CCM ya Waswahili wa Pwani itadumu?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
CCM ya Waswahili wa Pwani itadumu?Ansbert Ngurumo

SASA ni dhahiri kwamba tuna vyama vya mapinduzi vingi ndani ya CCM. Kipo kimoja cha Jakaya Kikwete na Yusuf Makamba; kingine cha Ali Hassan Mwinyi na Malecela; kingine cha Yusuf Makamba na Aggrey Mwanri, na kingine cha kina Joseph Butiku.
Cha Mwinyi kinasikiliza, kinajifunza na kinasema kukosoana ‘ruksa.’ Cha Kikwete, Makamba na Mwanri kinachekacheka na kucheza dansi, huku kikiigiza sauti na tabia za wapinzani kwenye luninga, kupotosha umma na kukwepa hoja katika mjadala wa kitaifa. Nguvu yake inategemea ‘takataka’ za kina Richard Tambwe Hiza na wachumia matumbo wengine!

Kile cha kina Butiku ni mithili ya mimba inayomlilia mama yake asiitoe; kinatamani kuishi katika tunu, misingi na fadhila zilizokiasisi, lakini wenye nguvu wa zama hizi wanasema: ‘no way!’

Mzee Butiku wiki hii amekuwa shujaa mwingine wa kitaifa, aliyerejea kauli iliyohitimisha uhai wa Horace Kolimba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, kwamba CCM imekosa dira na mwelekeo. Tunaamini kwamba Mzee Butiku ‘ataachwa’ aitetee kauli yake.

Naamini watawala walijifunza kwa tukio la kifo cha Kolimba, kwani laiti wangemuacha Kolimba afafanue kauli yake, CCM ya leo ingekuwa tofauti kabisa. Ingekuwa moja, imara na yenye dira aliyokuwa akiizungumzia.

Uimara unaoonekana sasa kwa CCM unatokana na serikali. Chama kinategemea zaidi nguvu ya dola. Nadhani niliwahi kusema huko nyuma kwamba CCM ya sasa ni kama KANU ya Daniel arap Moi. Ilipoondoka Ikulu haikuwa KANU ile ile.

Kauli ya Butiku kwamba CCM inaelekea kwenye kifo chake, imenikumbusha kauli ya kigogo mwingine aliyewahi kuniambia kuwa CCM ya sasa ni kama tairi la gari ambalo limetumika kwa muda mrefu, limejaa pumzi na sasa linakaribia kupasuka.

Alikifananisha chama hicho na dola nzee inayoelekea kwenye anguko.

Aliongeza kuwa CCM haipo tena, bali kuna mkusanyiko wa watu wanaofahamiana ambao hushikamana tu wakati wa uchaguzi. Hugawanyika na kufa mara tu baada ya uchaguzi, kwa sababu misingi imeshabomolewa.

Kwa mujibu wake, utawala wa sasa wa CCM na serikali ndiyo utakuwa chanzo cha anguko la CCM, kwa sababu uwezo wake sasa unategemea usanii, ubabe wa dola, ujinga wa wapiga kura, woga wa wananchi na mambo mengine.

Alikifananisha chama hicho na Dola ya Kirumi ambayo ilivuma sana kwa karne kadhaa, lakini wakati ulipofika dola hiyo hiyo ikamong’onyoka taratibu na kuanguka kwa kishindo kikuu. Viongozi walijisahau, wakakumbatia anasa. Na miongoni mwa walioangusha dola hiyo ni maswahiba wao!

Kama dola ya Kirumi ilianguka, ni kipi kitaizuia CCM hii ya Waswahili wa Pwani kuanguka? Mwingine alisema CCM ya sasa imejengwa juu ya mbinu zilizoiweka madarakani mwaka 2005; mbinu za uchonganishi, kupakana matope, migawanyiko na ubaguzi.

Na kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ubaguzi unapopewa nafasi hauishii pale ulipoanzia. Unakuwa kama moto wa kiangazi.

