CCM yaanza Usajili kwa chaguzi 2009 & 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yaanza Usajili kwa chaguzi 2009 & 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rev. Kishoka, Mar 3, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Habari zinanukia na kusema kuwa ili kujisafisha na kuondoa sura ya madoa ya EPA, RADA, Kiwira na dalili zozote za kuitwa Chama Cha Mafisadi, CCM imeanza kampeni za usajili wa wagombea Udiwani na Uchaguzi 2009 & 2010!

  Habari za upenuni zinasema dhumuni la Usajili huu ni kwanza kuwang'oa wabunge Machachari wa CCM ambao wamekuwa wakiukoroema ufisadi, na pili kwa kuwa baadhi ya Watuhumiwa wa Ufisadi wanaweza kuombwa waachiee ngazi, basi kunahitajika Wabunge wasio na madoa ambao wakiingia Bungeni, kazi yao itakuwa ni kukilinda CCM na hao Fisi wenye madoa madoa ambao wanatuhumiwa kuwa mafisadi!


  Usajili huu unafanywa kwenye taasisi za elimu ya juu na CCM imedhamiria kusakanya wasomi, iwe Mzumbe, SUA, UDSM, au kwingineko kunakoitwa chuo. Dhamira ni kuleta vijana ambao wataonekana ni safi na wapya ili kuondoa ukungu unaotanda ambao unadhihirisha kuwa CCM inaweza kuanguka.

  Kikubwa na cha kutisha ni danganya toto ya kutaka kuleta ufalme wa milele wa CCM na kulidna maslahi ya Mafisadi. Ikiwa CCM itashinda kwa kishindo kwa hizi sura mpya ambazo hazijapata madoa, itakuwa ni rahisi kwa CCM kuliongoza bunge kwa upinzani mdogo sana kutoka kwa Vyama vya Upinzani au wengine wote wanaopigia kelele udhaimu na mabavu ya CCM.

  Habari za kuaminika ni kuwa wale ambao wamekuwa watii wa vikao vya usajili na viongozi hawa wa CCM, wameahidiwa "Ufalme Mpya" na "usafi" wao utakingiwa kifua.

  Bado tuko mitamboni tukitafuta habari zaidi!
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wacha wasakane lakini Sultani CCM lazima aondolewe yeye na vikaragosi vyake ,wakitaka wasitake KATIBA ya Nchi lazima ibadilishwe ,tume ya uchaguzi lazima ibadilishwe.

  Zaidi ni kuwa Wananchi wameshachoka na Usultani wa CCM ,wanatafuta Chama mbadala ambacho kitaweza kuendeshwa kwa misingi ya Katiba mpya itakayopatikana na vilevile itakayopunguza nguvu za Raisi na kama haitoshi itakayosisitiza tume huru ya Uchaguzi ukiongezea wakuu wa mahakama wasiwe wakereketwa wa vyama vya siasa kwa maana mahakama,vyombo vya usalama ,tume za Uchaguzi viwekwe kando kabisa na kuachwa kuongozwa na Ukoo wa Sultani CCM.
   
 3. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nashukuru sana Mkuu Rev. Kishoka kwa taarifa yako hapo juu. Nakupongeza kwa kuwa wa kwanza mara nyingi ku-share na jamvi hili taarifa mbalimbali unazokuwa ukizipata ili kuelimishana, kuhabarishana na kuchangia katika mambo muhimu yanayolikumba Taifa letu.

  Pamoja na kuwa maamuzi hayo ya CCM kuanza kuandikisha wagombea Udiwani na Uchaguzi 2009 & 2010, CCM inatakiwa iwe makini sana kwa kuwa hatua hiyo inaweza kuigharimu zaidi ya kuipa faida katika uchaguzi ujao.

  CCM inaweza kupata shida kuwanadi wagombea hao wanaoonekana kuwa wasafi kutokana na

  1. kutowajua vyema usafi wao, kukubalika kwao na uwezo wao kisiasa
  2. watakaokuwa wamewekwa kando mapema kiasi hicho watakuwa na nafasi ya kuingia upinzani na kusababisha madhara makubwa kwa CCM kwenye uchaguzi mkuu (kwa maana wapinzani hawatakuwa wamependekeza majina ya wagombea)
  3. Wanaweza kuchafuliwa mapema zaidi, na hivyo kushindwa kuhimili vishindo vya uchaguzi
  4. Hoja ya CCM kujisafisha na tuhuma za ufisadi hazitakamilika kwa kubadili sura za watu. Badala yake chama kitasafishika kwa kubadili msimamo wake kuhusiana na ukingiaji kifua ufisadi, na kuchukua hatua kali kwa mafisadi
  5. CCM haishindi kwasababu imetumia watu wa vyuo vikuu peke yake. Hushinda kwasababu hutumia watu wenye uwezo wa kushawishi, wenye kujua mbinu za kampeni na wanaokubalika na watu. Hatua yao ya kuchagua mapema na kutoka ndani ya vyuo vikuu, itawanyima wengine haki ya kuchaguliwa na chama chao na hivyo kuwepo na uwezekano wa kura za maruhani (kura za kisasi)

  CCM ikitaka kijihakikishia ushindi wa kishindo, ni vyema ikaanza kujenga matumaini kwa wapiga kura sasa hivi. Haiwezi kupata kura kwa kujidanganya kuwa ikibadili wagombea, wananchi watawakubali. Mara nyingi hii sio rahisi kiasi hicho.
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wananchi,

  Tusisahau kuwa hii ni Tanzania, wananchi wake walipagawa kuona sura ya Kisura na kumpa kura za Tsunami!

  Ni mpaka pale Mtanzania atakapopata uhuru wa kufikiri kwa kutumia hiari yake kuwa huru na kutumia uhuru wa kufikiri, ndipo tutapiga hatua!
   
Loading...