Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Ukiwasikia baadhi ya makada maarufu ndani ya CCM, hasa walioko benchi, wakiwemo Nape Nnauye, Hussein Bashe, Prof. Mark Mwandosya, Bernard Membe etc, etc, etc; utabaki kushangaa namna wanavyokikosoa vikali tena bila aibu Chama chao, huku wakitabiri mara kwa mara kuwa, kwa mwendo wa CCM chini ya utawala wa Awamu ya Tano, Chama hicho kitaanguka.
Hata hivyo, ukifuatilia kwa undani, utagundua kuwa, makada hao hawaongei maneno yanayotoka moyoni bali sana ajenda yao binafsi.
Hii ni kwa sababu, Watanzania wengi hasa wana-CCM walipata shida sana katika kipindi cha pili cha Utawala wa Kikwete, hasa miaka yake mitatu ya mwisho (2013-2015) kuanzia kipindi cha Mchakato wa Katiba mpya hadi mchakato wa Uchaguzi Mkuu.
Kipindi hicho, wana-CCM wengi walikuwa wanajiona wanyonge na wakati mwingine wakibadilisha mavazi yao kila mara baada ya kumalizika kwa mikutano ama vikao vya Chama.
Licha ya kuwepo kwa Kampeni za kujivua gamba, pamoja na Ziara ya miaka miwili ya Kinana na Nape Nchi nzima (2013-2015) na kupata wanachama wapya 284,300 huku 38,984 walitokea Vyama vya Upinzani, wakiwemo viongozi, bado haikutosha kukiuza vya kutosha Chama cha Mapinduzi kwa umma na ililazimika kupoteza mwaka 2015 asilimia 3% zaidi ya zile 61% za urais ilizopata mwaka 2010. Hiyo inaonyesha wazi kuwa, mabaya ya CCM yalikuwa mengi kuliko mazuri.
Leo CCM ya Dk. Bashiru na Polepole, ikipata ushirikiano usio wa kinafiki kutoka kwa Mwenyekiti wao, inavutia watu wengi zaidi kujiunga na CCM, halafu kuna vichwa maji wengine wanakasirika kweli. Leo hii kila mwana-CCM anajiona fahari kuvaa sare ya CCM tofauti na kabla ya mwaka 2015.
Nadhani hapa wajuvi wa mambo na wazee wenzangu wa kutokwa mapovu tutaweza kutiririka katika hoja hii.
Je, Nape anaona wivu juu ya usajili wa mwenzake kuwa umetishia legacy yake ndani ya CCM ama anakerwa tu kuona Wapinzani wakijiunga CCM?