Hisia hizi hizi nimeziona katika kauli ya mzee Butiku. Nimeona hasira na kukata tamaa. Zaidi ya hayo ni hasira ya muda mrefu. Kwa sababu zozote zile, watu makini hawawezi kupuuza kauli ya mzee Butiku, kama wengine wanaojaribu kutoa kejli za kitoto dhidi yake. Hoja yake iko imara.

Naamini mzee Butiku asingeibuka leo kusema aliyoyasema, wala asingefika mahali pa kuonyesha nakala ya waraka wake kwa mwenyekiti wa CCM, ulioandikwa miaka miwili iliyopita.

Chama chake kimempuuza na kimeshindwa kujirudi. Uvumilivu na ukimya wake vimefikia kikomo. Akaamua kuwajulisha Watanzania jinsi alivyopuuzwa na wale wale wanaojidai kumuenzi Mwalimu Nyerere.

Taifa litaendelea kumshangaa Katibu Mwenezi wa CCM, Mwanri anayemkejeli mzee Butiku na kumkemea akisema angepeleka maoni yake kwenye chama badala ya kuyaweka mbele ya waandishi. Mwanri anajifanya kichekesho kwa wanaojua kwamba naye ana waraka huo ‘mezani kwake’ kwani mzee Butiku aliusambaza kwa wajumbe wote wa NEC tangu miaka miwili iliyopita.

Mwanri amezama katika siasa za usanii. Amesahau kumbukumbu zilizo kwenye mafaili yake.

Hakumbuki hata kanuni za chama, hadi mzee Malecela na Mwinyi wamkumbushe kuwa Butiku ana ruksa na haki, kwani aliapa: ‘Nitasema ukweli daima, fitina kwangu mwiko.’

Sisi tunabaki kujiuliza. Mwanri si Katibu Mwenezi wa CCM? Mwinyi si Mwenyekiti Mstaafu wa CCM? Malecela si Makamu Mwenyekiti wa CCM? Mwanri na Malecela wanaongoza chama kimoja? Sasa Mwanri ‘anaeneza’ nini? Wote bado wanaiamini misingi, kanuni na imani za CCM?

Mambo haya yanatukumbusha simulizi la kauli mbili tofauti za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Rashid Kawawa.

Ni kwamba, siku chama kilipokuwa kinamuaga mzee Kawawa (alipostaafu rasmi siasa za majukwaani), katika hotuba ya shukrani alisema, pamoja na mambo mengine: ‘Naahidi nitakufa nikiwa mwanachama mwaminifu wa CCM.’

Ilipofika zamu ya Mwalimu Nyerere kuzungumza, akasema: ‘Rashid una roho ngumu. Utakufa mwanachama mwaminifu wa CCM? Mimi siwezi kuyasema haya. CCM inaweza kubadilika. Siku ikiacha misingi, nami naachana nayo, kwa sababu CCM si mama yangu. Ninaye mama mmoja na siwezi kupata mwingine...’

Ndiyo maana aliwahi pia kusema kuwa maendeleo ya nchi yanategemea CCM madhubuti. Hii tuliyo nayo sasa ni goigoi! Ni huyo huyo pia aliyetamani CCM ikatike vipande viwili ili kuleta upinzani makini.

Je, yawezekana zama za upinzani makini ndo zinaanza kujiunda? Lakini je, upinzani makini utaletwa na watu waoga? Wako wapi wana CCM wengine, wenye uchungu na chama chao, wanaomuunga mkono mzee Butiku hadharani – liwalo na liwe?

Kama wangejitokeza, hatua hii ingesaidia mambo kadhaa. Kwanza, ingewashtua watawala kubadilika na kurejea katika misingi wanayoitupilia mbali. Wangejenga na kusimamia upya misingi ya uongozi na utumishi bora kama ilivyoasisiwa na CCM.

Na kama wangeshindwa kubadilika, ingekuwa fursa ya hawa wasiokubaliana nao kujitoa kabisa ili wasiwe sehemu ya ubovu wanaoukemea.

Ni wazi kwamba wengi sasa wanakubali kwamba ni vigumu kukirekebisha chama wakiwa ndani. Bora watoke walisaide taifa wakiwa nje.

