Ccm ya leo ni "feki"haina sifa ya kuaminiwa haina uhusiano na ccm halisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm ya leo ni "feki"haina sifa ya kuaminiwa haina uhusiano na ccm halisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Japhari Shabani (RIP), Jun 23, 2011.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katika ulimwengu wa leo kumezuka tabia ya wajanja wachache kutumia majina au blend za makampuni makubwa ya kuheshimika au watu maarufu kwa manufaa yao.Kwa kuzalisha bidhaa feki au kutenda matendo yao ambayo hayaendani na sifa au malengo ya blend au mtu mashuhuri husika chini ya mwamvuli wa blend au umaarufu wa mtu fulani,HILI LIMETOKEA KWA CCM.Ndugu zanguni CCM ya leo ni FEKI sio CCM ya Mwalimu Nyerere.Mwalimu JK Nyerere na viongozi wa wakati ule walijenga CCM yenye maadili iliyokua na lengo lakumkomboa Mtanzania kutoka katika ujinga,umasikini,maradhi,unyonyaji,ukandamizaji n.k.Juhudi zote na rasilimali zote zilielekezwa huko na mafanikio yalionekana wazi maneno na matendo ya viongozi wa wakati ule yalifanana na hii ilijenga imani kwa wananchi na chama kuheshimiwa ndani na nje ya Tanzania viongozi wake waliwatumikia wananchi.

  CCM hiyo iliaminiwa na wananchi kuikabidhi CCM hiyo kwa moyo mmoja na uaminifu ridhaa ya uongozi.Mafidi walililiona hilo na kugundua bila kupitia CCM ufisadi wake hautafanikiwa,kwani ilikua vigumu kuwalaghai Watanzani kutoka nje ya CCM ambayo iliku tayari blend yenye sifa na kuaminiwa.Hivyo basi walichokifanya nikujipenyeza katika chama kwa mbinu zozote zinazowezekana na kuanza kukiteka chama mpaka katika ngazi za juu za uongozi taratibu walmekigeuza chama mpaka kinavyoonekana sasa.CCM ya leo ni "FEKI"limebaki jina,bendera na sare.CCM ya sasa ni ya mafisadi ambayo ipo kwa ajili ya kulinda masilahi ya mafisdi ambapo masilhi namba moja ni kuwanyonya walalahoi na kujinufaisha mafisadi na kufanya kila njia kuhakikisha wanabaki madarakani milele chini ya kivuli cha CCM.Naimani baada ya kuondolewa madarakani ndiyo utakuwa mwisho wa Chama chenyewe.Mali zote za CCM ambazo kimsingi ni za walalahoi watanzania wote-KAMA ZIPO-Kwani nyingi zinaendeshwa chini ya CCM lakini fedha zinaenda mifukoni mwa mafisadi hatutaziona.Nina mashaka ata ya kuwepo kwa kumbukumbu za mali za CCM kwa sababu kila fisadi anamega anavyotaka.
  WATANZANIA HATUNA SABABU YA KUIAMINI CCM YA LEO NI CCM FEKI HAMKENI SI SWARI TENA WAKATI WA UKOMBOZI UMEFIKA.MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 2. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 488
  Trophy Points: 180
  Very nice analysis.Ukweli mtupu!
   
Loading...