiria bado amekaa ndani yake basi ujue abiria huyo ana mizigo mizito ndani ya hilo basi"
   
Loading...