CCM waweka mkakati kutumia UV-CCM kumng'oa Mbunge Ndesamburo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM waweka mkakati kutumia UV-CCM kumng'oa Mbunge Ndesamburo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ochu, Dec 9, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Na Ally Sonda, Moshi

  KATIKA hali inayoonekana kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekusudia kumng'oa Mbunge wa Moshi Mjini, Phillemon Ndesamburo (Chadema) ifikapo mwaka 2010, kimeamua kuutumia Umoja wa Vijana (UVCCM) katika kufanikisha ndoto hiyo.

  Ombi hilo la kuitaka UV-CCM itumike katika harakati hizo lilitolewa jana na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Profesa Jumanne Maghembe wakati akifungua mkutano mkuu wa umoja huo mkoani hapa na kusisitiza kuwa jimbo hilo kuendelea kushikiliwa na upinzani ni aibu kwa CCM na jumuiya zake, ikiwemo ya vijana.

  Bila kumtaja moja kwa moja Ndesamburo, Profesa Maghembe alisema CCM haina budi kuwatumia vijana wake mwaka 2010 ili kuing'oa Chadema, ambayo alidai inatamba kuwa haiwezi kung'olewa kwenye jimbo la Moshi Mjini.

  "Vijana nawaombeni sana hakikisheni mnakisaidia chama kukiondoa hiki kibabu kinachong'ang'ania hapa Moshi Mjini, lazima mwaka 2010 CCM ipate ushindi hapa Moshi mjini," alisema Profesa Maghembe bila kumtaja Ndesamburo.

  Akizungumzia uhai wa jumuiya ya vijana, Maghembe ambaye pia ni waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, aliwataka vijana kuwa wabunifu katika kuanzisha miradi ili waweze kujitegemea na kuacha tabia ya kuwa ombaomba.

  Aliwataka vijana watumie muda wao mwingi kufanya kazi za uzalishaji na vilevile kuwaeleza wananchi mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyopatikana ndani ya utawala wa serikali ya CCM, ikiwemo ubora wa elimu kwa kuongeza idadi ya shule na vyuo vikuu.

  "Vijana acheni tabia ya kukaa kimya wakati mnaona serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete inavyofanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo ya elimu, afya, mawasiliano, maji na michezo... lazima mfanye kazi ya kuwaeleza wananchi," alisema.

  Kuhusu suala la ufisadi, Profesa Maghembe aliwataka vijana kuisaidia serikali ya Rais Kikwete ili iendelee kuwanasa na kuwaburuza mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi, wakiwemo wale walioitia nchi hasara ya mamilioni ya fedha kwa kutoa misamaha ya kodi.

  "Vijana mna wajibu mkubwa wa kuisadia serikali kuwafichua mafisadi wote wa nchi hii ambao wanakwamisha maendeleo ya nchi, msaidieni Rais Kikwete ambaye hivi sasa ameamua kuwashughulikia mafisadi kweli kweli... vijana wa CCM fichueni ufisadi,"alisema.

  Mkutano huo mkuu wa uchaguzi ulihudhuriwa pia na mgombea uenyekiti wa UV-CCM Taifa, Hamad Yusuf Masauni kutoka Tanzania Visiwani ambaye alifika kujitambulisha kwa wajumbe wa mkutano huo na vilevile kuomba kura.
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  • Ni miongoni mwa Chami, Ngawaiya, Marealle
  MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro, Thomas Ngawaiya, anatuhumiwa kukigawa chama kwa kuunda makundi yenye mwelekeo wa kuwachafua wenzake, wanaodaiwa kutaka kuwania ubunge mwaka 2010 katika Jimbo la Moshi Vijijini.

  Wanaodaiwa kuchafuliwa na mtandao huo ni pamoja na Mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Dk. Cyril Chami, ambaye ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Manispaa ya Moshi, Aggrey Marealle.

  Habari zilizopatikana mwishoni mwa wiki kutoka ndani ya CCM zimedai kuwa Ngawaiya amekuwa akiwatumia baadhi ya waliokuwa wapiga debe wa Dk. Chami katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, kwa mikakati ya kuwamaliza wenzake kisiasa.

  Mbinu zilizodaiwa kutumiwa na kiongozi huyo wa wazazi ni pamoja na kubeza juhudi za kuleta maendeleo zilizofanywa na Dk. Chami jimboni mwake na kutamba kuwa yeye (Ngawaiya) alililetea jimbo hilo maendeleo makubwa alipokuwa mbunge kupitia Chama cha Labour (TLP) kuanzia mwaka 2000-2005.

  Ngawaiya na mawakala wake, pia wanadaiwa kukejeli misaada inayotolewa na Marealle kwa makundi mbalimbali ya jamii jimboni humo na kuwataka wanachama wa CCM kutowaunga mkono katika harakati zao za kutaka kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa 2010.

  Akizungumzia madai hayo, Dk. Chami, amekwisha kulalamikia vitendo anavyofanyiwa na Ngawaiya, hasa baada ya kuhusishwa na upotevu wa shehena ya saruji, iliyotolewa jimboni kwake na wafadhili.

  Akizungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki iliyopita, Dk. Chami alisema, wanaoendesha kampeni chafu dhidi yake ni wale wanaojiandaa kugombea jimbo hilo mwaka 2010.

  Alisema hofu ya wanaomchafua inatokana na wingi wa misaada anayoipeleka jimboni kwake, hali inayowapa wakati mgumu washindani wake, hasa namna ya kuwashawishi wananchi wawakubali.

  Kutokana tuhuma hizo dhidi ya Ngawaiya, uongozi wa CCM mkoani Kilimanjaro, umepanga kumhoji kupitia kamati ya maadili ya chama hicho.

  Mwenyekiti wa chama hicho wa mkoa, Vicky Nsilo Swai, alisema CCM, mkoani humo itamwita lakini hakuwa tayari kuweka wazi ni kikao kipi kitakachojadili suala la Ngawaiya.

  Akizungumzia tuhuma hizo, Ngawaiya kwa upande wake alisema anashangaa kusikia madai hayo kwani hajawahi kuzungumza na vyombo vya habari na hajui kwa namna gani anahusishwa kuwachafua wenzake.

  “Mimi sijui mambo haya yanatokea wapi, maana tangu Mrema alipokuja mjini hapa na kukutana nami ghafla kwenye moja ya migahawa, ndipo nilipoanza kuona taarifa za eti mimi nawachafua wenzangu.

  “Najiuliza, nawachafuaje, huo mtandao wangu unaundwa na kina nani na wako wapi wasijulikane? Hii yote ni hofu ya uchaguzi, maana kwanza nashangaa sijapata kutamka kama nagombea na hata nikiamua kufanya hivyo, ni haki yangu kikatiba ila sijasema,” alisema kwa kushangaa Ngawaiya.


  Source: Tanzania Daima
   
 3. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  CCM hapo ndipo mnaponichosha,Huyu Ngawaiya mnamjua tangu yuko NCCR MAGEUZI hadi TLP.Sasa mnamkaribisha humo ndani mnategemea nini hasa!Lazima akiparaganyue hicho chama kisha atafute upenyo mwingine.

  Ngawaiya aliianzia mbali,ni hodari wa migawanyiko na hatimaye hukimbilia mahakamani,Mtu huyu ni hatari sana hata kumfikiria kumwita Kiongozi. Ana siasa chafu, Ni mfanya biashara za magendo ya kutupwa.

  Tangu enzi ya bia za Kenya mkwepaji ushuru nambari one. Leo CCM mnamkumbatia tena kwa kumpa wadhifa wa Uenyekiti wa wazazi. Hakika mmepotoka,Wakati wowote jambo likishindikanika ndani ya chama yeye ni kutimka tuu.

  Muulizeni Lyatonga Mrema kwani alimjua fika lakini kwa kuwa mlimtumia kama ngao ya kujinga na Mrema basi ngao hiyo ni ya miiba mikali
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mimi najua tu Ngawaiya amezaa na dada mmoja wa Kichaga na kumfugulia Famasi na Stationary pale Magomeni karibu na Delux!

  Pia naskia kwa sasa anatembea na Lady JD

  Mchafuzi kweli wa wanawake!
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huyu JD naye kazidi jamani, si ameolewa na kijana mmoja hivi!
   
 6. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,272
  Likes Received: 4,256
  Trophy Points: 280
  Huyo Mareale amepania sana kugombea hilo jimbo na aliacha kazi TBL akarudi kujiandaa Moshi
   
 7. M

  Mpanda Merikebu Senior Member

  #7
  Feb 16, 2009
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 170
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa heshima na taadhima,

  Mzalendo Halisi, haya ya Ngawaiya kuzaa na dada wa kichagga na kisha kumfungulia biashara (Dar) au anatembea na Lady JD yanahusiana vipi na siasa za Kilimanjaro? Kwani na sisi tuna vitabia vyetu kama wanadamu ambavyo haviingiliani na shughuli zetu za kazi?
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Hafai tu Ngawaia ana tabia chafu!!!!

  Sasa nini hapo hauelewi?
   
 9. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  wote mafala tu hata huyu chami hana nyimbo mpyaa, sisi na chadema chadema na sisi

  chami na ngawaiyaa bye bye
   
 10. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Looh! msomi Dr. Chami na yeye kaingia kwenye genge lile lile, "MISAADA".

  Bila kuondoa mawazo finyu kama hayo tusitegemee maendeleo Tanzania.

  Kipaumbele cha kiongozi yeyote lazima kiwe kutumia resources zilizopo wilaya kusaidia kusukuma maendeleo mbele. Misaada iwe nyongeza tu na msingi mkubwa wa kuleta maendeleo utegemee watu wenyewe na utajiri wowote walio nao kama ardhi, mifugo, madini, maziwa nk.

  Inasikitisha sana!
   
 11. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,064
  Likes Received: 3,986
  Trophy Points: 280
  From DAILY NEWS Reporter in Moshi,
  16th July 2010


  THE race for Moshi Urban Parliamentary seat has gained momentum after a former Member of Parliament for Rombo constituency, Mr Justin Salakana, announced his intention to vie for the seat on CCM ticket.

