Cherenganya
JF-Expert Member
- Jan 21, 2018
- 2,309
- 1,775
Kuna jambo wanaCCM wanatakiwa kulielewa na waonyeshe kwamba wamelielewa. CCM inajisuka upya, CCM inafanya overhaul inataka Taasisi kuwa kubwa kuliko mtu.Tangu aingie madarakani Rais Magufuli amevuruga diplomasia ya nchi yetu kwa kiwango cha hali ya juu kuliko wote waliomtangulia.
Kipindi cha Baba wa Taifa, Julius Nyerere, Tanzania ilikuwa maarufu sana katika diplomasia ya kimataifa huku yeye mwenyewe akiheshimika duniani lakini pia tulikuwa na vijana wake mfano wa Salim Ahmed Salim waliomsaidia kuimarisha mahusiano ya kimataifa.
Mzee mwinyi naye hakuwa nyuma kwenye ushirikiano wa kimataifa, kipindi cha mzee huyu ndipo Salim Ahmed Salim alitumika kama Katibu Mkuu wa OAU (1989–2001), Rais Mwinyi na serikali yote ilimuunga mkono na kumtia nguvu. Hayati Mkapa alifufua Jumuiya ya Afrika Mashariki, pia alimsapoti Salim, kipindi chake pia kulikuwa na Watanzania wengi waliokuwa wanafanya kazi kwenye jumuiya za kimataifa wakiiwakilisha vema nchi yetu na kuitangaza.
Rais Kikwete alimtoa na kumpa sapoti ya nguvu Asha-Rose Migiro kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na wengine wengi.
Sasa njoo kwa huyu, sidhani hata kama kuna mtu amemuwezesha kuwepo kwenye ngazi za kidunia akifanya kazi na kuitangaza nchi yetu. Kama kukiwa na mtanzania kwenye jumuiya za kimataifa basi yaweza kuwa ni juhudi binafsi ama wao ndiyo wamemuona lakini hakuna sapoti kabisa kutoka kwa Rais Magufuli. Zaidi zaidi anawaona waliobahatika kupata uongozi jumuiya za kimataifa kama wasaliti na mawakala wa anaowaita mabeberu.
Kipindi hiki kumekuwa na kijana Stephen Masele msomi mzuri aliyepata elimu bora kabisa kwenye vyuo vikuu vya nje kikiwamo Chuo Kikuu bora kabisa duniani cha Harvard, kijana huyu amekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Pan-African tangu 2018 akiiletea sifa kemu kemu Tanzania.
Kwa kutokuona umuhimu wa Tanzania kuwa na mtu kwenye chombo hiki muhimu kabisa cha AU, CCM ya Magufuli imemkata kwenye nafasi yake ya kugombea ubunge kupitia jimbo la Shinyanga Mjini. Na kwa kuwa ili uendelee kutumika kama Makamu wa Kwanza wa Rais Bunge la Pan-African ni lazima uwe mbunge kwenye nchi yako, hivo basi Kijana Masele na nchi imepoteza fursa adimu na adhimu kabisa.
MLALE SALAMA!
Na ili Hilo litimie maumivu hayatakoma mpaka wanataasisi waelewe Hilo.
Ni Kama ambavyo katika Serikali yake alitimua timua Ila watu bado wakawa hawajamuelewa Ila alipomtimua Mkurugenzi wa Taasisi Ogopwa Viongozi serikalini wakajua kwamba sasa muda wa masihara kweli hakuna.