Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
CCM yaanza kumeguka
Katibu UWT Maswa atimuliwa
SIKU tano baada ya kumalizika uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani, huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikinyakua majimbo mawili ya ubunge ya Maswa Mashariki na Maswa Magharibi, Mkoa wa Simiyu, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani humo wameanza kutimuana kwa madai kuwa walikisaliti chama hicho.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya CCM na kuthibitishwa na mmoja wa viongozi wa juu wilayani humo, zinasema tayari Katibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Maswa, Nuru Mselemo ametimuliwa kwa madai ya kuiunga mkono CHADEMA.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutoandikwa gazetini (jina tunalo) kiongozi huyo, alisema tayari katibu huyo wa UWT amekabidhiwa barua ya kuondolewa katika nafasi hiyo na kuamriwa kuripoti kwa Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga ili aweze kupangiwa kazi nyingine.
Baada ya CHADEMA kuibuka na ushindi katika majimbo mawili ya Maswa Mashariki na Maswa Magharibi, Katibu wa UWT ametimuliwa kwa madai ya kukisaliti chama wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu huku akitoa siri kwa viongozi wa upinzani, kilisema chanzo hicho.
Taarifa zaidi zinadai kuwa, hata wakati wa kampeni alikataa kushiriki kukipigia debe chama hicho kwa kile kinachoelezwa kuwa kutokuwa na uhusiano mzuri na viongozi wa ngazi za juu wa CCM wilayani, akiwamo Mwenyekiti, Peter Bunyongoli, ambaye alikuwa anagombea ubunge katika Jimbo la Maswa Mashariki sambamba na Katibu Uenezi na Siasa, Jeremiah Shigala.
Akizungumza kwa simu na Tanzania Daima kuhusu madai dhidi yake, Nuru alikiri kupata barua hiyo ya uhamisho lakini kuhusu tuhuma hizo alisema hazina ukweli wowote bali ni chuki binafsi zinazofanywa na viongozi hao.
Madai hayo hayana msingi wowote, hizo ni chuki binafsi dhidi yangu zinazofanywa na viongozi hao kama ni suala la kampeni mimi nilipangiwa katika eneo la Maswa Magharibi, sasa mtu anaposema sikushiriki kampeni huyo ana chuki zake, suala si kulaumiana, ni kuona tumekosea wapi ili kujipanga katika kipindi kijacho na si kuanza kushikana uchawi kwa sasa, alisema Nuru.
Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Naomi Mayunga, akizungumza kwa njia ya simu, alisema hana taarifa zozote za kutimuliwa kwa katibu huyo.
Chanzo: T. Daima