Kadiri wanavyoendelea kubaki ndani, huku wakijua kabisa kwamba chama kinaendelea kuzama, wajue kuwa wakati utafika nao watazama pamoja nacho, na hawatapata faida ya malalamiko yao.

Nashawishika kuamini kwamba kama Mwalimu Nyerere angekuwa hai leo, asingekuwa ndani ya CCM hii. Yawezekana pia kuwa kama angekuwa hai, hata CCM hii isingekuwapo, maana asingewaruhusu waifikishe huko; au wao kwa kujua uwezo wake na ‘adhabu’ ambayo ingeweza kuwapata, wasingejiruhusu kufika hapo walipo leo.

Watawala wetu wanajisahau. Mwalimu Nyerere bado ana nguvu leo katika mioyo ya Watanzania. Ni vema wajue kuwa misukosuko inayowapata leo inatokana na ukweli kwamba wananchi wamegundua kuwa watawala wetu wamempuuza Mwalimu Nyerere, na wanashindana na wananchi wake.

Wakubali, wakatae; vigezo vilivyowekwa na Mwalimu Nyerere ndivyo vitakavyoendelea kuwapima viongozi wetu wa sasa na wa baadaye.

Mwanzoni mwa utawala wa Rais Kikwete, baadhi ya mashabiki wake walianza kupenyeza hisia kwamba sasa amepatikana Nyerere mpya. Du! Hili nalo lilikuwa tusi kwa Mwalimu Nyerere, maana naamini hata Kikwete mwenyewe hawezi kudiriki kujifananisha naye.

Mwalimu Nyerere alikuwa mtu mwenye dhamira safi. Nguvu yake ilitokana zaidi na uadilifu wake binafsi. Alikuwa na uwezo wa kuwaambia ndugu zake na rafiki zake kile alichokuwa anawaambia Watanzania wengine wote. Hakuwa mpenda anasa. Hakutumia siasa kujitajirisha.

Ndiyo maana hata akiwa mstaafu, Mwalimu Nyerere alikuwa na nguvu ‘kuliko hata dola yenyewe.’

Wanaokumbuka jinsi alivyosambaratisha uamuzi wa Bunge lililoridhia Muungano wa serikali tatu, watakubaliana na nguvu ya Nyerere, ambayo pia ilichangiwa sana na uwezo wake wa kujenga hoja na kushawishi kwa kutazama pande zote za hoja.

Aliposhindwa kuwashawishi kwa hoja za kihistoria, akawarejesha kwenye sera za CCM, na kuwauliza: ‘Serikali tatu ni sera yenu?’ Wakaitupa, hata bila kukubaliana naye, huku wakiogopa pia kuondoka kwenye chama.

Ushawishi wa Mwalimu Nyerere ulidhihirika pia katika mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia CCM mwaka 1995, alipomwengua Kikwete na kumpitisha Mkapa. Hakuwa na dola. Alikuwa na karama ya ziada ambayo viongozi wetu wa leo hawana.

Mwinyi na Mkapa leo wana nguvu gani na ushawishi gani? Hata Kikwete hana ushawishi tena. Amebaki na nguvu ya dola, mabavu yanayotokana na ‘uhalali’ wa urais wake. Akiondoka madarakani leo atakuwa kama Mkapa anayekimbia maswali ya wanahabari.

Ushawishi, uwezo na uadilifu wa Nyerere ndivyo viliifanya CCM yake iwe moja; iwe na nguvu. Naamini mambo haya haya ndiyo yaliwafanya wanaCCM waimbe ‘zidumu fikra za mwenyekiti.’ Wao hawakuwa nazo; na hili limethibitika baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka. Leo wanashindwa kujaza ombwe la uongozi linalojitokeza.

Wakati wanaomba kura wanatuletea fikra za Nyerere katika maandishi. Hazimo mioyoni mwao. Wakishapata madaraka wanatekeleza miradi yao na ndugu zao.

Ndiyo maana sasa wananchi wamegundua kwamba dawa ni kuwazomea. Kama watawala hawajifunzi kutokana na zomeazomea hii; wananchi wakimaliza kuwazomea watachukua hatua nyingine, labda kali zaidi. Wamechoka kudanganywa na kutumiwa.

