CCM watwangana ngumi mkutanoni Kyela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM watwangana ngumi mkutanoni Kyela

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Apr 20, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Na Mwandishi wetu.

  MTAFARUKU mkubwa umezuka ndani ya kikao cha Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kyela uliosababisha Polisi kuingilia kati na kumwokoa Katibu wa chama hicho wilaya, Bi. Maria Mwambanga.

  Polisi walichukua hatua hiyo baada ya, Bi. Mwambanga kupokea kipigo kutoka kwa wanachama hao waliomtuhumu kuwa ni kibaraka wa baadhi ya wanasiasa huku wajumbe wengine wakitwangana makonde wao kwa wao.

  Kikao hicho cha Kamati ya Maadili, kiliwaita makatibu kata wa chama hicho wa Kata za Kyela mjini, Kajunjumele, Makwale, Lusungo, Katumba Songwe, Itope na Diwani wa Kyela Mjini, Bw. Visk Mahenge wakidaiwa kuwa walimkashifu Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya

  Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti, Bw. Japhet Mwakasumi na Katibu wake Bi. Mwambanga, waliwaeleza makatibu hao na diwani kuhusu kumkashifu, Dkt. Mwakyembe na kuwataka waeleze sababu za kufanya hivyo na kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu.

  Kwa mujibu wa mmoja wa watuhumiwa hao, ugomvi uliibuka baada ya wao kuhoji hatua ya kuitwa peke yao bila pande zote zinazohusika kwenye mvutano huo.

  Baada ya suala hilo kuzua mtafaruku mkubwa, Polisi walifika eneo hilo la ofisi ya CCM wilaya kumwokoa Katibu huyo aliyekuwa akipokea kipigo, huku wajumbe wa kikao hicho wakisambaratika kila mtu na njia yake kwa hofu ya kukamatwa na Polisi.

  Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Bw. Japhet Mwakasumi alipotakiwa kuzungumzia sakata hilo alisema kwa muda huo akili yake ilikuwa haijatulia hadi hapo baadae.

  Naye Mwandishi Grace Michael anaripoti kuwa katika kile kinachoonesha kuwa hali si shwari katika majimbo mengi ndani ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani, Mbunge wa Ukonga Dkt. Makongoro Mahanga ameonya dhidi ya tabia ya wana CCM kuchafuana.

  Dkt. Mahanga amewataka badhi ya wanachama wenye nia ya kugombea udiwani na ubunge kuacha mara moja tabia ya kupitapita kwa wananchi na kuchafua majina ya viongozi waliopo madarakani kwa lengo la kujipatia umaarufu kisiasa.

  Alidai mbali ya kuchafua majina ya vingozi pia wanakwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kuwachanganya wananchi na kupoteza mwelekeo wao wa kushirikiana na viongozi katika shughuli mbalimbalia za maendeleo.

  Akifungua semina ya Jumuiya ya Wazazi katika Kata ya Ukonga, Dar es Salaam juzi, Dkt. Mahanga alisema ni vyema wanachama wa CCM, wakatumia muda huu kuweka mikakati ya namna chama hicho kitakavyoibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

  "Wapo baadhi ya wana CCM ambao tayari wameanza kuwapitisha wagombea wao kwa wananchi ili kufanya kampeni za ubunge mwakani, hatukatai watu kujitokeza kugombea kwani ni haki yao kidemokrasia lakini ni lazima kanuni na taratibu za uchaguzi za CCM zifuatwe kwa maana ya muda wa kuanza kampeni hizo," alisisitiza Dkt. Mahanga.

  Alisema kuwa tatizo kubwa linalofanywa na wagombea hao ni kupita kwa wananchi huku wakitoa kashfa kwa viongozi ambao bado wako madarakani nakuwataka kuacha mara moja tabia hiyo na kujikita katika kumaliza kero za wananchi zilizobaki katika kipindi hiki.

  Dkt. Mahanga alisema kuwa, vitendo vya kuchafuana kwa sasa vitasababisha kukwama kwa utekelezwaji wa Ilani ya CCM, ambapo kiongozi aliyepo madarakani anatakiwa kushirikiana na wananchi wake katika utekelezaji huo.

