BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,098
CCM yabariki ufisadi
Mwandishi Wetu Juni 18, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo
Yawasafisha Mkapa, Lowassa, Karamagi
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), wiki iliyopita, kilipoza tuhuma zote kubwa za ufisadi zilizowagusa wanachama wake katika hatua inayotafsiriwa kuwa ni kujitoa katika vita dhidi ya uoza huo, Raia Mwema imeambiwa.
Hatua hiyo, sawa na methali maarufu: Funika kombe mwanaharamu apite, ilifikiwa katika kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) na wabunge wote wa chama hicho mjini Dodoma, na imeelezwa kuwa inalenga kukifanya chama kijisafishe kutokana na tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazokikabili mbele ya umma kabla ya mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2010 kuanza.
Baada ya mikakati, mbinu na hila zilizoendelea chini kwa chini kwa zaidi ya miezi kadhaa sasa, wajumbe wa NEC, mjini Dodoma, walijikuta wakizidiwa nguvu na kundi lililokua likiwatetea wenzao waliotuhumiwa katika kashfa mbalimbali zikiwemo zile za mradi tata wa umeme wa dharura wa Richmond na sakata ya wizi wa fedha za EPA ndani ya Benki Kuu.
Miongoni mwa waliotajwa moja kwa moja kwa kusakamwa na kutetewa ni pamoja na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye anasakamwa kwa kufanya biashara na kujitwalia mradi wa mkaa wa mawe wa Kiwira akiwa Ikulu na aliyekua Waziri Mkuu, Edward Lowassa, aliyejiuzulu kwa kuhusishwa na sakata la Richmond.
Pamoja na kutokuwapo kwa azimio ama uamuzi wa pamoja kuhusiana na masuala hayo, Raia Mwema imeambiwa kwamba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, hakuchukua upande wowote kati ya wanaoshambulia na wanaotetea na ananukuliwa akiwaambia wajumbe wa NEC kwamba asingezuia wabunge wa CCM kuikosoa Serikali kwa hoja na ushahidi wakati wote.
Baadhi ya wajumbe katika kikao hicho wanasema pia kwamba Kikwete aliwaambia wajumbe wajiepushe kunyoosheana vidole, na badala yake wazingatie mshikamano na kujadili masuala muhimu ya nchi kwa hoja bila kuathiri mshikamano ndani ya chama hicho kinachoonekana kwenda mrama kwa sasa.
Katika hali inayoashiria kuwapo mshikamano mkubwa miongoni mwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi, mjumbe mmoja wa NEC, ambaye naye ametajwa katika tuhuma mbalimbali za kifisadi, alisimama na kumtetea Mkapa akisema kwamba ni kiongozi anayepaswa kuenziwa kutokana na kazi nzuri aliyoifanya wakati wa utawala wake.
Habari za ndani ya kikao hicho zinaeleza kwamba mjumbe huyo, ambaye ni mbunge na mfanyabiashara, maarufu alikiambia kikao hicho kwamba Mkapa aliacha Taifa likiwa na utajiri mwingi ikiwa ni pamoja na akiba ya kutosha BoT, na kwamba wanaomshambulia ni wajinga na wasiokuwa na elimu ya kutosha kuhusu taifa hili..
Hata hivyo, baada ya kumaliza kumsifia Mkapa mjumbe huyo alipigiwa makofi na wajumbe wachache mno akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba ambaye naye mambo yake si mazuri sana kutokana na kubanwa na baadhi ya wajumbe wanaotaka aondolewe katika nafasi yake kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na afya na tuhuma za kushindwa kazi.
Habari zaidi zinaeleza kwamba, baadhi ya wabunge wa CCM wameelezwa kuwa na mkakati maalumu wa kutaka Makamba aondolewe katika nafasi yake ya ukatibu mkuu wa CCM lakini wamekuwa wakipingwa vikali na wenzao akiwamo Katibu wa Wabunge wa CCM, Ali Ameir Mohamed.
Imeelezwa kwamba mbali ya kutaka CCM iwachukulie hatua watuhumiwa wa ufisadi ili ijitenge na tuhuma hizo, walitaka pia Makamba aondolewe katika wadhifa huo kwa kushindwa kuhimili hali ya sasa ya kisiasa nchini na kutajwa kuwalinda watuhumiwa wa ufisadi lakini pia kutokana na kuwa na matatizo ya kiafya.
Pamoja na Kikwete kuhimiza mshikamano miongoni mwa wana CCM, matukio ya mwishoni mwa wiki yamezidisha mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM badala ya kuupunguza baada ya kujitokeza kwa wajumbe waliotetea moja kwa moja watuhumiwa wa ufisadi.
