CCM Wazalendo tuandamane Rais Ramaphosa arudishe zawadi zetu!

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,215
Ni majuzi tuu Rais wa SA alikuja kwa ziara ya siku mbili kabla ya mkutano wa SADC na katika ziara hiyo tulimpa zawadi nyingi yeye na mkewe.

Hatukuishia hapo tulimpa vitabu vingi vya kujifunza kiswahili kumbe anatusanifu tuu sio ndugu yetu.Nawashauri wana CCM "wenzangu"

tuandamane kudai zawadi zetu maana haiwezekani aone ndege yetu "HapaKaziTuu" inakamatwa kwa amri ya mahakama yeye kimya tuu kama vile yeye na Mtukufu Rais wetu sio "marafiki"!

Hajui kwamba ingekuwa huku pamoja na mahakama kuzuia wa kwetu angeamuru ndege iondoke?

Mbona mahakama iliwahi kuzuia nyumba zisibomolewe Kimara akasema "bomoa" pamoja na zuio la mahakama? Ndio, kwani Kimara sii hawakumpa kura kama wa Mwanza?

Ramaphosa kashindwa nini wakati alisema hapa TZ ni marafiki zangu?

Tuandamane bwana! Kwanza polisi hawawezi kutuzuia kama wote tutavaa mashati yetu ya kijani na mabango ya kumsifu mzee wetu.

Jee tuanzie wapi maandamano yetu?
Wale wanaotumiwa na mabeberu wasichafue adhima yetu hii, ambayo watu mashuhuri tutawaalika. Atakuwepo Dr Slaa na rafiki yake wa siku hizi Musiba, Polepole, Wabunge kama Lusinde, Nkamia, Musukuma na Mlinga kwa kutaja wachache.
 
Kweli kabisa
IMG_0544.JPG
 
unafikiri mahakama za wenzetu ni kama zetu?,acha umbugila ccm inavyohodhi mihimili mengine ya dola unafikiri na south africa ndio hivyo hivyo.Ni sawa na wewe umbake mke wa rafiki yako kisha utake huyo rafikiyo akukutetee
 
Ni majuzi tuu Rais wa SA alikuja kwa ziara ya siku mbili kabla ya mkutano wa SADC na katika ziara hiyo tulimpa zawadi nyingi yeye na mkewe. Hatukuishia hapo tulimpa vitabu vingi vya kujifunza kiswahili kumbe anatusanifu tuu sio ndugu yetu.
Nawashauri wana CCM "wenzangu" tuandamane kudai zawadi zetu maana haiwezekani aone ndege yetu "HapaKaziTuu" inakamatwa kwa amri ya mahakama yeye kimya tuu kama vile yeye na Mtukufu Rais wetu sio "marafiki"!
Hajui kwamba ingekuwa huku pamoja na mahakama kuzuia wa kwetu angeamuru ndege iondoke? Mbona mahakama iliwahi kuzuia nyumba zisibomolewe Kimara akasema "bomoa" pamoja na zuio la mahakama? Ndio, kwani Kimara sii hawakumpa kura kama wa Mwanza? Ramaphosa kashindwa nini wakati alisema hapa TZ ni marafiki zangu?
Tuandamane bwana! Kwanza polisi hawawezi kutuzuia kama wote tutavaa mashati yetu ya kijani na mabango ya kumsifu mzee wetu.
Jee tuanzie wapi maandamano yetu?
Wale wanaotumiwa na mabeberu wasichafue adhima yetu hii, ambayo watu mashuhuri tutawaalika. Atakuwepo Dr Slaa na rafiki yake wa siku hizi Musiba, Polepole, Wabunge kama Lusinde, Nkamia, Musukuma na Mlinga kwa kutaja wachache.
wazo zuri. tulifanyie kazi fasta!
 
Yani wewe sasa umeandika nini?
Imekamatwa kwa amri ya mahakama, rais anahusika vipi? Au hauelewi maana ya mihimili mitatu ya nchi?
Rudi shule, lasivyo ni bora wakunyonge tu utaishia kumlaumu Rais wa SA bila sababu yoyote.
Labda kama kuna unachomaanisha.
 
Wewe! Subiri tamko Kali la Polepole kiboko ya "mabeberu" ndio utaelewa huu mchezo! Chezea CCM wewe!
 
Hahahahahahahaha Chakaza mbavu zangu mm😂😂 niliwashangaa mmeweka waru foleni moro eti mnaenda mwonesha makaburi . hahahaa hao sio marafiki zetu ..hha maana kule wanatuua hovyo alafu huku mnajigonga kuwa ni marafiki wa kweli!hehhee MNALOOO
 
Usimlaumu sana mwenzio anajua mihimili hiyo mitatu yaweza kufanywa vyovyote na mtu mmoja kama ilivyo hapa nchini.HAPA NCHINI MHIMILI NI MMOJA TU
Yani wewe sasa umeandika nini?
Imekamatwa kwa amri ya mahakama, rais anahusika vipi? Au hauelewi maana ya mihimili mitatu ya nchi?
Rudi shule, lasivyo ni bora wakunyonge tu utaishia kumlaumu Rais wa SA bila sababu yoyote.
Labda kama kuna unachomaanisha.
 
Ni majuzi tuu Rais wa SA alikuja kwa ziara ya siku mbili kabla ya mkutano wa SADC na katika ziara hiyo tulimpa zawadi nyingi yeye na mkewe.

Hatukuishia hapo tulimpa vitabu vingi vya kujifunza kiswahili kumbe anatusanifu tuu sio ndugu yetu.Nawashauri wana CCM "wenzangu"

tuandamane kudai zawadi zetu maana haiwezekani aone ndege yetu "HapaKaziTuu" inakamatwa kwa amri ya mahakama yeye kimya tuu kama vile yeye na Mtukufu Rais wetu sio "marafiki"!

Hajui kwamba ingekuwa huku pamoja na mahakama kuzuia wa kwetu angeamuru ndege iondoke?

Mbona mahakama iliwahi kuzuia nyumba zisibomolewe Kimara akasema "bomoa" pamoja na zuio la mahakama? Ndio, kwani Kimara sii hawakumpa kura kama wa Mwanza?

Ramaphosa kashindwa nini wakati alisema hapa TZ ni marafiki zangu?

Tuandamane bwana! Kwanza polisi hawawezi kutuzuia kama wote tutavaa mashati yetu ya kijani na mabango ya kumsifu mzee wetu.

Jee tuanzie wapi maandamano yetu?
Wale wanaotumiwa na mabeberu wasichafue adhima yetu hii, ambayo watu mashuhuri tutawaalika. Atakuwepo Dr Slaa na rafiki yake wa siku hizi Musiba, Polepole, Wabunge kama Lusinde, Nkamia, Musukuma na Mlinga kwa kutaja wachache.
Mii sio ccm ila naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom