CCM ya biashara ya utumwa

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
129
Ansbert Ngurumo

“NINAJITOA CCM kwa kuwa msingi wa mimi kujiunga na chama hicho ulikuwa ni ajira na si sera wala itikadi, kwa kuwa wamekiuka makubaliano yetu nimeamua kujitoa rasmi, sharti letu lilikuwa ajira nono na huo ndio ukweli ambao sekretarieti ya CCM inautambua.”

Hii ni kauli iliyotolewa wiki hii na msanii wa muziki wa Kiafrika, Fulgence Mapunda (Mwana Cotide), akieleza hatua yake ya kujiengua kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ni mmoja wa ‘maelfu’ ya wanachama wapya waliojiunga na CCM kwa mbwembwe katika mwaka uliopita.

Ni tunda mojawapo la jitihada za Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, katika kuongeza idadi ya wanachama na kuimarisha chama.

Mapunda alikuwa mmoja wa mavuno ya CCM; bidhaa iliyonunuliwa kutoka upande mwingine ili kudhoofisha upinzani na kuijenga CCM.

Ni ushahidi mwingine kwamba CCM imekuwa ‘inawanunua’ wanachama kwa pesa na ahadi nono, ingawa mara kadhaa imeambiwa hivyo, na imekana.

CCM imekuwa inatumia shida za watu kujinufaisha kisiasa. Wakati mwingine, ni vema kusema kwamba imekuwa inasababisha hali duni ya maisha ya wananchi, ili iyatumie hayo hayo kuwanunua.

Huyo ni mmoja. Amekuwa jasiri na kusema walichokubaliana. Huyo ni mmoja, hakutekelezewa ahadi yake. Amerejea ‘uraiani’.

Wapo wengi wa aina hiyo ndani ya CCM, walionunuliwa kwa ahadi nono, lakini hazijatekelezwa. Wamo waliotekelezewa kiasi, lakini bado wananung’unika chini chini.

Tukitaka tunaweza kuwataja hapa. Kwa kuwa ni wengi, tutawataja wale wanaosikika wakilalamika mara kwa mara juu ya ‘kutotendewa haki’ na CCM. Vyovyote jamii inavyowaona, nao tutawatetea, wapewe haki zao.

Wamo kina Tambwe Hizza, Thomas Ngawaiya na Shaibu Akwilombe.

Katika kundi la kina Mapunda, yumo pia Amani Kabourou. Wamo mamia ya walalahoi wa Tanga na Kigoma na kwingineko, walioitikia wito wa Makamba.

Tofauti ya Kabourou na Mapunda ni moja. Kabourou aliwabana mapema, akapewa alichotaka.

Kinachowaunganisha wote hawa, kama alivyosema Mapunda ni njaa. Urafiki wao wa ghafla na CCM haukujengwa katika sera wala itikadi.

Mioyo yao haiko na CCM. Akili zao haziko na CCM. Uhusiano wao na CCM umejengwa katika tumbo.

Maana yake nini? Watu wa namna hii si msaada kwa CCM. Wana haki ya kuwa popote wanapotaka, wakati wowote; lakini haituzuii kusema kwamba wanatangatanga. Na kwa kuwa mioyo na akili zao havimo ndani ya CCM, viko pengine.

Sasa tumuulize Makamba. Kama hii ndiyo mbinu yake ya kuongoza chama, anadhani CCM ina muda gani kabla ya kuangushwa na wale wale walio ndani yake?

Makamba anaweza kuwaeleza wana CCM kwa nini anatumia pesa nyingi za chama kupandikiza wapinzani wa chama chao miongoni mwao?

Wana CCM wana haki ya kuhoji matumizi ya pesa za chama katika ununuzi wa wanachama bandia, wakati wamo wanachama halali na waaminifu wa muda mrefu wanaendelea kusota, lakini wanaendelea kukitetea chama chao.
Wamuulize Makamba, kwa mfano, inawezekanaje watumishi wa CCM walipwe mshahara wa sh 30,000 kwa mwezi, huku chama kikiwa tayari kumlipa ‘mamluki’ mmoja sh 300,000 kwa mwezi?

