CCM yaanza kujipanga kunyakua Ilemela, Nyamagana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yaanza kujipanga kunyakua Ilemela, Nyamagana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 22, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145

  22 NOVEMBER 2011

  Na Moses Matthew, Mwanza

  KAMATI ya Habari na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza, imekamilisha kazi ya kupata maoni mbalimbali kutoka kwa
  wananchi ngazi ya Kata kujua sababu zilizosababisha chama hicho kupoteza majimbo mawili ya Ilemela na Nyamagana katika uchaguzi Mkuu uliopita.

  Kamati hiyo iliyoanzishwa mwezi Mei na kuanza kazi rasmi mwezi wa saba mwaka jana, imebaini sababu kubwa nne zilizosababisha CCM kushindwa katika majimbo hayo mawili ikiwemo urasimu na ukandamizaji kwa baadhi ya watendaji, walimu kutopewa haki zao kwa wakati, uratatibu wa kura za maoni na migogoro ya ardhi.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Jijini hapa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Musa Magabe, alisema lengo kuu la kamati yao kufanya ziara kwenye kata zote za wilaya hiyo ilikuwa kujua kwa undani kero mbalimbali za wananchi wa kada zote wakiwemo wafanyakazi zilizosababisha CCM kunyimwa kura mwaka jana ili ziwasilishwe kwenye kamati ya Siasa ya wilaya na kufanyiwa maamuzi ya utatuzi kwa manufaa ya taifa.

  Alisema ili kufikia lengo waligawa kazi hiyo kwa makundi makubwa mawili. Kundi la kwanza ikiwa ni la wananchi na la pili ikijumlisha viongozi wote wa CCM waliokuwa wapigadebe na wasimamizi wakati wa uchaguzi uliopita ili waweze kubaini wapi walipokosea na kujirekebisha mapema.

  Akitaja matokeo ya kazi hiyo kwa upande wa wafanyakazi alisema, watumishi wa serikali ngazi za Kata Kamati iligundua udhaifu mkubwa kwa baadhi ya Maofisa wa ngazi ya juu kwenye Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuwanyanyasa walio chini yao hivyo kuwafanya waichukie CCM na serikali yake.

  Alitoa mfano kwa watumishi wa sekta ya elimu na kuweka wazi kuwa kamati yake imebaini walimu kukasirishwa na kucheleweshewa mafao yao, malipo yao ya likizo, kupandishwa madaraja na fedha za kujikimu kwa walimu wanaoanza kazi.

  Alisema walibaini wananchi wengi wakiwemo wafanyakazi kulalamikia ukiritimba kwa baadhi ya watendaji katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza hivyo kuwafanya waichukie CCM hatimaye kukiadhibu chama hicho kwa kukinyima kura katika uchaguzi mkuu uliopita hususan katika majimbo hayo mawili.

  Kwa mujibu wa katibu huyo kero zingine zilizobainishwa na kamati hiyo ni Maofisa watendaji wa kata kutopewa fedha za kuendesha Ofisi na ucheleweshaji wa fedha za maendeleo ikiwemo ukarabati katika sekta za afya, elimu na kero mbalimbali za kijamii.

  Kuhusu migogoro ya ardhi alisema kamati hiyo ilibaini wananchi kuchukizwa na kero hiyo kukithiri na kuwapa wakati mugumu katika kata zao na kwamba hawaoni dalili ya wazi kushughulikia tatizo hilo na kwamba waliwekwa wazi kuwa hicho ndicho chanzo cha CCM kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 Jiji la Mwanza.

  Akizungumzia viongozi wa CCM ngazi za kata alisema kilio chao kikubwa kilikuwa chama hicho kiliwasahau mabalozi wa nyumba 10 ambao ndiyo uti wa mgongo na uhai wa chama pamoja na mfumo wa utaratibu wa kura za maoni kutosimamiwa vizuri hivyo kuzaa makundi.

  Kuhusu suluhisho la matatizo hayo baada ya kazi hiyo Bw. Magabe alisema kuundwa kwa kamati hiyo na kubaini chanzo cha CCM kukosa ushindi wa ubunge na baadhi ya kata ni suluhisho la kwanza kwa kuwa maoni hayo yatawasilishwa sehemu husika na wananchi wataanza kuona mabadiliko.

