CCM ya zamani iliongozwa na Wapinzani?

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Laweza kuwa swali la kitoto. JF ni jukwaa huru linalovumilia hata wenye maswali ya kitoto.
Hivi sasa mitandao ya kijamii hasa facebook imejaa vijana wa CCM wanaojitambulisha kuwa "CCM Blood". Hawa wana ruhusa ya kutukana, kukebehi, kuzusha, kudanganya, na kueneza fitna. Sina tatizo na hilo. tatizo ni pale vijana wenzao wasio wa CCM wakijaribu kufanya wanachofanya vijana wa CCM, wakamatwa na kufunguliwa kesi. Uonevu huu haukubaliki na unapunguza thamani ya Mwenyekiti wa CCM na chama chenyewe.

Kuna hili dai kuwa hii ya sasa ni CCM mpya. Upya wake unaonekana kwa kuilinganisha na CCM ya zamani. CCM ya zamani (Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete) inatuhumiwa na CCM mpya kwa rushwa, ufisadi, kukosa uzalendo, kuuza raslimali za nchi, wafanyakazi hewa, vyeti feki, uzembe serikalini, n.k.

Dai linaendelea kuwa wapinzani hawajajipanga kuweza kuongoza dola. Amehoji kijana Katambi kwamba wapinzani hawawezi kwa sababu hawana watu wa kuongoza nchi. Namkubali kwa sharti moja tu; atueleze CCM ya zamani ilikuwa ni Wapinzani na ndiyo tukaanzisha CCM mpya?

Nini kimebadilika? Nchi ni ile ile? Katiba ya CCM ni ile ile isipokuwa idadi ya wajumbe kwenye vikao? Ilani ile ile? Jibu ni kuwa amebadilika kiongozi mkuu wa chama. Je ni sahihi chama kukiita kipya kwa badiliko la sura ya mtu mmoja? Kwa hiyo akiondoka, hii tunayoiita CCM mpya itabadilika na kuwa CCM ipi? Ya zamani au zamani kidogo?

Kama wanataka kujijua, waruhusu uhuru wa maoni waje waone jinsi watanzania wanavyoelewa mambo. Hata maoni huru ndani ya CCM hakuna. Kuna vijana makini wasiohitaji hoja nyepesi ndani ya CCM lakini hivi sasa hawana jukwaa la kujenga hoja. Usinambie watu kama Bashe, Mwigulu, January, Nape, Nchimbi, Serukamba, Kamala, Kitila, Chegeni, n.k wana nafasi tena katika CCM mpya isiyopenda kukosolewa. Hakuna ukomavu wa chama bila kuruhusu maoni huru na tofauti. Kina Lukuvi, Shirima, Lowasa, Kikwete, Henjewele, Masaburi, Gupta, na wengineo walio hai na marehemu, walikuwa wanamtoa jasho Mwalimu kwa hoja nzito ndani ya chama na alipokuwa anatembelea mlimani kusikiliza fikra mpya. Tusikubali ukomavu wa chama utokane na ulinzi wa virungu vya polisi, mabomu na mbwa wa polisi. CCM sasa ni gereza la fikra mpya na pepo ya ibada ya sanamu.

Mwenyekiti wetu JPM juzi Dodoma amejaribu kukumbushia enzi za UVCCM iliyokuwa imejaa uzalendo lakini hakuwahi kuwa mwana UVCCM hiyo. Alikuwa anasimulia alivyosimuliwa. Namshauri akubali fikra tofauti ili taifa lisonge mbele na aiache CCM mpya ipambane na wapinzani kwenye siyo hoja za wapinzani kujibiwa na bunduki. Polisi watuachie chama chetu.
 
Back
Top Bottom