  "Kuanza kuvutana kwa sasa ni kupoteza dira kwani uchaguzi ni mwakani hivyo ni bora tukajikita kwanza kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na sio kuweka nguvu katika uchaguzi ambao muda wake bado, lakini wanaotumia jina la Mbunge kusaka udiwani hilo nalo pia ni tatizo linaloweza kunigombanisha na wanachama wangu, haya mambo tuyaache kwanza," alionya Dkt. Mahanga.

  Naye Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji, Bw. Ahmad Mkude, alisema kuwa vitendo vya watu kupita kwa wananchi huku wakiharibu majina ya viongozi, si sahihi hivyo aliwataka wanajumuiya hiyo kuwa makini na watu hao.

  "Hawa watatugombanisha na viongozi wetu, tunatakiwa kuwa makini zaidi na sio kusikiliza maneno ya watu bila kuangalia wamefanya nini ndani ya jamii yetu, wanatakiwa kuja kwa hoja lakini si kwa kashfa kwa kiongozi aliyepo na tukiendekeza itatugawa na madhara makubwa yatatokea ndani ya chama chetu," alisema Bw. Mkude.
   
 2. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mweh! tufwile!
   
 3. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ukabila mbeya umezidi!!! ACHA TU WAENDELEE KUTWANGANA! INGEKUWA KAMA WANATWANAGANA KWA SPIDI HII KUTETEA MAENDELEO YA TAIFA, BASI HAKIKA LEO HII TUNGEKUWA MBALI ! Mzee six mwenyewe anakwambia, speed na viwango, LOL! So, wazazi endeleeni tu kutwangana !
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sasa hapa jumba bovu linamwangukia Mwakyembe au wabaya wake??? mbona kama hao wote wamemkashifu mwakyembe then hata yeye si shwari sana huko kwao?

  Mh siasa za bongo kwa kweli zinataka moyo... sometime ni bora kutafuta nama ya kuifanya siasa kuwa haina high profile kwa maendeleo yetu

  HAO WALIOITWA MKUTANO, HAWAKATHIRI UZALISHAJI KWA SIKU HIYO KATIKA NYANJA WALIZOMO??

  NA SIKU HIZI HATA VIJANA VERY INTELIGENT NA PRODUCTIVE NAO WAMEJIINGIZA HUMO KWENYE MICHEZO YA MAIGIZO

  SHIT!!!!

  INAUMA SANA MJOMBA KUTUMIA KURA ZETU KAMA MAZALIO YAO
   
 5. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kule speed ya maendeleo ni kubwa sana. Ndiyo maana wanatwangana. Ukilala lala huwezi kumbuka kumtwanga mwezako anayeongea mbofu mbofu
   
 6. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Hiki ni kiswahili au External :)
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kutwangana kwa wenyewe kwa wenyewe ni dalili ya CCM kuporomoka kama chama chenye maadili. Kama ufisadi ukishaingia, unategemea uadilifu na uvumilivu kuwapo?

  Kuna tofauti gani na chama cha Mrema? Wanatwangana kule kwa kugombea ruzuku -- ni ufisadi tu. Juzi Tambwe Hiza alivikandia vyama vya upinzani kwa mambo kama haya -- hivi sasa atasema nini kuhusu chama chake alichokipiga teke na kukirudia?
   
 8. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sijaelewa au mimi ndio sijui maana ya ukabila. Waliotwangana ni watu wa wilaya ya kyela na wote ni wa kabila moja. Kama wote ni wa kabila moja, kinachowagombanisha ni ukabila au kitu kingine?
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na watangwana sana mwaka huu (serikali za mitaa) na mwakani (uchaguzi mkuu)
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Na wanatwangana kikweli ila habari zinakuwa wanazifichaficha lakini kuna mapigano na sio mapigano bali kuna makonde sasa fikiria mwenyewe ,halafu jamaa wanaambizana kama tuone kama kiti cha ubunge utakikalia ,kwa maana atamnunulia viungo vya binadamu kwa bei yeyote.
   