  "Chama cha Mapinduzi hakipindui serikali, kinajipindua chenyewe ndiyo maana unasikia dhana ya kujivua gamba, wananchi watarajie mabadiliko makubwa maana tumeshajua chanzo cha tatizo", alisema Bw. Magabe.

  "Dhana ya kujivua gamba siyo geni, wakati wa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere, alitumia dhana hiyo kwa jina la tujisahihishe katika jitihada za kuweka mambo sawa," alisema.


   
 2. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Muf a maji haachi kutapatapa
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,090
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Wenje na CHADEMA makao makuu watafute copy ya matokeo ya hiyo research na kuyafanyia kazi. Simple!
   
 4. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu wala usiumize kichwa hakuna reserch yoyote iliyofanywa na magamba, uliona wapi hawa jamaa wakafanya reserch??
   
 5. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  asante mkuu nyoka_bndm.JPG
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Viti vyote Mwanza pamoja na ile Ilemela hapati mtu mpaka tujuzwe kwanza MKE WA KWANZA kifo chake kilitokeaje huko miaka ya nyuma kidogo; watu lazima kwanza wajisafishe tangu majumbani ndipo watoke nje kwenda kugombea viti huko.
   
 7. O

  Ok'neil Member

  #7
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :
  i like your idea
   
 8. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,441
  Likes Received: 1,739
  Trophy Points: 280
  binafsi niliongea na mbunge wa Ilemela kupitia CHADEMA nikampa tips za jinsi ya kuimarisha kuungwa mkono na wananchi wa Ilemela,mpaka leo miezi 4 hakuna lolote aliloshughulikia kati ya yale niliyomtajia. Nina uzoefu wa kutosha katika maeneo yale,miaka 6 ninatoa huduma za kijamii katika jimbo hili,nafahamu sehemu ambazo hata kwa efforts kidogo ukizishughulikia matokeo utayaona haraka, tatizo la wanasiasa wengi ni kutofanya vitu kisayansi.

  Hebu jiulize,wauguzi,madaktari, walimu n.k wenye migogoro na mkurugenzi wa jiji wakiamua kuvurunda makazini mwao impact yao itakuwaje kwa wapiga kura? Ccm walishindwa kwa mchezo huo pamoja na kero nyingine
   
 9. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,838
  Likes Received: 2,083
  Trophy Points: 280
  hawana jipya.
   
 10. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Poor watanzania.
   
 11. S

  Straight JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  labda research ya mbinu za uchakachuaji....
   
 12. JOASH MUSSA

  JOASH MUSSA JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 492
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ndio hawapati tena
   
 13. All TRUTH

  All TRUTH JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 2,664
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Duh ccm ndo msahau nani anawataka nyie wezi!
   
 14. M

  MwanaCCM Senior Member

  #14
  Jul 9, 2013
  Joined: Feb 5, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mke wa nani tena jamani? naomba utupe information
   
 15. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2013
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 23,998
  Likes Received: 1,565
  Trophy Points: 280
  Walimu JK si alisema hataki Kura zao?kumbe nayo ni sababu tena?
   
 16. Jalood

  Jalood JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2013
  Joined: Dec 13, 2012
  Messages: 751
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa tunalisubiri Jimbo la Mtwara
   
 17. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2013
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,761
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Mwandishi mwenyewe gamba la chui. Mosses Mathew ni Pinda mkubwa
   
 18. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #18
  Jul 9, 2013
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 2,732
  Likes Received: 1,232
  Trophy Points: 280
  Hata majimbo ya Iringa na Mbeya mjini yanarudi CCM
   
 19. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,013
  Likes Received: 1,483
  Trophy Points: 280
  Chadema kwishney
   
 20. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #20
  Jul 9, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,013
  Likes Received: 1,483
  Trophy Points: 280
  Ni jambo jema kwa ccm kujitafakari na hatimaye kuja na majibu ya kile kilichowavuruga
   
Loading...