CCM ya wakati ule na hii ya sasa nini kimekwenda kombo?

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,561
19,056
Miaka ya mwanzoni na kati ya 80 (1980s) wakati timu yetu ya taifa ya soka Taifa Stars ilipokua ikicheza katika uwanja wowote wa nyumbani, iwe pale Taifa shamba la bibi, CCM Kirumba pale Mwanza au Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha mashabiki walikua wakihanikiza na kelele za CCM, CCM, CCM pale Stars wanapofunga goli

Hawakua wakifanya hivi kwa unafiki bali kwa mapenzi ya dhati kwa Chama na uzalendo wa kweli kwa nchi yao na walifanya hivyo sio kwa kujipendekeza au kutaraji malipo ya fedha au upendeleo fulani kutoka kwa yeyote katika viongozi ama wa siasa au wa serikali

Hata katika jamii za Watanzania ilipokua ikitokea migongano na kutofautiana watu walikua wanaambiana twende CCM ambapo migogoro yao itatatuliwa. Hata ambao hawakua wanachama walilikubali hilo

Hivi sasa hali ni tofauti sana. Japo tupo katika mfumo wa vyama vingi lakini ni rahisi kuliona jambo moja, kwamba wengi wanaounga mkono hadharani chama hiki pembeni wanakisema vibaya pamoja na viongozi wake!

Kwa sasa mimi sio mfuasi wa Chama chochote cha siasa lakini uzoefu wangu unanambia hisia kama zile za miaka ya 1980s waweza kuziona hata kama ni kwa mbali kutoka vyama vya upinzani na kinachoonekana kwa waungaji mkono wa CCM ni unafiki na kujipendekeza

Nini kimetokea mpaka ikawa hivi? Mbona wakati huu CCM inarasilimali nyiingi sana kuanzia rasilimali vitu,rasilimali fedha hadi rasilimali watu, tena wenye ujuzi na usomi wa hali ya juu na ile rasilimali yenye turufu muhimu yaani rasilimali dola, lakini kila ukiangalia kwa jicho la tatu unagundua kuna ma opportunists watupu ambao kila mmoja ana jambo lake binafsi akisubiri ama kulipata ndani ya chama na serikali au tayari anafaidika na jambo flani binafsi ambalo inabidi aendeleze unafiki ili asijeletewa 'MATATIZO"
 
Sisi-m ya sasa hivi inawenyewe...

Sisi-m ya sasa hivi ni ya kutambuana kwa majina...


Cc: mahondaw
Watu walijitolea muda, nguvu na mali zao kwa mapenzi ya Chama na nchi yao na wala hawakutarajia malipo ya pesa, vyeo au fursa za kiuchumi wakijua wanajenga Tanzania boa ya baadae kwa ajili yao na vizazi vijavyo
 
Back
Top Bottom