CCM ya Jana,CHADEMA ya leo,kesho na Mabadiliko ya kisiasa Tanzania

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Wakati tunaelekea kufanya mabadiliko makubwa ya kisiasa katika Taifa letu la Tanzania hebu tutafakari maneno haya ya Hayati Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere na tuangalie relevance za maandishi haya katika political environment ya sasa:


  1. "Uongozi wa vitisho si uongozi, na uongozi wa namna hiyo utaendelea kwa muda mfupi tu. Wananchi wanapoonyesha makosa ya maamuzi ya kipumbavu wanatumia haki yao ya uraia…tunachotaka kuzuia ni ufidhuli, ubovu, na uzembe wa baadhi ya viongozi " ("AZIMIO LA ARUSHA BAADA YA MIAKA KUMI" ukurasa wa 47 na 49)
  2. "Tungekubali kuwa waoga na wazembe wakati wa kupambana na mkoloni, leo tusingekuwa tunajitawala. Tukianza woga na uzembe hatutaweza kujenga na kudumisha demokrasia nchini mwetu" (Hotuba yake ya Arusha tarehe 5 Februari 1977)
  3. …."Haisaidii mtu yoyote kujidai kwamba mambo yalivyo sivyo ……."na hasa….kama mambo ni mabaya hayatoweki kwa sababu tunajidai hayapo…" ("After Arusha Declaration" p.8 )(Tafsiri)
  4. "Lazima uwepo … utekelezaji wa siasa kwa akili kufuatana na mazingira, mahitaji ya nchi na nyakati zilivyo. Hakuna jibu moja ambalo linaweza kutumika nyakati zote na mahali pote. Kila nchi na kila kizazi lazima kizingatie matatizo yake kwa mipango yake yenyewe ikitumia kwa ufanisi mkubwa zile nafasi zinazopatikana katika mazingira yake" (Karamu rasmi aliyomfanyia Waziri Mkuu Chou Enlai 4.5.1965)(Tafsiri)





ANGALIZO:
Nilituma uzi huu kwa title nyingine iliyokuwa na kichwa cha habari "Mwalimu Nyerere na maamuzi ya kipumbavu,Uoga na Uzembe" mods mkaifuta without reading the content hivyo nimetoa fursa nyingine kutafakari maandishi haya ya Mwalimu.
 
Mkubwa! Hizo nukuu si mchezo kabisa.zinahukumu serikali iliyopo madarakani na zinailenga hali iliyopo ya sasa kuhusu muungano na siasa kwa ujumla.Ni ushauri wangu JK akae chini aya tafakaria haya kwa kina kisha achague kusuka ama kunyoa
 
Ccm badala ya kuzifanyia kazi hizo nukuu za Nyerere wanaziweka makumbusho wanasubiri kuazimisha kumbukumbu ya kifo chake wanaziweka kwenye redio siku hiyo tuu
 
kilichobaki naona ni sisi wananchi kuzifanyia kazi na si nyingine bali kuwang'oa madarakan hawa mafidhuli 4 real tumechoka na ufidhuli wao uliokemewa tangu kale............vijana twende kazini mpaka kieleweke
 
Back
Top Bottom