CCM Yaanza Rafu Zake Pemba: Watu 500 Wakataliwa kuandikishwa Micheweni. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Yaanza Rafu Zake Pemba: Watu 500 Wakataliwa kuandikishwa Micheweni.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Jul 9, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Uandikishaji Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Wilaya ya Micheweni: Taarifa ya Awali – Siku ya Pili 8 Julai, 2009
  “Watu 584 wanyimwa haki ya kuwa wapiga kura katika siku ya pili”
  Zoezi la uandikishaji wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Zanzibar lililoanza juzi katika wilaya ya Micheweni unaendelea katika hali ya mashaka. Ushirikiano ambao sisi katika Chama cha Wananchi (CUF) tunauita ‘utatu usio mtakatifu’ (trinity of the demons) kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia masheha wake, Idara ya Vitambulisho na Tume ya Uchaguzi (ZEC) unaendeleza azma yake ya kuwanyima Wazanzibari haki yao ya kuwa wapiga kura.
  Katika rikodi zilizokusanywa juzi, wapiga kura 830 walinyimwa haki hiyo katika vituo sita vya jimbo la Konde huku wakiandikishwa 133 tu katika vituo vyote hivyo. Rikodi za jana zinaonesha kwamba watu 584 wamenyimwa haki hiyo na walioandikishwa ni 224 tu. Kwa hivyo, kwa juzi na jana tu, watu walionyimwa haki ya kuwa wapiga kura katika jimbo la Konde peke yake ni 1,414. Siku hizi mbili zilikuwa ni za uandikishaji wapiga kura wapya. Sababu inayotumika kwa ZEC kuwanyima watu hao haki ya kuwa wapiga kura ni kutokuwa kwao na vitambulisho vya Uzanzibari, sharti ambalo limewekwa na ZEC kwa kusudi maalum la kuvuruga uchaguzi.
  Sharti hili liko kinyume na Katiba ya Zanzibar na misingi ya demokrasia ambayo nchi hii inajaribu kuijenga. Wengi wa watu walionyimwa haki hiyo wanazo shahada nyingine zinazothibitisha uzawa na ukweli kwamba wameshafikia umri wa kuwa wapiga kura.
  Tunatuma taarifa hii ikiwa ni indhari ya namna hali inavyoendelea na makisio ya hali inakoelekea. Tutakuwa tukituma taarifa kila siku hadi kumalizika kwa zoezi.

  Imesambazwa na:
  Kurugenzi ya Uenezi na Mahusiano na Umma
  CUF
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  JK upoooo?! mfupa uliomshinda fisi huo waja.
   
 3. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sheria Baba Kama tumekubaliana katika sheria za uchaguzi utambulishi ni Mzanzibari Mkaazi , Tume lazima itekeleze hivyo Huko ndio kusema Tume Huru siyo matakwa yenu ya CUF.
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Sheria haina tatizo hila ndiyo zenye matatizo, wananchi wanafuata sheria, wanakwenda kuomba vitambulisho kwa mujibu wa sheria hiyo unayosema ifuatwe, wanakataliwa makusudi na masheha wanapoendewa kutoa barua za uthibitisho wanatazama watu usoni, wana wanyima makusudi ili baadae wasipate fursa ya kuandikishwa. Kibaya zaidi jambo hilo limeshalalamikiwa kabla zoezi la kuandikisha halijaanza lakini "utatu usio mtakatifu" umenyamaa kwa makusudi kwa kuwa wanajuwa wanachokifanya.
  Shauri yao mara hii maandamano yataanzia Victoria Garden kuelekea Ikulu.
   
 5. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Waje Tanzania bara wajiandikishe watapiga kura without problem...
   
 6. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  siku aliyoipanga MMungu haijafika na ikifika hakuna wa kuizuwika kama vile royo ya mwanadamu inapotolewa huwa haizidi siku dakika wala sekunde ,leo tulidhani kuwa tutayajuwa maovu ya baadhi ya viongozi wa nchi hii na serekali katika kujilimbikizia mali za nchi .
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Yaa Allah wanausuru ndugu zangu wa hapo Konde na madhila makubwa ya kudhulumiwa haki zao.

  Yaa Zanzibar Kikwete hayawezi.
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hao watakuwa wamehusu TA
   
 9. C

  Calipso JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mungu awaangushie gharka wote wanaofanya hila za kuwahujumu haki yao ya kikatiba wazanzibar,awape kuwapa,awatetemeshe viwili wili vyao,awaoneshe la kuwaonesha.. AMIN.

  Safari hii,tunaangalia nyumba moja moja ya mtu aliehusika na kuwadhulumu wazanzibar la sivyo wahame nchi mapema... tumechoka na manyanyaso ya ccm.
   
 10. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Shauri lenu. OCD wa Wilaya Mjini yupo. Anatosha -ilimradi tu apate mgao kidogo, kati ya wale vijana wa FFU 7,000 ambao Wizara ya mambo ya ndani imeamua kuwaajiri na kuwapa mafunzo kumarisha nguvu ya Jeshi letu la Polisi.
   
Loading...