Ndiyo maana habari za kusikitisha za wakulima wa Tandahimba kuchoma moto nyumba ya Mbunge wa Jimbo hilo, Juma Njwayo, zinapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa kwani sasa Watanzania wameanza kujipigania, kujikomboa.

Ni tukio ambalo mabavu hayataweza kulikabili, kwani linatoka mioyoni mwa wananchi. Ajabu ni kwamba mambo haya haya yanajitokeza wakati kina mzee Malecela wanajitapa (mbele ya wananchi wale wale) kwamba CCM inatekeleza sera zake. CCM ipi?

http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/10/21/makala2.php
 
"Ni kwamba, siku chama kilipokuwa kinamuaga mzee Kawawa (alipostaafu rasmi siasa za majukwaani), katika hotuba ya shukrani alisema, pamoja na mambo mengine: ‘Naahidi nitakufa nikiwa mwanachama mwaminifu wa CCM.'

Ilipofika zamu ya Mwalimu Nyerere kuzungumza, akasema: ‘Rashid una roho ngumu. Utakufa mwanachama mwaminifu wa CCM? Mimi siwezi kuyasema haya. CCM inaweza kubadilika. Siku ikiacha misingi, nami naachana nayo, kwa sababu CCM si mama yangu. Ninaye mama mmoja na siwezi kupata mwingine...' "

Alama za nyakati,hapa ndipo busara za Nyerere zilikua zinaonekana,hakua mnafiki.
 
Nimeanza kusoma makala yako, ghafla nikakutana na spin ya "CCM ya watu wa pwani". Hizi ni kauli za kimakusudi kujaribu kuwagawa watu kutumia upwani na ubara. Hivi Upinzani wauwezi kushinda bila kutugawa Watanzania?
 
"Ni kwamba, siku chama kilipokuwa kinamuaga mzee Kawawa (alipostaafu rasmi siasa za majukwaani), katika hotuba ya shukrani alisema, pamoja na mambo mengine: ‘Naahidi nitakufa nikiwa mwanachama mwaminifu wa CCM.’

Ilipofika zamu ya Mwalimu Nyerere kuzungumza, akasema: ‘Rashid una roho ngumu. Utakufa mwanachama mwaminifu wa CCM? Mimi siwezi kuyasema haya. CCM inaweza kubadilika. Siku ikiacha misingi, nami naachana nayo, kwa sababu CCM si mama yangu. Ninaye mama mmoja na siwezi kupata mwingine...’ "
Alama za nyakati,hapa ndipo busara za Nyerere zilikua zinaonekana,hakua mnafiki.

Haya maneno yalikuwa mazito sana na yanaweza kusemwa na watu makini na ambao wana uchungu na nchi siyo mafisadi na wapenda madaraka.
 
Ilipofika zamu ya Mwalimu Nyerere kuzungumza, akasema: ‘Rashid una roho ngumu. Utakufa mwanachama mwaminifu wa CCM? Mimi siwezi kuyasema haya. CCM inaweza kubadilika. Siku ikiacha misingi, nami naachana nayo, kwa sababu CCM si mama yangu. Ninaye mama mmoja na siwezi kupata mwingine...

Hawa wanasiasa wanatakiwa kuweka Maslahi ya Nchi mbele, sio ya Chama na yao binafsi. Nyerere was a Smart person, tutamkumbuka daima.
 
Nimeanza kusoma makala yako, ghafla nikakutana na spin ya "CCM ya watu wa pwani". Hizi ni kauli za kimakusudi kujaribu kuwagawa watu kutumia upwani na ubara. Hivi Upinzani wauwezi kushinda bila kutugawa Watanzania?

Nadhani ulichokiona kati ya haya yote ni hilo la CCM ya Pwani. Dont rush for non sense, angalia contents. Kuna ujumbe mzito hapa. Makundi yapo hata huko CCM, Kuna Mtandao, CCM halisi nk, sasa iweje useme Wapinzani wanawagawa wakati mlishagawika tayari? CCM ndio inayowagawa watu.
 