  Announcing his intention, Mr Salakana said he has decided to challenge incumbent Member of Parliament Mr Philemon Ndesamburo ( Chadema), so that he could use his experience to speed up development in the area and bring people closer to the government.


  "The constituency has been under the opposition MPs for the last 15 years, causing the development processes within Moshi Urban to slow down. This is because the constituency has been lacking active representative," he said.


  He said the people of Moshi have been in a self-styled imprisonment as far as development was concerned and that if he is nominated by his party to vie for the seat, all that was happening would be history.


  As to why he was after Moshi Urban seat instead of Rombo which he represented between 1995-2000, Salakana said the government had implemented all that he was fighting for on behalf of 'wananchi' in Rombo.


  "When I was MP for Rombo, I used to challenge the government on development. The fourth phase government implemented all that I was fighting for on behalf of the people of Rombo," he noted.


  Salakana further said that as a result of successful implementation of development in Rombo, he had decided not to challenge his successor, Basil Mramba in the 2010 elections. A few years later he decided to cross back to the ruling party CCM.


  "Moshi Urban has been under opposition MPs for the past 15 years. I want to bring the badly needed development changes," he added.


  Mr Salakana became the first MP for Rombo under the multi-party system which was introduced in 1995, but later defected from Chadema to the ruling CCM.


  Daily News | Moshi Urban race for parliamentary seat hots up
   
 12. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,064
  Likes Received: 3,986
  Trophy Points: 280
  Patamu hapa, sijui itakuwaje na Ngawaiya naye? all the best !
   
 13. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #13
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Huu ni mkakati wa siku nyingi, swali ni JE WATAFANIKISHA??? Binafsi najua wanapoteza muda tu, lakini heri wajaribu na kujua kuwa ni maji marefu!
   
 14. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,064
  Likes Received: 3,986
  Trophy Points: 280
  lakini ikumbukwe Salakana ametokea Chadema so don't underestimate him na pia anashabihiana na Ndesa hata kwenye biashara wanazofanya zinafanana na wako wote hapo Moshi so kama network si haba! Tushuhudie
   
 15. U

  UncleSam Member

  #15
  Jul 17, 2010
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HAHA in there dreams i for one have been a resident of moshi all my life. and just to let CCM know Moshi peole don't give a damn about the blah blah y'all are good at!! we want a leader who is versertile and can effect change in the community. Ndesamburo can hold on to that seat for as long as he lives because he id that person.
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mvua huja baada ya wingu kutanda
   
 17. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,064
  Likes Received: 3,986
  Trophy Points: 280
  Marealle akataa kugombea ubunge

  MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Kamanda wa UVCCM Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Aggrey Marealle, amesema hatagombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

  Marealle ambaye pia ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Executive Solutions, aliyasema hayo juzi baada ya kutoka kumsindikiza Justin Salakana ambaye ni mkwe wake, kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na CCM katika kura za maoni ili agombee kiti cha Moshi Mjini.

  Salakana aliwahi kuwa Mbunge wa Rombo kuanzia mwaka 1995 hadi 2000 kwa tiketi ya Chadema, lakini baadaye akajiunga na CCM.

  Mwaka huu, ameamua kuwania kiti cha Moshi Mjini kwa tiketi ya CCM, na alisema wakati wa kutangaza nia kuwa hakuona haja ya kugombea tena Rombo kwa sababu serikali ilishatekeleza mambo yote aliyokuwa akipigania wakati wa Ubunge wake.

  Taarifa ya ofisi yake Dar es Salaam leo imesema, Marealle, kwa sasa hawezi kugombea kwa sababu ya majukumu ya kampuni hasa baada ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa Executive Solutions, Alan Turner kufariki dunia Februari mwaka huu.

  "Mimi na wanaCCM wenzangu tumefanya mengi kukiimarisha chama katika Mkoa wa Kilimanjaro na hususani Manispaa ya Moshi na msaada wangu mkubwa umetokana na Executive Solutions," alisema Marealle.

  Watu wengi walitabiri kuwa kamanda huyo wa UVCCM angegombea ubunge Moshi Mjini mwaka huu.

  Alisema iwapo Turner angekuwa hai, ingekuwa rahisi kwake kujikita kwenye masuala ya ubunge moja kwa moja huku Alan akiendesha kampuni.

  Alisema, licha ya shinikizo kubwa kugombea ubunge, anatambua kuwa CCM ni kama timu ya Taifa ya Hispania iliyoshinda Kombe la Dunia mwaka huu, kwani kina hazina kubwa ya wachezaji nyota na yeye atakuwa tayari kumuunga mkono mgombea atakayechaguliwa na CCM.

  "Nina imani kubwa kuwa CCM ikiungwa mkono na wananchi wa Moshi Mjini kwa kutumia nguvu ya Serikali ya chama tawala na si ya mtu binafsi, itaweza kuleta mapinduzi ya kiuchumi na maisha bora kwa jamii," alieleza Marealle.
  HabariLeo | Marealle akataa kugombea ubunge
   
Loading...