mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,753
- 7,075
Wana Jf,
Katika watu wanaoleta hisia mzito mpaka kufikia hatua ya kutoa machozi ni pale unapoona watu wakishangilia urejeshwaji wa usafiri wa Treni, ufufuaji wa njia nyingi za treni tena nyingine watu walijenga juu yake hata kufika mitalimbo ya chuma kuitumia kama nguzo.
walioshiriki kuua njia hizi ni hizi tawala za Mkapa na Jk, mfano. Mkoa wa Kagera, Katavi bei ya vitu kama sukari, cement , mabati nchi nzima ilikuwa sawa,lakini baada ya kumaliza kujenga barabara ya lami dar- mtukula hujuma mbali mbali zilianza, Mara waangushe treni za mizigo, Mara za abiria. Tulishuhudia watu wengi wakifa, njia hii ikawa sio ya uhakika tena.
jinsi Mkapa na JK walivyosababisha kufa kwa usafiri wa UMMA hilo hawawezi kulikwepa kwani baada ya kufa usafiri wa reli kulijitokeza makampuni mengi ya kusafirisha mafuta, vifaa vya ujenzi, chakula, kila kitu kilipanda mpaka watu walitamani kutumia bidhaa za nchi za jirani.
Haya maroli ndio yanayotesa barabara zetu mpaka Leo, barabara zimekuwa za marekebisho ya Mara kwa Mara huku tukitumia gharama kubwa ambazo zingeepukika.
Hili swala LA kusifia Ccm ya Magufuri kwa kurejesha usafiri wa reli ni LA kushangaza mno kwani waliohua reli hizi wapo. Ifike hatua waliotenda makosa ya makusudi nao washitakiwe angalau walipe gharama kwa makosa waliyoyatenda . Haiwezekani unaua NASaCO, UDA, KIUTA, NMC alafu unaachwa ili watakaofanya kazi ya kufufua ndio waonekane watendaji makini.