Ilipofika zamu ya Mwalimu Nyerere kuzungumza, akasema: ‘Rashid una roho ngumu. Utakufa mwanachama mwaminifu wa CCM? Mimi siwezi kuyasema haya. CCM inaweza kubadilika. Siku ikiacha misingi, nami naachana nayo, kwa sababu CCM si mama yangu. Ninaye mama mmoja na siwezi kupata mwingine...

Hawa wanasiasa wanatakiwa kuweka Maslahi ya Nchi mbele, sio ya Chama na yao binafsi. Nyerere was a Smart person, tutamkumbuka daima.

Ha ha ha haaaaaaaaa Usitukumbushe wengine walisema sumu ya Nyerere inabidi wajinyonge.
 
Nadhani ulichokiona kati ya haya yote ni hilo la CCM ya Pwani. Dont rush for non sense, angalia contents. Kuna ujumbe mzito hapa. Makundi yapo hata huko CCM, Kuna Mtandao, CCM halisi nk, sasa iweje useme Wapinzani wanawagawa wakati mlishagawika tayari? CCM ndio inayowagawa watu.

I will definitely rush and address NONSENSE as I read on. Haina maana kwamba kama kuna contents nzuri na Subject ambayo ni nonsense nisiseme.

Jaribu kuacha kutumia, maneno yako mwenyewe, "Mlishagawanyika". Kukemea nonsense haina maana niko na chama chochote.

CCM haijawahi kuwa na "CCM ya Waswahili wa Pwani" kama huyo propagandist Master Spinner Ansbert anavyosema. Anaonyesha chuki ya wazi kwa watu wa pwani.
Ujumbe mzito unaweza kuwepo lakini nonsense itamulikwa hata kama itajificha na points nyingine za maana.
 
Hii ni makala nzuri sana ingawaje hilo la CCM ya Waswahili wa Pwani nafikiri angeweza kuiandika makala hii bila kutumia kichwa hicho.

Kitu kimoja ambacho kinaanza kujitokeza, kila mtu anajua sasa kwamba CCM bomu, boti inaanza kuzama, lakini kitu ambacho wengi wetu tunakikosa hapa JF ni je liko wapi boti la kutuokoa? Tuna uhakika gani na lenyewe halivuji? Tuna uhakika gani na lenyewe halina mafisadi? Tuna uhakika gani kwamba sio tu linavuja, lakini kuna mamba wamekaa tayari kuturarua kabla hata boti halijavuka?

Nafikiri akina Ngurumo wangetusaidia pia kwa kutuonyesha sera za
vyama vya ushindani ambazo zitaweza kumwokoa Mtanzania.

Kuichukia CCM peke yake hakuwezi kuwa sababu ya vyama vya ushindani kuingia madarakani. Inabidi waingia kwa sera, kwa visions zao.

Lakini kwa muda sasa sioni sera zikijadiliwa zaidi ya kutuonyesha ubaya wa CCM, kitu ambacho wengi wetu tayari tunajua.

Mimi nitafurahi kuona mada pia za je kwanini nichague au nijiunge na CHADEMA, TLP, CUF au NCCR?
 
Mtanzania
Mawazo ya kwamba CCM ni mbovu; lakini tuende wapi(?) ni mawazo ya wengi pia humu. Na hasa mashabiki wa sisiem hutumia sana mtego huu kuteka akili za wengine.

Kwangu mimi falsafa ni moja tu: CCM wameshindwa kutekeleza matakwa yetu, basi waondoke. FULLSTOP. Katika nchi ya watu karibu milioni 40, utashindwaje kupata viongozi wengine? Suala la kwamba watakaokuja wanaweza kuwa wabovu zaidi ni hofu ya kitu kisichokuwepo.

Kama chanzo na msingi wa madaraka ni wananchi, sielewi kwa nini mwenye kampuni(wananchi) amwogope mtu aliyemwajiri(serikali) kumfanyia kazi. Fukuza yoyote anayeharibu kazi.
 
I will definitely rush and address NONSENSE as I read on. Haina maana kwamba kama kuna contents nzuri na Subject ambayo ni nonsense nisiseme.