Hali hiyo imekuja huku kukiwa na wingu la tuhuma za rushwa, ushirikina, vitisho na hata ulaghai uliogubika mikakati ya kuhakikisha watuhumiwa wote wa ufisadi wanasafishwa huku upande mwingine wa wajumbe ukisisitiza kuchukuliwa kwa hatua dhidi yao.
Muda wote huo Mwenyekiti wa CCM (Kikwete), alikuwa akimuangalia mjumbe huyo aliyemsifu Mkapa, na kisha (Kikwete) kutoa maoni yaliyowachanganya kidogo wajumbe wengine kutokana na kumsifia mjumbe huyo kuwa ni mwenye busara na akili zaidi ya wajumbe wengine wote waliohudhuria kikao hicho, anasema mjumbe mmoja wa NEC kutoka mkoa wa Dar es Salaam. Kauli ya Kikwete ya kumsifu mjumbe huyo, hata hivyo, ililenga kumkejeli kwa yale aliyoyasema.
Katika utetezi wao, wajumbe waliochangia kuhusu sakata la Richmond walisema wazi kwamba Lowassa hakuhusika moja kwa moja na sakata hilo na kwamba alijiuzulu kulinda hadhi ya chama, hoja ambayo ilipingwa na wajumbe wengine waliohoji kama CCM sasa haihitaji tena hiyo hadhi.
Kama alijiuzulu kulinda hadhi ama heshima ya chama katika uso wa jamii, ina maana kwa sasa CCM haihitaji tena hiyo heshima? Ina maana sasa anataka CCM ianguke au anamtakia mabaya Kikwete mwaka 2010 atakapowania tena kipindi cha pili cha urais wake? alihoji mjumbe mmoja ambaye ni Mbunge aliyezungumza na Raia Mwema kwa simu juzi.
Kuhusu suala la wizi wa BoT na wahusika wa sakata la Fedha za Madeni ya Nje (EPA) pamoja na uchunguzi wa kesi ya rada unaomgusa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, wajumbe wa NEC wameelezwa kwamba masuala hayo yako mikononi mwa vyombo vya dola na hivyo chama hakiwezi kuyajadili kwa sasa.
Wakati tuhuma dhidi ya kuwapo mbunge mmoja wa CCM aliyedaiwa kufanya ushirikina ndani ya Bunge zikiwa zinafukuta, aliyekua Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ametajwa kuzidiwa ghafla ndani ya Bunge na kukimbizwa hospitali na hadi sasa hajarejea bungeni.
Chama cha Mapinduzi kimekuwa katika wakati mgumu tangu kuibuka kwa sakata la mgodi wa dhahabu wa Buzwagi lililoibuliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, na baadaye kuibuka kwa mfululizo wa kashfa zikiwamo za Richmond, EPA na rada, na hatua zilizochukuliwa na Bunge na Serikali kuhusiana na mambo hayo hazikukisaidia chama hicho kuonekana makini kwa wananchi.
Baada ya kuibuka kwa sakata la Buzwagi lililomhusisha aliyekua Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, Serikali ilisambaza mawaziri wake mikoani kwa kile walichodai kuelezea Bajeti ya Serikali lakini walipata wakati mgumu kutokana na kuzomewa na wananchi maeneo mengi.
Baada ya kuonekana tunafanya vizuri kupitia Bunge na Serikali, sasa tunataka kuharibu kwa kuwatetea, ni bora tungenyamaza kimya badala ya kuwatetea. Kwa kweli tunaendelea kujimaliza kwa wananchi maana wananchi wa sasa wamechangamka kweli kweli, anasema kiongozi mmoja wa CCM, ambaye ni mjumbe wa NEC.
Kufanyika kwa kikao hicho cha pamoja cha NEC na wabunge wa CCM, imeelezwa kulitokana na ombi la wabunge kwa Mwenyekiti Kikwete ili kujadili ajenda mbili.
Raia Mwema imeambiwa kwamba ajenda hizo ni ya hali ya baadaye ya nafasi ya Katibu Mkuu Makamba, ambaye wao wanamwona kuwa ni mtendaji aliyekwisha kuchoka.
Ajenda ya pili kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari ilikuwa ni ya kuachana na wote ambao wametuhumiwa, kwa nyakati na aina mbalimbali za tuhuma, waondoke kwenye chama.
Lakini habari zinasema ajenda hizo hazikufikishwa mkutanoni huku Ofisi ya Katibu Mkuu Makamba ikituhumiwa kuzihujumu.