Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
[h=2]Na Victor Bariety, Geita - Mtanzania[/h]
*Mwenyekiti wao asema hatapeleka maendeleo kata za CHADEMA
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Geita, Joseph Musukuma, jana aliwaacha hoi wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Nyawilimilwa, kilichopo Kata ya Kagu, baada ya kusema hatakuwa tayari kupeleka miradi ya maendeleo katika kata hiyo, kwa kuwa inaongozwa na diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Musukuma alitoa kauli hiyo mbele ya Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Moses Minga pamoja na Ofisa Mipango wa Wilaya hiyo, Frank Makonda, waliokuwa wamehudhuria kikao hicho kilichofanyika wakati akikagua miradi ya maendeleo ya kata hiyo.
Nilitumia gharama kubwa sana wakati wa uchaguzi uliopita wa udiwani, lakini wananchi wa kata hii mkanisaliti na kumchagua Lukondo Mkukura wa CHADEMA.
Mlifanya hivyo kwa sababu zenu wenyewe na hii ilitokana na ninyi wenyewe kuendekeza makundi na ukabila. Kwa hiyo, naomba mkome kabisa na hayo ndiyo matunda ya kuchagua upinzani.
Kutokana na tabia mliyoifanya, niko tayari kumzuia mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya, asiwaletee fedha za ruzuku zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya shughuli za maendeleo, ili liwe fundisho kwa watu wengine wanaoacha kuchagua CCM na kuchagua vyama vya siasa vya upinzani hususan CHADEMA.
CHADEMA hawana uwezo wa kuwaletea maendeleo katika kata hii na ni vigumu pia na mimi kuwaletea maendeleo ama kuruhusu miradi ya maendeleo ije kwenu.
Huenda nifanye hivyo kwa huruma tu ya chama changu, kwa sababu nyinyi wenyewe mlichagua shetani, acheni mkome, alisema Musukuma.
Soma zaidi hapa
Je hizi ni sera za chama au ni mtu binafsi mwenye uelewa finyu?