CCM wenye GUBU mwacheni Mhe Rais afanye kazi yake.Dhihaka hazijengi, na atawapuuza.

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Salaam za Eid El Fitri!

Ndugu zangu wanaccm hasa waliojawa na roho za chuki na Gubu nawaomba ujumbe huu uwafikie siku ya leo mpate kuelewa.
Acheni dhihaka zenu za reja reja kwenye mamlaka inayotambuliwa na katiba ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania, hizi Gubu,chuki na roho mbaya zenu ni kelele za chira bwawani hazizuii ng'ombe kunywa maji.Mlie mcheke, mlale muamke lakini Rais wa JMT ni Mhe Samia Suluhu Hassan, Kama mna wasi wasi nae hameni nchi mkatafute wa kwenu.

Imeshaanza kujitokeza vitabia vya kijinga na kipuuzi kila wakati Mhe Rais akitenda au hata kusema jambo lolote ambalo lina maslahi kwa taifa na lenye kuleta umoja, kuna watu wanaumia wakihisi labda mama anabomoa ya mtangulizi wake, hizi ni roho mbaya na mwisho wake ni umauti tu hakuna kiingine. Kamwe Samia na Hayati wanatofautiana katika maumbile na hata kifikra, wanaunganishwa na Ilani ya chama wanayotekeleza lakini kila mmoja anatekeleza kwa njia na ubunifu wake tofauti.Hata makuzi yao ya kifamilia ni tofauti.

Ni ujinga na ni dhihaka kusema eti Mhe Rais anachukua kelele za mitandaoni na kuzifanyia kazi, ulisikia wapi? Kwani hakuna taratibu za uwajibikaji kwa misingi ya kiuongozi? Kuna informers wangapi wa Ofisi ya Rais kila mahali? Mnataka kusema ninyi wachache ndio mnajua nchi hii kuliko mkuu wa nchi. Acheni Gubu na ubinafsi, acheni mazoea yasiyokuwa na maana.

Hili la kusema ati ni vibaya Rais kukaa kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya siasa nchini au kuamua kutumia watanzania wenye uwezo bila kujali itikadi zao ni ubinafsi, husda,chuki na gubu analotembea nalo Ibilisi. Nchi yetu sote, kuishi katika umoja na kuijenga pamoja inakuuma kitu gani? Unapenda kuona siku moja nchi inaingia katika sintofahamu kwa sababu watu wachache kuendekeza uchu wa madaraka, chuki na ubinafsi?

Cha kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ukubwa wake ni kwamba tuna Rais Mchamungu practically no siyo wa maneno tu. Tuna Rais aliyejaa haki na hofu ya Mungu kwa vitendo, kwahiyo sisi wazalendo tutazidi kusimama naye na kumuombea siku zote za utawala wake. Ninyi wenye roho za choyo na Gubu mtaki nazo hivyo hivyo na kamwe dau la kuku halimpati mwewe.

Ninawaaga kwa kina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Kazi iendelee!
Eid Mubarak!
 
Wala usihangaike na hiki kikundi cha wachumia tumbo wenye hofu ya kupoteza kila kitu pale nchi itakapooendeshwa kwa misingi ya haki.
Kamwe hatutakubali kuona wapuuzi nna walafi wachache wakiendelea kumshambulia kiongozi ambaye amesimama katika haki. Wakiinuka tunainuka wote, wakikaa tunalikalisha wote, wakiliamsha dude tunawahi kuliamsha.
 
Salaam za Eid El Fitri!

Ndugu zangu wanaccm hasa waliojawa na roho za chuki na Gubu nawaomba ujumbe huu uwafikie siku ya leo mpate kuelewa.
Acheni dhihaka zenu za reja reja kwenye mamlaka inayotambuliwa na katiba ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania, hizi Gubu,chuki na roho mbaya zenu ni kelele za chira bwawani hazizuii ng'ombe kunywa maji.Mlie mcheke, mlale muamke lakini Rais wa JMT ni Mhe Samia Suluhu Hassan, Kama mna wasi wasi nae hameni nchi mkatafute wa kwenu.

Imeshaanza kujitokeza vitabia vya kijinga na kipuuzi kila wakati Mhe Rais akitenda au hata kusema jambo lolote ambalo lina maslahi kwa taifa na lenye kuleta umoja, kuna watu wanaumia wakihisi labda mama anabomoa ya mtangulizi wake, hizi ni roho mbaya na mwisho wake ni umauti tu hakuna kiingine. Kamwe Samia na Hayati wanatofautiana katika maumbile na hata kifikra, wanaunganishwa na Ilani ya chama wanayotekeleza lakini kila mmoja anatekeleza kwa njia na ubunifu wake tofauti.Hata makuzi yao ya kifamilia ni tofauti.

Ni ujinga na ni dhihaka kusema eti Mhe Rais anachukua kelele za mitandaoni na kuzifanyia kazi, ulisikia wapi? Kwani hakuna taratibu za uwajibikaji kwa misingi ya kiuongozi? Kuna informers wangapi wa Ofisi ya Rais kila mahali? Mnataka kusema ninyi wachache ndio mnajua nchi hii kuliko mkuu wa nchi. Acheni Gubu na ubinafsi, acheni mazoea yasiyokuwa na maana.

Hili la kusema ati ni vibaya Rais kukaa kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya siasa nchini au kuamua kutumia watanzania wenye uwezo bila kujali itikadi zao ni ubinafsi, husda,chuki na gubu analotembea nalo Ibilisi. Nchi yetu sote, kuishi katika umoja na kuijenga pamoja inakuuma kitu gani? Unapenda kuona siku moja nchi inaingia katika sintofahamu kwa sababu watu wachache kuendekeza uchu wa madaraka, chuki na ubinafsi?

Cha kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ukubwa wake ni kwamba tuna Rais Mchamungu practically no siyo wa maneno tu. Tuna Rais aliyejaa haki na hofu ya Mungu kwa vitendo, kwahiyo sisi wazalendo tutazidi kusimama naye na kumuombea siku zote za utawala wake. Ninyi wenye roho za choyo na Gubu mtaki nazo hivyo hivyo na kamwe dau la kuku halimpati mwewe.

Ninawaaga kwa kina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Kazi iendelee!
Eid Mubarak!
Hawa wajinga unafikiri ni wengi basi? Makundi cha roho mbaya japo kidogo hakatusumbui sisi Watanzania million 60
 
Back
Top Bottom