CCM yaahidi neema na utatuzi wa kero Ukonga

MASIGA

Senior Member
Aug 29, 2015
130
281
05 Septemba 2018

Katika mkutano wa hadhara Kata ya Ukonga Wilaya ya Ilala wa kumnadi Ndg. Mwita Mwikwabe Waitara mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Ukonga, Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitalivalia njuga suala la utatuzi wa kero za wananchi kwa umahiri zaidi katika Jimbo la Ukonga pindi wananchi watakapo mchagua Ndg. Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga.

Akifananua namna ambavyo CCM itasimamia, itaratibu na kufanikisha utatuzi wa kero za wananchi na kuleta maendeleo ya Jimbo la Ukonga mbele ya mamia ya wananchi waliojitokeza katika Mkutano huo Ndg. Polepole amesema CCM kupitia Serikali yake itafanikisha upatikanaji wa maji safi na salama, ujenzi wa shule ya Sekondari ya Ukonga, ukarabati na uimarishaji wa miundombinu ya barabara za mitaa na kukomesha kero za tozo kubwa zenye maudhi za ukusanyaji wa taka zinazowakumba wananchi wa Jimbo la Ukonga.

"Kampuni inayokusanya taka hapa Ukonga imeonyesha haina uwezo wa kukusanya taka wala haina dhamira njema nina muelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri afanye utaratibu kampuni hii itafute kazi nyingine… CCM imeelekeza kutengwa na kutolewa zaidi ya Bilioni 4 kwa ajili ya Mikopo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu na hii ni mikopo isiyo na riba… wiki moja toka leo watu wa DAWASCO wataanza kuchimba mitaro na kutandika mabomba ya kusambaza maji hapa ili mpate maji safi na salama... Tunaomba mtupatie Ndg. Mwita mtu tunayemuamini vizuri ili tushiriki naye kuwaletea maendeleo kwa haraka" amesisitiza Ndg. Polepole

Huu ni muendelezo wa Mikutano ya hadhara ya kuwanadi wagombea Ubunge na Udiwani katika maeneo ambayo yana uchaguzi mdogo wa marudio ambapo CCM imejipambanua kwa siasa safi, hoja na sera nzuri zinazogusa maslahi ya wananchi.

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
IMG-20180906-WA0089.jpg
 
Hahahaha "CCM yaahidi neema".

Na watu wanashangilia kama mazuzu wakiamini CCM itawaletea 'NEEMA'!!.
 
mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Miaka 50 bado wanaahidi tu,kibaya walichokiahidi miaka ya nyuma wanaahidi hadi leo.
 
Back
Top Bottom