Job K
JF-Expert Member
- Oct 4, 2010
- 9,315
- 7,113
Taarifa nilizozipata muda huu kutoka kwa mmoja wa viongozi wa CCM (W) - Meatu (Jina limehifadhiwa) ni kwamba mgombea ubunge kupitia CCM Ndugu Khamis Salum Mbuzi ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge kwa jimbo la Meatu ambalo limenyakuliwa na Mgombea kupitia CHADEMA Mh. Meshack Opulukwa.
Kwa maelezo ya kiongozi huyo Kata iliyowaangusha CCM ni Kata ya Mwamishali ambayo ndo ilikuwa ya mwisho kuwasilisha matokeo yake. Kwa jimbo la Kisesa ambalo ni jimbo dada na Meatu limenyakuliwa na mgombea wa CCM Mh. Joelson Luhaga Mpina ambaye alikuwa anatetea kiti chake na amefanikiwa.
Hongera CHADEMA kwa kazi nzuri!!!!!!!!