Inawezekana Makamba haoni kwamba sh 300,000 ni nyingi, kwa kuwa kiasi hicho wala hakitoshi kwa gharama ya vocha za simu yake kwa wiki moja!

Hakitoshi kwa mafuta ya gari lake kwa mwezi! Kiasi hicho hicho ni kidogo ya kile anachojilipa kwa siku moja kama masurufu ya safari anapokuwa nje.
Anajua si nyingi kwa kuwa CCM inapata takriban shilingi bilioni moja kutoka serikalini kama ruzuku kila mwezi. CCM ina miradi mingi nchi nzima, vikiwamo viwanja vyetu vya michezo ambavyo imeshindwa kuviendesha.

Hakika, kama kuna chama kinapaswa kuwa tajiri ni CCM. Lakini kimeshindwa kutawala miradi yake, ukiwamo mradi mkuu wa Shirika la Uchumi na Kilimo Tanzania (SUKITA).

Anapokuwa anawanunua kina Mapunda, Makamba anajiona mjanja. Lakini lipo jambo moja la dhahiri.

Ununuzi huu wa wanachama ni ishara kwamba CCM inakufa. Nguvu yake sasa imebaki katika pesa na hadaa.

Sasa ona, hata huyu walimuahidi masilahi manono, wameshindwa kumtimizia! Na ni wale wale wanaojitapa kuwa chama chao kinatimiza ahadi zake kwa wananchi milioni 40!

Laiti Watanzania milioni 40 wangekuwa jasiri kama Mapunda huyu, yangesemwa mengi, na ungekuwa mwanzo mpya wa siasa za Tanzania.
Vile vile, huu ni ushahidi mwingine wa tuhuma dhidi ya CCM kuhusu ununuzi wa kura wakati wa uchaguzi ili wapate ushindi wa kishindo!

Bahati mbaya ni kwamba, baadhi ya hawa wanaonunuliwa hawasemi hadi yanapowakuta mambo kama haya yaliyomkuta msanii Mapunda.
Kwa muda sasa, na hili limekuwa zaidi katika Serikali ya Awamu ya Nne, pesa imekuwa ndiyo sera na itikadi ya CCM.

Nguvu pekee waliyobaki nayo ni pesa. Wanakoitoa wanajua wenyewe. Na ndiyo maana yalipoibuka mambo ya ufisadi Benki Kuu ya Tanzania, yakihusisha pia makampuni hewa yaliyoundwa na kuchota pesa kipindi cha uchaguzi, halafu yakafutwa usajili mara tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2005, wenye akili walijua kwa nini tangu awali serikali ilikataa Bunge kuunda tume huru ya kuchunguza ubadhirifu huo.

Sasa wamechunguza moja ya kumi ya ubadhirifu wa Benki Kuu, na tayari gavana amefukuzwa kazi.

Kama wangechunguza ubadhirifu mzima, si ajabu hata serikali ingepinduliwa! Na hili ndilo waliloogopa, kwani walijua nani anahusika wapi, hata kabla ya wapinzani kutangaza hadharani tuhuma zao.

Nasema sera na itikadi ya CCM (na serikali sasa) ni pesa. Ndiyo hiyo inayotembezwa kila kona, si kununua tu wanachama, bali hata watu wenye taaluma zinazoweza kutumika vema kuijengea CCM sifa nzuri mbele ya umma.

CCM mnakazania kutufundisha siasa za kununiana na kuuzana. Inatufundisha ufisadi. Imeacha kuwafundisha wanachama wake siasa, imeacha sera na itikadi. Sasa inawafundisha ufisadi!

Haya yanaturejesha kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, hayati Horace Kolimba, na mmoja wa wanachama wa muda mrefu wa chama hicho, Joseph Butiku.
Miaka zaidi ya 10 iliyopita Kolimba alisema CCM imepoteza dira na mwelekeo. Kuna kitu alikiona. Kabla hajawasaidia kukirekebisha chama chao, wakamweka kiti moto, akapoteza uhai.

Mwaka jana, mzee Butiku ameibuka na kurejea kauli ile ile ya Kolimba. Akasisitiza kwamba CCM imepoteza mwelekeo. Wakambeza, lakini wakaogopa kumchukulia hatua.

