CCM ya Magufuli ni ya kijima kweli kweli: Hivi unamkataje Stephen Masele, Makamu wa Kwanza wa Rais Bunge la Pan-African, chombo muhimu cha AU?

CreativityCode

Senior Member
Aug 8, 2020
158
653
Tangu aingie madarakani Rais Magufuli amevuruga diplomasia ya nchi yetu kwa kiwango cha hali ya juu kuliko wote waliomtangulia.

Kipindi cha Baba wa Taifa, Julius Nyerere, Tanzania ilikuwa maarufu sana katika diplomasia ya kimataifa huku yeye mwenyewe akiheshimika duniani lakini pia tulikuwa na vijana wake mfano wa Salim Ahmed Salim waliomsaidia kuimarisha mahusiano ya kimataifa.

Mzee mwinyi naye hakuwa nyuma kwenye ushirikiano wa kimataifa, kipindi cha mzee huyu ndipo Salim Ahmed Salim alitumika kama Katibu Mkuu wa OAU (1989–2001), Rais Mwinyi na serikali yote ilimuunga mkono na kumtia nguvu. Hayati Mkapa alifufua Jumuiya ya Afrika Mashariki, pia alimsapoti Salim, kipindi chake pia kulikuwa na Watanzania wengi waliokuwa wanafanya kazi kwenye jumuiya za kimataifa wakiiwakilisha vema nchi yetu na kuitangaza.

Rais Kikwete alimtoa na kumpa sapoti ya nguvu Asha-Rose Migiro kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na wengine wengi.

Sasa njoo kwa huyu, sidhani hata kama kuna mtu amemuwezesha kuwepo kwenye ngazi za kidunia akifanya kazi na kuitangaza nchi yetu. Kama kukiwa na mtanzania kwenye jumuiya za kimataifa basi yaweza kuwa ni juhudi binafsi ama wao ndiyo wamemuona lakini hakuna sapoti kabisa kutoka kwa Rais Magufuli. Zaidi zaidi anawaona waliobahatika kupata uongozi jumuiya za kimataifa kama wasaliti na mawakala wa anaowaita mabeberu.

Kipindi hiki kumekuwa na kijana Stephen Masele msomi mzuri aliyepata elimu bora kabisa kwenye vyuo vikuu vya nje kikiwamo Chuo Kikuu bora kabisa duniani cha Harvard, kijana huyu amekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Pan-African tangu 2018 akiiletea sifa kemu kemu Tanzania.

Kwa kutokuona umuhimu wa Tanzania kuwa na mtu kwenye chombo hiki muhimu kabisa cha AU, CCM ya Magufuli imemkata kwenye nafasi yake ya kugombea ubunge kupitia jimbo la Shinyanga Mjini. Na kwa kuwa ili uendelee kutumika kama Makamu wa Kwanza wa Rais Bunge la Pan-African ni lazima uwe mbunge kwenye nchi yako, hivo basi Kijana Masele na nchi imepoteza fursa adimu na adhimu kabisa.

MLALE SALAMA!
 
CCM ndio inajielewa Sasa inatudhihilishia wananchi kuwa siyo Mali ya mtu/watu fulani. Kuna genge moja la kisiasa ukishakuwa maarufu tu wa kutukana tukana hovyo wewe ndo unakuwa ushajihakikishia utawala wa kudumu kugombea ndani ya Chama Tena utapitishwa kwa kura za ndio na Hapana utafikiri wanachagua mwenyekiti wa TANU.

CCM itaendelea kuwa kioo Cha siasa nchini na taasisi inayoendesha vyama vyingine nchini. Ukitaka kuamini Hilo CDM ipo tayari hata kumuengua mgombea wake ili tu kigogo aliekatwa kutoka CCM apewe yeye kugombea.
 
Vipi kama anamuhitaji kuongoza taasisi za ndani ili kujiletea maendeleo? Tulieni
 
CCM ndio inajielewa Sasa inatudhihilishia wananchi kuwa siyo Mali ya mtu/watu fulani. Kuna genge moja la kisiasa ukishakuwa maarufu tu wa kutukana tukana hovyo wewe ndo unakuwa ushajihakikishia utawala wa kudumu kugombea ndani ya Chama Tena utapitishwa kwa kura za ndio na Hapana utafikiri wanachagua mwenyekiti wa TANU.

CCM itaendelea kuwa kioo Cha siasa nchini na taasisi inayoendesha vyama vyingine nchini. Ukitaka kuamini Hilo CDM ipo tayari hata kumuengua mgombea wake ili tu kigogo aliekatwa kutoka CCM apewe yeye kugombea.

Yaani kama vile Shilinde alivyopitishwa na Chama kisa tu alihama kutoka Chadema,so sad.
 
Yaani kama vile Shilinde alivyopitishwa na Chama kisa tu alihama kutoka Chadema,so sad.
.
Ndio wewe ulitaka akatwe ili ubate Cha kuja kubwabwaja huku.
Ndo maana nikasema CCM Ni Chama Cha wananchi yeyote anaweza teuliwa kukiwakilisha Chama katika Uchaguzi ilimuradi tu awe na kadi ya CCM.

Achana na Ile soccos inayoongozwa na Wahuni Wachache tu kwa biti na vitisho vikali vya "SUMU HAIONJWI"
 
Naona Mangula yeye alionja Sumu mara akajikuta yuko muhimbili.
 
Kwani awamu yake huko AU haijaisha?

Hatutaki viongozi wa maisha, ndani ya nchi na Afrika nzima.

UBUNGE MIAKA MITANO YA JAMHURI NA MITANO YA AU HUKO INATOSHA!

Tuko milioni 60, Masele yeye ana ujuzi gani wa kipekee ambao wengine hawana?

Harvard my arse. Andrew Chenge went to Harvard to learn how to sell the country in mid-day robbery contracts as Attorney General.

Masele kule aliko AU kagombana nao!
Hapa ndani Spika kagombana nae.
Wizara Mambo ya Nje kagombana nao!

Hawezi diplomasia!
 
Kwani awamu yake huko AU haijaisha?

Hatutaki viongozi wa maisha, ndani ya nchi na Afrika nzima.

UBUNGE MIAKA 5 INATOSHA!

Tuko milioni 60, Masele yeye ana ujuzi gani wa kipekee ambao wengine hawana?

Harvard my arse. Andrew Chenge went to Harvard to learn how to sell the country in robbery contracts as Attorney General.

Masele kule aliko AU Ikagombana nao!
Hapa ndani kagombana na Spika. Hawezi diplomasia!
Na wala shinyanga hakubaliki. Juzi baada ya jina la katambi kutangazwa ilikuwa km sherehe
 
Back
Top Bottom