CCM Wazipiga kavu kavu-kisa Ngawaiya kuomba kitu kidogo-pilika pilika za uchaguzi

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Kampeni za uchaguzi wa mwenyekiti wa jumuhia ya wazazi ya CCM Taifa jana zilihitimishwa kwa masumbwi baada ya kuhibuka vurugu kwenye baa ya chako ni chako na kusababisha baadhi ya watu kujeruhiwa vibaya na magari ya wagombea kuvunjwa vioo.Uchaguzi huo ,ambao umehairishwa karibu mara tatu,unafanyika leo kwenye ukumbi wa jengo la makao makuu ya chama hicho
vurugu zilitokea baada yaThomas Ngawahiya mwenyekiti wa wazazi mkoa wa kilimanjaro (Ngawahiya amaye aliwahi kuwa mbunge kupitia chama cha TLP) kuombaa apewe angalahu kitu kidogo (rushwa ya bia na kuku wa kuchoma ) ili abadili msimamo wake wa awali wa kumuhunga mkono mzee mhina,kahuli hiyo ilimuhudhi kada maarufu wa CCM Emanuel Nzungu ambaye ni mwenyekiti wa wazazi,Nzungu alisikika akisema ""wewe Ngawahiya tumekukaribisha tu,hivyo hutakiwi kuomba rushwa unakidhalilisha chama chetu,Tafadhali ishia hapo, Nzungu aliendelea kumshishia madongo '''Tuachie chama chetu sisi tunakipenda na tuna uchungu kuona unakidhalilisha kwa kuomba bia na kuku
 
- Haya ya wazazi yapo tu si najua Muungwana alisema hakitaki hiki chama cha wazazi maaana ni mzigo kwa taifa na CCM in general kumbe bado wapo?

Respect.

FMEs!
 
Juzi nimeambiwa hao wagombea walipeleka magari kuwabeba wajumbe toka Mwanza, je hizo pesa wanatoa wapi? Inaelekea CCM wameshindwa kabisa kukabiliana na hili tatizo la rushwa kwenye chaguzi zao.

Hata 2010 rushwa itatawala tu kila sehemu. Mtu atapelekaje magari kwenda kufuata wajumbe? Si ajabu hao wajumbe wamefichwa sehemu wakilishwa na kunyweshwa.
 
Tatizo kubwa hapa ni watu kutokuwa na uelewa wa uchaguzi sasa huyo Ngawaiya mbona anajidhalilisha sana! yaani bia na kuku tu!
 
Its unfortunate, ila tunashukuru pumba zinaonekana mapemaa!!! Ngawaiya ni prositute wa siasa tu!! Tusipoangalia kuna siku atahamaia chadema, msimkaribishe huyo kicheche was siasa
 
Nadhani Ngawaia alikuwa anafanya matani kwa CCM, kwani hilo ni la kushangaza kwenye kampeni za hicho chama? Watu waache utani Bwana, hata huyo aliyekurupuka na kudai aachiwe chama chake huo ni usanii tu!
 
Rushwa ndani ya CCM imeasisiwa, kulelewa na kutokemewa na haohao wana CCM tunaowafahamu.Ngawaiya kuomba rushwa kuna ubaya gani wakati fedha inatembea?
CCM inajiua yenyewe , tena pole pole.Yaliyokuwa yafikiriwa ni mambo ya aibu sasa yanafanyika wazi wazi.
Kutokemea rushwa zile kubwa iliyofanywa na vigogo wa chama ndio kinachoelekea kukimaliza chama hiki kikongwe.Kwa upande mmoja wa shilingi,viongozi waandamizi wa CCM wanapogwaya kuwachukulia hatua wenzao ambao umma umedhihiri kuwa ni vinara wa wizi, ubadhirifu na vikongwe wa rushwa.Upande wa pili ni viongozi ha hao kukosa ujasiri wa kuwa kemea wale wadogo kwa vile hawakufanya hivyo kwa wakubwa.
Picha nyingine ni kwa wala rushwa wadogo kupata ujasiri wa kuendelea na rushwa kubwa kubwa kwa vile wanajua kuwa hawatakemewa/kuchukuliwa hatua zozote za maana.
Haya ni mambo ambayo wananchi wame yapigia saana kelele katika vyombo mbali mbali.
Sasa yameanza kujikita katika vikao vizito vya chama.
 
We acha tu...tuna msururu wa watu wenye kiu na njaa badala ya viongozi.
 
- Haya ya wazazi yapo tu si najua Muungwana alisema hakitaki hiki chama cha wazazi maaana ni mzigo kwa taifa na CCM in general kumbe bado wapo?

Respect.

FMEs!
Muungwana alikuwa haitaki kabisa jumuiya ya wazazi kwani ni jumuiya pekee iliyompinga katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa kugombea urais!! Ndio maana baada ya kuukwaa ukulu muungwana akahakikisha kuwa Aliyekuwa M/kiti wa wazazi wakati huo Malegesi, anashuhulikiwa kikamilifu na kuachia ngazi; huyo ndio Kikwete fundi wa kulipiza visasi!!
 
Vurugu hizi zinasomeka tu katika matukio kwa waliohusika wachache. lakini ndani yake kuna wakubwa ambao wana;linda maslahi yao makubwa.

Watanzania tunachekelea vurugu hizi zinazotokana na mzaha wa kuombana bia. Lakini ninawahakikishia kuwa gharama yote ya kutawaliwa na mapoyoyo wanaotokana na mchakato huo mchafu na wenye upofu mwingi ni yetu sote. Kila mmoja wetu atalipa kwa kutawaliwa na mapoyoyo hayo.

Hata hivyo ninawahakikishia kuwa CCM haiwezi kufanya uchaguzi wowote wa ndani ama wakigombea dhidi ya vyama vingine bila ya masumbwi.
HIKI NI CHAMA CHA DAMU
 
Nzungu alisikika akisema ""wewe Ngawahiya tumekukaribisha tu,hivyo hutakiwi kuomba rushwa unakidhalilisha chama chetu,Tafadhali ishia hapo, Nzungu aliendelea kumshishia madongo '''Tuachie chama chetu sisi tunakipenda na tuna uchungu kuona unakidhalilisha kwa kuomba bia na kuku


Jamaa kweli kavamia maana hata wao wanamshangaa kuomba rushwa ndogo kiasi hicho wakati wenzie wameshazoea ma EPA, RICHMOND... CCM mchezo!!!!
 
Nadhani wakati umefika CCM kuangalia upya kama ni lazima kuwa na jumuia kama hizi. I can understand, youth wing, women empowerment etc but jumuia ya wazazi?? pheww?? hilo naona limepitwa na wakati. Ni vichaka vya mafisi (mafisadi). Labda waanzishe jumuia ya walemavu au jumuia ya wapinga ufisadi (yes will work by fighting from within) etc.
 
Back
Top Bottom