Tunao mashahidi wengi walio hai, ndani na nje ya CCM wanaoyasema haya. Hatuwezi kuwapuuza. Hata hatua na kauli hii ya Mapunda, vinaingizwa katika kumbukumbu.

Pole pole, tutaanza kukubaliana kwamba CCM ya Jakaya Kikwete na Yusuf Makamba ni CCM ya ufisadi. Tafuta tafsiri yoyote ya ufisadi. Huu ununuzi na uuzaji wa binadamu wenzetu ni ufisadi wa viwango vyake.

Ni mbinu mpya ya kuwatumia binadamu wenzao. Ni udhalilishaji na utumwa! Na ipo siku Makamba na wenzake watatueleza kwa nini wanaendeleza ‘biashara ya utumwa’ katika siasa za Tanzania.

+447828696142
ansbertn@yahoo.com
www.ngurumo.blogspot.com

Source: Tanzania Daima
 
Sokomoko,
Hao wanaonunuliwa toka ktk vyama vingine kwenda ccm, wote hawa ni wasaliti, hawafai ktk jamii, leo Dr. Kabulu anatamani kurudi CHADEMA ila mlango umefungwa,

Naomba ujue, hatima ya ccm iko mikononi mwetu kwa sasa, watanzania tumeleewa yote wanayotuhadaha.

Sasa tunakuomba hapo ughaibuni,waambie watanzania wenzako mrudi hapa home tufanye mapinduzi kwa kutumia kura yetu 2010, tuache kulalama huku ccm wakitufanya majuha.

Ndugu zangu mtu hapigani vita akiwa njee ya nyumba yake, na pia ukimfukuza mwizi kimyakimya lazima atapagawa,ccm kweli wajipange vema 2010.

Watanzania wa leo sio wa 2005, ccm ilishinda kwa sababu za kumuamini JK, Watanzania walimuamini kutokana na ile sera yake ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA na pia alikuwa kipenzi cha watanzania.
 
Huyu ni wa kumuangalia sana maana ni msaliti, anaweza kuuza chama kwa njaa yake, chama kitakacho mpokea kiwe makini sana.
 
Kwa kweli Ngurumo anafanya kazi kubwa sana! Ni waandishi wangapi amabo wameamua kubaka taalumayao,na pamoja na wimbi lote la ufisadi bado wanambeba Chenge,RA,Lowasa,Mramba nk?

Kwa kutumia kalamu yake,naweza kumuona Kenny sara wiwa nakiwa hai.Huyu ni muandishi mkongwe aliyepambana na utawala wa dikteta Sani Abacha Kule Nigeria kwa kutumia kalamu yake.

Ngurumo Mungu akupe Nguvu sana ndugu
 
2071edz.gif
 
Kazi nzuri sana Ngurumo .... Tanzania bado haijaishiwa vichwa bora...... Asante sana!
 
mimi nashindwa kumuelewa mtu aliyehamia kwenye chama kwa ajili ya masilahi binafsi na si kwa mvuto wa sera zake.

mtu wa namna hii ni wa kumuogopa na kutoka kwake hadharani na kueleza yaliyompeleka ccm hakujamfanya aonekane hero kwangu.
 
Sokomoko,
Hao wanaonunuliwa toka ktk vyama vingine kwenda ccm, wote hawa ni wasaliti, hawafai ktk jamii, leo Dr. Kabulu anatamani kurudi CHADEMA ila mlango umefungwa,

Naomba ujue, hatima ya ccm iko mikononi mwetu kwa sasa, watanzania tumeleewa yote wanayotuhadaha.

Sasa tunakuomba hapo ughaibuni,waambie watanzania wenzako mrudi hapa home tufanye mapinduzi kwa kutumia kura yetu 2010, tuache kulalama huku ccm wakitufanya majuha.

Ndugu zangu mtu hapigani vita akiwa njee ya nyumba yake, na pia ukimfukuza mwizi kimyakimya lazima atapagawa,ccm kweli wajipange vema 2010.

Watanzania wa leo sio wa 2005, ccm ilishinda kwa sababu za kumuamini JK, Watanzania walimuamini kutokana na ile sera yake ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA na pia alikuwa kipenzi cha watanzania.

Tunakusubiri wewe.
 
Back
Top Bottom