 11. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  sijaelewa katika haya makundi waliokuwa pro Mwakyembe ni akina nani? na hao waliohongwa pesa za kampeni ni kina nani? isije ikawa kuna mkono wa rostam aziz hapa, hawa wahindi watatuvuruga sana mwaka huu.

  HII NI NCHI YETU, TUSIKUBALI KAMWE KUKATANA MAPANGA KWA VISENTI VYA MAFISADI
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Jamani Rostam Azizi si mhindi ,wahindi na wairani picha haziendi kabisa ni watu mbalimbali na mambo yao hayalingani wala hawashirikiani ,matajiri wengi wa kihindi ni mahindus na huyu ni mpiga kifua shia wa kiirani.
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Siasa za kyera zaidi uuavyo.....waachieni wenyewe wa kyera wameshaizoea....
   
 14. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  kama huwajui watu wa mbeya mzee, haya. uliza uambiwe !
  turudi kuleeeeee-- mwakyembe vs mwakipesile!
   
 15. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mwakyembe Vs Mwakipesile wote wanyakyusa. Sasa kinachowagombanisha ni ukabila au ni kitu kingine? Ingekuwa mwakyembe angekuwa msafwa halafu Mwakipesile mnyakyusa hapo mi ningekuelewa.
   
 16. E

  Engineer JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu mgogoro ulianza kama wiki mbili zilizopita. Kulikuwa na kikao cha CCM wilaya na mbunge akiwa mjumbe. Mbunge alipopewa nafasi ya kuongea aliwashambulia wajumbe na kudai wanamwomba mwomba pesa kisa wanamsaliti, wamehongwa lakini yeye hawamuwezi na hawezi kushindana na wajinga ambao hawajui kitu na kwamba yeye anashindana na Rostam. Baada ya hayo maneno hao watu wa CCM walichukia na kuanza kuguna na kuzomea.

  Baadaye Mwenyekiti wa CCM kwa kushirikiana na katibu wake wakaitisha kikao cha maadili na kuwatuhumu hao wajumbe waliotajwa kwenye hiyo makala kwamba wamemkashifu mbunge. Waliposomewa mashitaka yao ndio wakaanza kuhoji mbona mbunge ambaye naye aliwatukana hajaitwa? Baada ya hapo wakaanza kutembeza mikono wakidai wamechoka kutukanwa kwamba wamehongwa wakati hakuna ukweli wowote. Pia walikuwa wanamtuhumu mwenyekiti wao kuhongwa pikipiki na Mengi kupitia kwa mbunge. Mimi nimeiona hiyo pikipiki mpya (hizo za India) lakini sijui kahongwa au kanunua kwa pesa zake.

  Hapa Kyela mambo hayako sawa kabisa na tutashuhudia mengi mno kabla ya hiyo 2010. Kuna mengi tu hatuandiki maana watu watasema tunamwandama Mbunge na tumetumwa na Rostam.

  CCM imemhamisha huyo katibu mara moja na kumpeleka Mbeya vijijini. Pia wameamua kesi isipelekwe mahakamani, kwa kifupi hakuna kesi tena. Sijui hiyo nguvu ya kuwaamuru polisi wasipeleke kesi mahakamani wameitoa wapi?
   
 17. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kazi kweli kweli! afadhali tuanzishe boxing team labda wengine watafaidika kuliko kutwangana mangumi shauri ya wanasiasa uchwara.

  Ujinga na njaa vikukutana huwa balaa kabisa!

   
 18. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mikoa ya kusini imechoka na ujinga unaoendelea ndio maana sasa wanademonstrate kwa wapindisha mambo, That's fine
   
 19. O

  Ogah JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kwi kwi kwi kwi kwi kwi..........unajua nilifikiri Dada yangu alikuwa akisingizia tu....kuwa anapigwa pigwa na shemeji.........aroo this time nikisikia tu Dada yangu kapigwa kutawaka moto........
   
 20. M

  Mtuwamungu Senior Member

  #20
  Apr 21, 2009
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hi Ogah, ukisikia dada kapigwa utafanyaje? Utamfuata shemeji au nawe utampiga dada wa shemeji yako uliyepanga naye bed-room moja?
   
Loading...