Jaribu kuacha kutumia, maneno yako mwenyewe, "Mlishagawanyika". Kukemea nonsense haina maana niko na chama chochote.

CCM haijawahi kuwa na "CCM ya Waswahili wa Pwani" kama huyo propagandist Master Spinner Ansbert anavyosema. Anaonyesha chuki ya wazi kwa watu wa pwani.
Ujumbe mzito unaweza kuwepo lakini nonsense itamulikwa hata kama itajificha na points nyingine za maana.

Insurgent, kwa hili umekurupuka au labda niseme umegahfirika kwa sababu ya hasira tu. Kama sikosei wengine wanaweza kusema pia kwamba umeonyesha upeo mdogo wa mambo, naumshambulia bure mwandishi wa makala.

Mimi binafsi nashangaa unachukia nini au huelewi nini, kwa sababu hayo maneno unayoyaona magumu wengine tunaona kama vile Ngurumo ametumia 'nahau' ya Waswahili wa Pwani kufikisha ujumbe wake, kwani tunao usemi kuhusu 'Waswahili wa Pemba.' Hivi tukisema 'Waswahili wa Pemba hujuana kwa vilemba' tunakuwa a chuki dhidi ya watu wa Pemba? Huu ni usemi wa siku nyingi wenye maana ya ndani kabisa. Nina hakika Ngurumo asingeutumia huu kufikisha ujumbe wa makala hii, kwani ukiisoma vizuri unaona kwamba jina la makala limefikisha zaidi ujumbe mzito, na ndivyo ilivyuo, kwamba CCM imekuwa ya 'Waswahili wa Pwani.' Kama nawe hulielewi hili, basi, lakini hasira zako zinaonyesha mwandishi amefanikiwa!

Kuhusu wale wanaooogopa kuondoka kwa CCM, ni kwamba lazima kwanza ifanyike kazi moja kuu ya kuwaandaa watanzania juu ya ubovu wa CCM anhaja ya kuiondoa madarakani. Haya maneno ya kutaka kuangaia pande mbili kwanza ni propaganda nyingine za klutakak kuipa likizo CCM. Tuiahe ibanwe, imeyataka yenyewe, na ikishaondoka replacement itapatikana tu, hakuna chama ambachi ni indispensable. Kama alivyosema Invincible na wengine hapo juu, katika watu milioni 40 wapo wengi wenye akili uwezo, utashi na uzalendo wa kuongoza lakini hawana pa kupumulia na kjitokeza kwa sababu waliopo wameziba kila mwanya. Tunasema hivi, waondoke kwanzaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Mtanzania
Mawazo ya kwamba CCM ni mbovu; lakini tuende wapi(?) ni mawazo ya wengi pia humu. Na hasa mashabiki wa sisiem hutumia sana mtego huu kuteka akili za wengine.

Kwangu mimi falsafa ni moja tu: CCM wameshindwa kutekeleza matakwa yetu, basi waondoke. FULLSTOP. Katika nchi ya watu karibu milioni 40, utashindwaje kupata viongozi wengine? Suala la kwamba watakaokuja wanaweza kuwa wabovu zaidi ni hofu ya kitu kisichokuwepo.

Kama chanzo na msingi wa madaraka ni wananchi, sielewi kwa nini mwenye kampuni(wananchi) amwogope mtu aliyemwajiri(serikali) kumfanyia kazi. Fukuza yoyote anayeharibu kazi.

Invicible,

Hilo ndilo tatizo maana ili kuwafanya hao wananchi wawanyime kibarua CCM inabidi wawe wamejua kwamba CCM ni mbaya kuliko X.

Lakini kiini macho cha sasa ni hilo la kuambiwa ubaya wa CCM lakini hatuambiwi uzuri pia wa X.

Duniani kokote watu ni wagumu wa change na kama wanaona risk ya kubadili ni kubwa basi hubaki na status quo. Hili ndilo naliona
ni tatizo kubwa kwetu Tanzania.

Unaweza kuita ni ushabiki wa CCM, lakini ndio ukweli wenyewe, kwamba kama huoni kwa kurukia, ni bora ubaki na boti unalolijua, hata kama huko mbele litazama, kuliko kutaka kuruka na kuogelea kwenye maji usiyo na uhakika kama ni salama.

