CCM ya Muunga Mkono Raila Odinga Urais Kenya ,Yawakilishwa na Magufuli Mkutano wa Uteuzi

kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,025
494
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha CCM imeingiza Taifa katika siasa za Ukanda wa nchi jirani baada ya kutuma na kuwakilishwa na mwanachama na waziri wa Ujenzi katika mkutano Mkuu wa uteuzi wa Mgombea Urais nchini Kenya kupitia muungano wa ODM/CORD Eng.Raila Ammolo Odinga (RAO).Katika mfumo wa vyama vingi nchini Kenya ambapo kuna kambi tofauti mbili kubwa zinazoshindan ni kukosa busara kwa nchi huru na serikali iliyopo madarakani kuonyesha upendeleo wa wazi kwa wagombea Urais.Pia maswali ya kujiuliza ni kwamba John Magufuli ni Waziri wa nchi na siyo kiongozi wa chama pia ni mwanaccm asiye na wadhifa kwenye chama maana siyo MNEC ,CC inakuwaje anawasilisha ccm wakati kuna viongozi pure wa kazi hizo kutoka Sekretariati na CC ya CCM?.Wapi NEPI katibu mwenezi,Wapi Mangula,Makamu Mwenyekiti ,Wapi Kinana Katibu Mkuu, Wapi Mukama,Makamba snr, Kingunge ?.Je kama Magufuli amewakilisha CCM gharama zote za kwenda kwenye mkutano huo amelipiwa na ccm au Kodi ya wananchi kutoka katika ofisi ya Wizara ya Ujenzi?.au Magufuli amekwenda kwa hiari yake ?,siyo rahisi kwa Mujibu wa KTN TV News, Magufuli ni mwakilishi wa CCM.
Je kambi ya Uhuru na Ruto ikishinda Uchaguzi huo wa machi 2013 mahusiano ya nchi hizi mbili ambazo pia ni wanachama wa EAC yatakuwa katika hali gani huku CCM ikiwa bado madarakani?.
Kwa siasa hizi za CCM ni janga katika siasa za Ukanda na inataka kuwaletea wananchi wa Taifa lao lisiaminiwe tena katika siasa za kutoingilia mambo ya ndani ya nchi.
 
Hata bibi yangu ambaye hakwenda shule hata kidogo asingeingilia jambo la jirani yake lenye utata wa namna hii. Nadhani sala zetu zinawafanya waehuke. Nawaombeni nyote tukazane kuomba, they will all perish! Wametunyanyasa vya kutosha.
 
Pacha wa CCM ni KANU, wamekua pamoja na kufanya ufisadi ktk nchi zao pamoja. Hapa ilitakiwa wamuunge mkono Uhuru Kenyata.
 
Ukiwa ndani ya CCM inabidi ujitoe fahamu. Huyo ndio Dr Magufuli mwenye Phd ya kemia ya UDSM. Yale yale yalikwishawahi kusema, watu wazima wasomi lakini akili zao wameamua kuziweka mfukoni. What if RAO akishindwa? Ni lini Kenya walishawahi kuja kushadadia uchaguzi wetu na hata kutuma wawakilishi kwenye mikutano ya vyama? Kwa nini tusingeamua kuwa neutral tu? na huyo Magufuli ahakikishe amehudhuria mikutano ya vyama/kambi zote zinazogombea huko Kenya ili basi 'asawazishe' uchemfu huu!
 
Takalani Sesama , huko sahihi ulicho sema ugumu ni kuwa Magufuli ataweza kusema kwenye mkutano wa Uhuru na Ruto yale aliyoyasema kwenya Mkutano wa CORD/ODM wa Raila?,Mbona atakuwa kichekesho kwa nchi kuwa na marais wawili kwa wakati mmoja
 
Back
Top Bottom