CCM ya Mwalimu Nyerere haiwezi kutokea tena


activisty

activisty

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Messages
315
Points
195
activisty

activisty

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2012
315 195
Nashuhudia nia za urais ndani ya chama cha mapinduzi zikitangazwa kwa mbwembwe za aina yake.Lowassa, Wassira, Mwigulu n.k na wengine wengi ambao bado wanatarajia kutangaza nia.

Naziita mbwembwe kwa sababu kuu moja, nia hizi hazina uhalisia. Sio nabii, na pia kuliona na kufahamu hili haliitaji unabii historia inajieleza.

Mwaka 2005 tuliwashudia watu kama Prof. Mwandosya, Salim ahmed Salim, J.Kikwete n.k wakichuana ndani ya CCM, ili kupata nafasi ya kuwania urais. Mbio za watu hawa mwaka 2005, zilionesha sura ya uhalisia wa jambo piganiwa, ingawaje matokeo yaliigeuza sura ile.

Lakini leo miaka kumi baadaye (2015), watanzania tunaaminishwa tena kuwa urais ni lele mama. Yamesemwa mengi, na watangaza nia, kila mmoja akija na kauli yake lakini je, dhamira ya kweli ipo? Kwa ufupi niseme tu kuwa, inawezekana kuwa na watangaza nia wengi sana ndani ya ccm huu mwaka lakini swali ni je wametoka wapi?

Kwanini wamejitokeza sasa?miaka ya nyuma hawakuwepo? Je yale makundi ndani ya CCM yamepotea? Wako wapi Tanzania kwanza? Viko wapi vile vyama vya misimu? Wako wapi wale wapinga ufisadi?

Si jambo dogo hata kidogo, na tusipokuwa makini Tanzania itayeyuka mithili ya theluji. Kwa ufupi naona makundi mawili ndani ya CCM, na makundi hayo yametoa watu wawili ambao watashindana ndani ya ccm katika nani awanie urais.

Wengi wametangaza nia kama kivuli cha ushawishi kwa wananchi, ila nyuma ya pazia ukweli ni kuwa wote wapo nyuma ya watu hao wawili, ambao ni zao la makundi mawili yaliyojengeka ndani ya CCM, makundi yaliyoanza kujengeka mara tu baada ya uchaguzi mkuu 2005, makundi ambayo yameifikisha Tanzania na watanzania hapa walipo sasa.

Makundi yenye nguvu ndani ya ccm, na makundi ambayo yapo tayari kufanya lolote kuhakikisha yanaendelea kujilinda ndani ya ccm na nje ya CCM.

Pengine yalikuwepo awali lakini sasa ndio yanaonyesha makucha yake hadharani. Zao la ufisadi, chuki, umasikini, na ung'ang'anizi wa madaraka.

Vyote ni zao la utengano ndani ya ccm. Kwa mwanachama anayetafuta kula, HILI HALITAMWINGIA AKILINI. Halikadhalika kwa mwanasiasa anayetafuta na kushikilia madaraka kwa ajili ya kula, hili halitamwingia akilini.

Lakini kwa raia ambaye alishaenda zahanati ya kata kupatiwa matibabu huku ikiwa ndio tegemeo lake la mwisho, kwa mtumiaji wa daladala Dar es salaam, kwa mwanafunzi aliyeko chuoni, pengine kakosa mkopo kabisa ama pengine kapata lakini amekaa miezi mitatu hajapatiwa fedha ya kujikimu, na kwa mwalimu aliyepangia kule kijijini, hana pa kushukia, mshahara mdogo, hali ngumu, na watanzania wengine wengii, waliovaa sura zinazofanana na hizi HILI LITAWAAINGIA AKILINI.

CCM iliyokuwa chini ya waziri mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine, na CCM iliyokuwa chini ya rais hayati mwalimu J.K.Nyerere, sio CCM tuliyonayo sasa, na siyo CCM itakayokumbukwa Tanzania.Nilisema 2012 KIFO CHA CCM KIMETIMIA, nikiwa nalenga mwaka 2015.

Lakini yote yatatokana na uamuzi wa wananchi juu ya hili. Kwanza ndani ya ccm je ni Lowassa? Au ni Membe? Nani awanie urais kwa chama hicho? Wanaccm wakijitambua, watautambua uamuzi wa kufanya.

Na je, ni TLP,UDP,CHADEMA,CUF,NCCR,ACT au ni UKAWA? Wale wapinzani wakijitambua watapata pia uamuzi wa kufanya lakini yote wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho.

Tusijidanganye CCM ya mwalimu itarudi tena, tutizame watu kwa jicho la tatu, tuwakatae mapema na kuwapinga kama mwalimu alivyofanya, ama tukae kimya tuwaache waendelee kututafuna na kubaki masikini.

Nimalize kwa kusema urais si lele mama, narudia urais si lele mama, nenda kajiandikishe kwa gharama yeyote ile.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.

By True ACTIVISTY-activistyi@yahoo.com.
 
I

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Messages
2,752
Points
2,000
I

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2014
2,752 2,000
Bora wakoloni warudi tu otherwise nchi itamalizwa kwa ufisadi
 
D

Descartes

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2013
Messages
2,769
Points
2,000
D

Descartes

JF-Expert Member
Joined Jul 24, 2013
2,769 2,000
Kila zama na kitabu chake...
 
L

ligati

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2015
Messages
223
Points
170
L

ligati

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2015
223 170
Sasa kwanini itokee upya,,sema tu unataka CCM bora na thabiti ,lakini sio lazima iwe Kama ya hayati Nyerere.
 
activisty

activisty

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Messages
315
Points
195
activisty

activisty

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2012
315 195
Sasa kwanini itokee upya,,sema tu unataka CCM bora na thabiti ,lakini sio lazima iwe Kama ya hayati Nyerere.
Ya hayati mwalimu, ilikua bora na thabiti pia.
 

Forum statistics

Threads 1,283,910
Members 493,869
Posts 30,805,818
Top