Pamoja na kuambiwa boti linazama lakini pia tuambiwe yale maji ni salama, tunaweza kuruka na kuogelea salama mpaka ufukweni.

Ninategemea vyama vya ushindani sasa vianze kuelezea tena mapema juu ya sera zao na nini wao watakuwa tofauti na CCM. Mpaka sasa naona hilo linakosekana. Hapa nilipo mimi kama kiongozi wa upinzani atatumia hotuba yake yote kuelezea ubaya tu wa chama tawala, nina uhakika kesho yake magazeti yote yatamwambia kakosa vision.
 
Mtanzania:
Wewe na mimi tunamtizamo sawa kuhusu ni wapi pa kurukia tunapoachana na hili boti bovu CCM. Wakati huu vyama vya Ushindani vinayo nafasi nzuri tu ya kutuonyesha waTanzania kwamba tusiwe na wasiwasi, kwani hawa wako tayari kutuvusha.
Hii ni nafasi ambayo hivi vyama vinatakiwa viitumie kuwashawishi waTanzania wakubali kuwapaa nafasi ya kuongoza nchi ifikapo 2010.

Sasa kuhusu jungu kuu: Kwa kuwa 'CCM imekuwa bomu' hivi wale watu wanaodhaniwa kuwa ni watu walio na msimamo unaokubalika waliomo ndani ya hii CCM bomu wao hawalioni hili bomu? Watakaa kwenye uzio hadi lini? Mpaka boti lote lizame kabisa? Butiku na akina Malicela wamekwishawafungulia mlango, tunataka tuwaone na wahesabiwe, vinginevyo tutataka boti zima lizame.
 
hii idea ya ubara na upwani na uzanzibari inapandikizwa kwenye akili za watu kwa kasi zote, ili ccm iwe rahisi kutawala.

na tuwe macho, hakuna kabila au mkoa bora kuliko mwengine, ni jinsi gani wewe utajiweka ndio cha umuhimu.

hizi propaganda za kikabila na zife, kabla amani haijavunjia
 
Insurgent, kwa hili umekurupuka au labda niseme umegahfirika kwa sababu ya hasira tu. Kama sikosei wengine wanaweza kusema pia kwamba umeonyesha upeo mdogo wa mambo, naumshambulia bure mwandishi wa makala.

Mimi binafsi nashangaa unachukia nini au huelewi nini, kwa sababu hayo maneno unayoyaona magumu wengine tunaona kama vile Ngurumo ametumia 'nahau' ya Waswahili wa Pwani kufikisha ujumbe wake, kwani tunao usemi kuhusu 'Waswahili wa Pemba.' Hivi tukisema 'Waswahili wa Pemba hujuana kwa vilemba' tunakuwa a chuki dhidi ya watu wa Pemba? Huu ni usemi wa siku nyingi wenye maana ya ndani kabisa. Nina hakika Ngurumo asingeutumia huu kufikisha ujumbe wa makala hii, kwani ukiisoma vizuri unaona kwamba jina la makala limefikisha zaidi ujumbe mzito, na ndivyo ilivyuo, kwamba CCM imekuwa ya 'Waswahili wa Pwani.' Kama nawe hulielewi hili, basi, lakini hasira zako zinaonyesha mwandishi amefanikiwa!

Kuhusu wale wanaooogopa kuondoka kwa CCM, ni kwamba lazima kwanza ifanyike kazi moja kuu ya kuwaandaa watanzania juu ya ubovu wa CCM anhaja ya kuiondoa madarakani. Haya maneno ya kutaka kuangaia pande mbili kwanza ni propaganda nyingine za klutakak kuipa likizo CCM. Tuiahe ibanwe, imeyataka yenyewe, na ikishaondoka replacement itapatikana tu, hakuna chama ambachi ni indispensable. Kama alivyosema Invincible na wengine hapo juu, katika watu milioni 40 wapo wengi wenye akili uwezo, utashi na uzalendo wa kuongoza lakini hawana pa kupumulia na kjitokeza kwa sababu waliopo wameziba kila mwanya. Tunasema hivi, waondoke kwanzaaaaaaaaaaaaaaaa!

Kichwamaji,

A spade will be a spade. Sisi sote ni waswahili, yeye ametumia Waswahili wa pwani kwa makusudi ya kuonyesha CCM ni chama cha wachache, tena wa pwani.

Point zinazofuata, zinaonyesha kupingana kwa mawazo ndani ya CCM yenyewe. Hii ni demokrasia ambayo huwezi kuiona kwenye vyama vya upinzani. Ni kweli ndani ya CCM wapo ambao, kama binadamu wengine wamekuwa "convinced" na tuhuma za wapinzani. Wako ambao wanajua nini maana ya chama na mawazo yao wameyafikisha mpaka Central Committee ya Chama. Tumeona tuhuma zilizofika CC zilivyowang'oa vigogo wa UWT, na vile vile wako ambao wametumia haki yao kuongea na vyombo vya habari kuhusu mawazo yao kuhusu kile kinachoendelea.

Binafsi, sipendi kusikia mtu akisema hakuna ufisadi ndani ya chama na kutoa "blanket statement" inayolinda kila mwanachama aliyetajwa kwenye list. Huwezi kutoa "blanket statement" kwa watu wote kwani uchunguzi haujakamilika. Na kama ilivyo tuhuma yoyote kuna ambao watapatwa na hatia na kuna ambao inawezekana wasipatwe na hatia. Tuhuma sio Hukumu.

Wengi hupenda kumnukuu mwalimu kuonyesha unabii wake kwamba Chama Cha Mapinduzi kitasambaratika. Na mimi nimnukuu, alisema "Bila CCM madhubuti Nchi Yetu itayumba". Hapa ni obvious anaamini inahitajika CCM, tena madhubuti nchi yetu isiyumbe. Ni ukweli usiofichika, upinzani tokea kuanzishwa umekuwa hauna dira. Kuanzia na CUF, ambayo ilitumia misikiti kuendesha kampeni mpaka NCCR iliyomegeka na kuunda TLP. Wapinzani wengi ni watu ambao wako blinded na hate, watu hawa hawajali kuhamasisha watanzania kuleta machafuko ndani ya nchi yao, hii kwao ndio njia ya kuiondoa CCM. "Shortcuts" zina madhara yake, na wavivu wengi hupenda shortcuts. Kama uhuru wa nchi hii tuliupata kwa kutumia akili na sio nguvu, vipi sasa twende kwa wananchi na kuwahamasisha otherwise?

Siandiki nachoandika kwa hasira kama vile unavyodhani. Shortcut ya kuwagawa watu kimajimbo, kikabila, etc ilimradi utawale, ni kitu kinachoboa.
 
. Shortcut ya kuwagawa watu kimajimbo, kikabila, etc ilimradi utawale, ni kitu kinachoboa.

Talking about calling a spade as a spade, basi hapa hakuna la kuongeza, the whole article juice yake ni hii sentesi moja tu!
 
Talking about calling a spade as a spade, basi hapa hakuna la kuongeza, the whole article juice yake ni hii sentesi moja tu!

ES,

Hapo ndio utakapooona unafiki wa hawa watu, tuliposema hapa Chadema ni cha wa Kilimanjaro tukaambiwa wakabila na tunataka kuigawa nchi kwa mtazamo wa kikabila, leo mwandishi anaelipwa na mbowe anaandika makala kuchochoea mgawanyiko wa jamii kwa upwani na ubara watu wanatetea wanasema tuangalie ujumbe uliopo ktk makala. Huu ni upuuzi na ndio umakengengeza wa JF wanaangalia mambo kama mwenyekiti mbowe. sasa leo ccm ishakuwa ya watu wa pwani kwa taarifa yenu watu wa pwani walishaporwa TANU ya siku nyingi na hawana mpango na ujinga unaousema ngurumo, wewe ngurumo endelea kula vya mbowe vitakutokea puani.
Es nilikuambia siku nyingi hawa chadema ndio wakabila namba moja si unaona sasa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom